Ndugu mleta uzi. Upo sahihi but napenda uniruhusu kuwasilisha maoni yangu kama ifuatavyo.
Mtazamo wa maisha ni jambo very tricky sana usipokuwa makini na maamuzi yako unapoamua kufanya mabadiliko ya maisha.
Kuishi kwa unafuu ni jambo moja zuri ila kwa upande mwingine si jambo lenye faida sana ukitazama in the long run.
Hebu watazame kama wahindi wenzetu mathalani..... Wanaishi maeneo gani?! Umeaona bunju, umewaona tegeta umewaona Chanika.....?!
Wanaishi upanga, kwenye flats na apartment na nyumba za national housing. Na ndio wanampunga kutishinda sisi tunaojiita wajanja......
Siri moja kuhusu maisha, ukitaka unafuu wa chini ya tabaka lako (comfort zone) basi jiandae kushuka daraja.
Mfano, umeona kulipa 350,000 ni mzigo na ingawa umeweza kumudu basi wewe unaanza kuishi early retirement wakati haupo katika huo umri wa kuretire. Hayo ni mawazo anatakiwa kuwa nayo mzee wa miaka 85+ ambaye anahitaji utulivu wa kuishi miaka iliyosalia kwa kupumzika na kucheza na wajukuu.....
Kijana wa miaka 20 hadi 70+ unasemaje kuwa unakwenda kujenga nje ya mji kutafuta unafuu wa maisha...... C'amon?!
Nikwambie tu, maisha yanataka katika kila stage unayo graduate au kufika basi usichukulie ndio hitimisho, bali hiyo ni stepping stone ya the following phase ya maisha.... Tena ushukuru umefika hapo kuna mtu akiona wewe unalipa laki tatu na nusu ya kodi anakuona mharibifu sana wa pesa. Sababu yeye ameshajilimit kuwa hatopanga nyumba zaidi ya kodi ya 30,000 kwa mwezi. Huyu mtu unamuonaje hivi?!
Ipo hivi, pesa ndio maana inaitwa "Currency" kutokana na neno CURRENT ambalo humaanisha mkondo. Ukitaka pesa sharti maisha yako yawe na value pesa itakufuata. Kama ninachosema ni uongo tazama uhalisia hivi ukiwa na maisha ya kubana bajeti kesho ukafa ndugu wakagombania muounga wako unakuwa umeacomplish nini kwa mfano?!
Unajua kuna mtu unamfuata unamwambia brother naomba unazime 500,000 chap hapo jibu lake ni okay nikutumie kwenye namba gani?! Unajisikiaje kuongea na mtu wa hivi?!
Mwingine hata elfu 20 tu ataingia kwenye wallet atatoa chap atakupatia.
Mimi as a business person nitavutiwa sana kuongea na mtu anaendesha gari ya wastani 2000, anaishi nyumba ya kupanga hata kama ni 200,000 au 350,000, **** the price what matters upo comfortable na unaishi kwa nafasi nzuri. Ana budget nzuri na haogopi kufikiria chanzo kipya cha mapato kila baada ya miezi kadhaa. Hii itanipa picha kuwa huyu mtu ana discipline ya pesa na anajiamini na yupo positive financially.
Vijana wengi wa bongo atatoka kodi ya chumba kimoja, ataenda chumba na sebule, akishatiana mimba na mwenzake wakapata tutoto tuwili watakodi kanyumba ka vyumba vitatu then wataanza ujenzi wa nyumba nje ya mji then wakishamaliza wanahamia story imeisha wanajiona ni wazee wameshamaliza maisha, watu wa namna hii huwa hata kuongea nao naona kero maana wanajiona safari ya maisha wameifika na wanasubiria wajukuu na uzee ufike wadedi picha liishe.
Hivi mnaona wenzetu rangi nyeupe wanavyofanya?! Wakati sisi goal yetu na accomplishment kubwa na ya mwisho ya average Tanzanian youth ni kuoa, kupata watoto, kujenga nyumba yenye fremu mbele ya fensi huko nje ya mji, kununua gari, kuwa na shamba mlandizi au chanika la kulima viazi gunia mbili, na kuokota maembe kiroba kimoja kisha kuendelea kuishi tukisubiria uzee utuvae huku tukisomesha watoto kwa hela za pension na kujiuguza magonjwa kama kisukari na pressure sababu ya stress za retirement era,..... Tazama wenzetu race nyingine wanafanyaje huo umri?!
Average white race person goal yake kubwa ni kuishi standard ya maisha itakayompa privilege ya kubakia kuwa superior race no matter what it costs. Amini nakwambia hakuna kitu kama gharama katika haya maisha ila kuna choice za gharama gani unataka maisha yako yawe evaluated.
Unataka kuishi maisha ya free from everything?! Yaani mtu anakwambia anajenga ili kukwepa kulipa bili za makazi kama kodi?! Seriously?! Nani alikwambia kuishi katikati ya mji huku unalipa kodi ni sumu ya kufeli maisha....?!
Its okay to own a piece of land ila huwa nashangaa mtu anakimbiaje maisha ya kupambana for the luxury of the comfort zone?! Comfort zone ndipo watu hujitengenezea hell ya uzeeni. Hivi hawa wazee wote wanaodedi kwa pressure, kisukari, msongo wa mawazo, wengi si huwa wana majumba yao ya kuishi, shida huwa ni nini unadhani?!
Ni financial freedom hakuna. Mtanzania average anapoanza kupata access ya kutoka katoka tabaka la chini kuingia la kati anaanza upuuzi huu wa kuishi maisha ya kizee na hatimae kurudi nyuma badala ya kukaza zaidi na kubadili mbinu ilikuwa 100% tabaka la kati yaani tabaka six figures income every month na kurudi chini kwenye tabaka la three to two figures a month.
Walipo wahindi ndio na sisi tunatakiwa kuwapo. Wahindi sasa hivi ni sehemu ya kabila la kitanzania maana wapo waliozaliwa hapa. Why tusiwaige njia zao na sisi tusione shida kwenda kupanga pale upanga kwenye apartments tunaishi maisha ya popo huko vingunguti.
Ukienda nje ya mji barabara mbovu, gari zinaumia, mafuta uhitaji utaongezeka , gharama za vipuli vya gari na services vitakuhusu, plus unaenda kukaa nje ya mji utatakiwa kurejea home mapema sababu ya umbali, pia ni ngumu kuwa karibu na wazee wa connection kupeana connection.....
Nadhani hili hebu tulitazamie upya..... Kila kitu kitawezekana ndani ya muda na sisi tukiwa watu wa kujiongeza na changamoto zetu......