Hii style nimeiona kwa wengi mjini

Eeh chukulia mtu ana Mshahara wa 12M kila mwezi huyu anajengaje kwa uchungu sasa? Maana hata akisema avute 100M ya Chap hapo NMB ana uhakika wa kuipewa fasta sababu sio rahisi ku default.

Hata ukiwaambia wakate 6 kila mwezi ndani ya 3 yrs deni limeisha na life linaendelea kama kawaida. Hawa ndio wale wa kuporomosha kitu mwanzo mwisho. Anakamata ground ya 20M fasta akianza hapoi mpaka anahamia ndani ya miezi 6 tu.
 
True man...iko waz
 
Ahahhaha....sema namuan sna.Gym ni collosium hotel na akina Mo.😎.. jogging asbh company zake akina salama jabir ..😁..apartment yake ya kwanza ku rent majiran zake ni akina wolper 😂 hapo nisikutajie mambo mengine.. kifup namkubali 😆 ..anasema atajenga hata akifa
 
Atakuja kukumbuka shuka pamekucha, unless awe na mshahara wa level za UN!

Ila kama ni lile kundi la 2.2M kwa mwezi namtakia kila la heri, tukutane 45 yrs hapo akiwa na watoto wawili na mke mpenda starehe!
 
Hawa ndio wanaobwiaga unga, ghafla mkataba umeisha. No more coloseum, no more butters, wana wote wamekata bogi 😂 utajua hujui.
Hapo kazungukwa na marafiki wa uongo, wanamnywea na kumlia hela, wanam-mwambafayi, anajiona Don, ngoja mambo yabadilike, 😂 😂 atatamani hata ajiunge na kanisa la Don Nalimison, awe muimba kwaya tu.

Everyday is Saturday................................😎
 
Sehemu zote hata Mbweni palikuwaga mashambani miaka ile ya 2003-2004 ila leo, 2020 ni kama Beverly Hills ya Bongo 😂😂😂 maamuzi ambayo mtu angeweza kuyafanya 2008 tu yangekuwa na manufaa sana leo.
Sahihi sana ujana unakataa mambo mengi ambayo ni manufaa uzeeni
 
Viwanja si vipo Chanika pia 😂 au Vikindu tena vya bei rahisi sana. Million 5 unapata uwanja wa kujigaragaza 😁 ila ndio mbali balaa 25KM+
25km kutoka wapi?
Kuna watu wana biashara/shughuli ambazo zinahamishika kirahisi na wanaweza kufanyia popote na faida ikawepo ila anakomaa kukaa mjini garama kubwa kodi kubwa na anaona kukaa chanika ni mbali wakati umuhimu wa kukaa kati ya mji haupo.
So unavyosema ni mbali itategemea na mishe zako au kazi zako.
Kuna watu wanakaa tabata ila posta sijui k.koo na samaki samaki.Next door mara 1 kwa miezi 4
 
Baba mdogo wangu alihamia dar miaka ya katikati ya 90! Life akaanzia Sinza, maisha yakawa Safi Sana, akataka kujenga akaenda kuoneshwa kiwanja Mbagala eneo la Zakhem pale! Akapaona bush Sana, anatokaje Sinza akajenge kijijini Mbagala! Miaka ya kuanzia 2010 akashtuka amezeeka life linaanza kuyumba, hawezi kupanga katikati ya mji, akaenda kupanga Mbagala Nzasa huko Mbagala ndani ndani! Ndio akili ikamjia inabidi ajitahidi ajenge, maeneo ya kujenga hakuna inabidi aende mbali zaidi!

Kahangaika Sana hatimaye akapata kakiwanja kadoooooogo hapo hapo Mbagala ndio kajenga yaani kadogo balaa, akikumbuka likiwanja aliloonyeshwaga pale Zakhem na akikumbuka ile bei moyo unamuuma anasema kilikuwa pembeni ya barabara tu, angeweka hata frame maisha yangeenda kuliko alipojenga saa hizi! Anasema kwa miaka ile hata huko Tabata huko sijui Chang'ombe, kisukulu kulikuwa bado na mashamba ya mihogo yaani angeweza kununua kiwanja kikubwa tu ila akaona mjini ni Sinza! Imekula kwake!

Bado nakua, bado najifunza!
 
Acha uongo banda hani la mil 20 kuku wa milioni 2. Kuna watu mnakuaga wachawi sana kwenye kushauri mtu . Sijui mnatokaga famikia za kishua sana au ndo kuhikweza tu.
Bila shaka umeanza kusikia kabla ya kusoma, sasa nakushauri anza kusoma mwenyewe kisha usimuliwe.

Wapi nimesema banda la milioni 20?
Unazijua gharama za kuwahudumia kuku wa biashara wewe!
Achana na hawa kuku vitoga, nazungumzia kuku wa biashara unawajua wewe.

Hilo banda hata ukisema la elfu50 ndio ufugie kuku wa kukupa faida?

Acha mihemko utapata tatizo la upumuaji, soma vizuri kisha km huna cha kuandika kukaa kimya nayo ni uungwana.

Andika vizuri kitu unachokusudia kuandika .
Sio HANI bali GANI
Sio FAMIKIA bali FAMILIA
Sio KUHIKWEZA bali KUJIKWEZA.

Uchawi wenu umepitia kwenye ushauri bila shaka.
Uwe na siku njema
 
Wahindi zile nyumba wanazoishi zilikua ni za kwao maana zilijengwa na babu zao ni vile tu Nyerere alibinafsisha nyumba zao,viwanda vyao na mashule yao kwa serikali.

Baada ya ubinafsishaji wahindi hawapendelei sana ku invest vitu kama nyumba maana walishaonjeshwa shubiri hapa Tz na Uganda,investment zao nyingi ziko in liquid(cash, money market funds, shares etc).

Pia wahindi hawajioni kama ni watanzania wengi wanajiona ni wahindi na wacanada zaidi na ndio huko wanakojenga majumba yao.Sasa hata wewe sidhani kama ungeona fahari kujenga sehemu unakooana sio kwenu.

So kufananisha wahindi na wabongo ni irrelevant.
 
Kuzikwepa hizo ndio utajikuta unanunua kiwanja cha 15*20 kwa million 20 eneo la 10KM kutoka ilipo ferry
Daah kanakuwa kadogoo kwelikweli, huwezi hata kuweka kigarden kupata oxygen [emoji256][emoji3515][emoji268][emoji269][emoji267][emoji271][emoji264]

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Akhela au kwa Mungu uko ndo kuna moto ndio sehem ya kuteseka kwa hyi binafsi siwezi kuteseka mara mbili dunian na akhela mbinguni/ nimechagua duniani nile maisha mazuri( bata) uko mbele hata nikichomwa moto sio mbaya
Hehe hehe unacheza na moto wewe[emoji23][emoji23][emoji16]

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…