Hii style nimeiona kwa wengi mjini

Mtu mwenye uwezo wa kulipa kodi ya nyumba laki 3 na nusu kwa mwezi uchumi wake ni mzuri asee ningekuwa mimi nahamishia maisha pembezoni mwa mji ambako maisha ni nafuu ndani ya miaka 5 ntakuwa nshajenga.

Japo kupanga ni kuchagua.
Ukikaa huko nje ya mji wakati una crown athlete unajikuta upo pale pale...
 
Mtu mwenye uwezo wa kulipa kodi ya nyumba laki 3 na nusu kwa mwezi uchumi wake ni mzuri asee ningekuwa mimi nahamishia maisha pembezoni mwa mji ambako maisha ni nafuu ndani ya miaka 5 ntakuwa nshajenga.

Japo kupanga ni kuchagua.
Ila siku zote, mpangaji, hapendi kupanga, sehemu ambayo inamgarimu sana, kwenda kwenye, shuguri zake, na kurudi nyumbani.
Wapangaji wengi utasikia nataka karibu na barabarani.
 
Puna, Pembamnazi kote shamba ila kuzuri sana ukiwa haswa na usafiri. Hakuna foleni!

Everyday is Saturday.............................. 😎
Ila ni 70km kutoka Kigamboni kwaio kwenda na kurudi ni 140km x 5 days = 700km kwa mwezi ni 2800km hio gari itakua inaenda service kila mwezi aisee..hapi sijapiga hesabu ya mafuta...
 
Umeongea uhalisia. Safi sana.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 

Hawa wanaodai hawawezi kukaa kwenye pagare, wenzao wakistaafu wana nyumba sehemu ishakua mjini frame za maduka anazo, anakisima cha maji anayauza, anapiga tofali anauza, ana maturubai na viti anakodisha. Bonge la alwatan. Pensheni inakua ya kununulia vocha na kulipia azam.

Wewe unafuatilia penshen ndiyo uanze kujenga. Mipango kama mia hv pesa inakata.
Unafia nyumba ya kupanga. Unasumbua watoto tuu.. ooh msiba shughuli zote tutamalizia msikitini kumbe nyumba huna. Aibu tupu.
 
Hata mimi nilichukua miaka kadhaa.
 
Mzee wangu alinunua kiwanja tuangoma,ukubwa wa eneo 2100 square meters for 1.2M vikiwa vimepimwa na serikali tayari kati ya 2006-2008, akaanza kujenga mdogo mdogo, niliwahi kupaona mara ya mwisho mwaka 2009, akiwa kaezeka na kupiga madirisha ya wavu tu. Mimi nilipaona porini, hakuna umeme wala maji, akachimba kisima chake hapo, nyumba ya karibu ipo mbali sana. Nimerudi january 2021(miaka 12 baada ya kuwa mikoani mfululizo) nilibaki nashangaa tu, maghorofa kila kona, umeme, maji na huduma zote zinapatikana. ndo nikajua huyu jamaa alikuwa anaplan parefu sana.
 
Alone kabisa...Alikua na ka girl friend ila kamempiga chini last week [emoji23][emoji23] yeye anasema anapend kuishi quality life sio life bora mradi tu

Duh bado ana akili za ujana sana
Anyway with time ata badilika japo inaweza kuwa kwa kuchelewa
Dogo anaenifata nae ana mambo kama hayo ya quality life mpaka maza kaingilia kati mshahara ukitoka kuna percent anampa kwa lazima ameanza kujenga,yani ni kwa mbinde mpaka wamefika hapo
Huyo jamaa anahitaji guidance labda pengine ni wa kishua kila kitu kipo
 
Nyumba zipo za 25m unaifanyia finishing kiasi unajngia, sema wengi wanagaka kiwanja Mbezi Bunju n.k ambapo ni ghali sana
Viwanja si vipo Chanika pia πŸ˜‚ au Vikindu tena vya bei rahisi sana. Million 5 unapata uwanja wa kujigaragaza 😁 ila ndio mbali balaa 25KM+
 
Sema sasa nje ya mji kwa sasa utapelekwa mbali mnoo..sio chanika tena ni mkuranga hko au tuseme kigambon ndani ndani hukoo 😁
Huwezi kupata kwanja cha million 6 bila kuwa 30KM+ toka city center.

Kigamboni yenyewe utaambiwa kiwanja kiko 25KM toka darajani. Ukienda upande wa Morogoro Road unazungumzia mbele ya Kibaha ambako ni 30KM+

Ukija Bagaomoyo road Labda bunju ambako nako ni ishu kupata kiwanja sasa. Unazungumzia 25KM+! Goba nako ni ghali sana na hamna tena kiwanja ukibahatisha ni 10M plus na hicho ni high density.

Inshort tumefikia ule wakati ambao kupanga karibu na kazini ni less costful kuliko kuweka mafuta ya gari daily na kulipa kodi.
 
Sehemu zote hata Mbweni palikuwaga mashambani miaka ile ya 2003-2004 ila leo, 2020 ni kama Beverly Hills ya Bongo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ maamuzi ambayo mtu angeweza kuyafanya 2008 tu yangekuwa na manufaa sana leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…