Hii tabia imekuwa sugu; mtu anaamua tu aje Dar kukusalimia na afikie kwako

Nyie ndo watu JF huwa mnadai mna maisha mazuri sana humu....

Swali la kuwa na maisha mazuri au mabaya hakuna aliyelisema popote, nachosema sisi tunathamini ndugu zetu hata waje na magaga au bila viatu mjini.

Vyote tulivyonavyo ni Mungu ametupa tu kwa Rehema zake, tunaweza kuwa hao wa vijijini na hao wakawa wa mjini.
 

Siku zote hua namwomba mungu nimudu shida zangu, hua sitaki kumsumbua mtu na maisha yake na yeye asinisumbue.

Shida ya watu wakija kwenye nyumba wanakuja na mazoea ya walipotoka na akifika akakuta utaratibu fulani tofauti na alivyozoea anaona anaonewa japo kuonewa kweli kupo ila ni kwa uchache wengi wanasumbuliwa na huelewa mdogo.

Unakuta mtu keshazoea kula milo mitano kwa siku akija kwako akakuta milo mi3 nyama chache anaanza kujudge mbona mnaendesha magari ila chakula ndani hakuna mara mwanamke anaroho mbaya hatak tule..! na n.k.

Mi siwezi kukaa kwa ndugu, na ndugu wakija kwangu wafate utaratibu wangu hutaki left, binafsi ni bora nilale stand kwa ndugu ntapita kusalimia tu.
 
Magufuli hostel si zipo Coca[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hii kubwa kuliko,hawapeleki hata daraja la Mfugale wakashangae kidogo ndio awarudishe.....?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haina shida,ila mahusiano na watu wa kwenu,yawe mazuri na ujitahidi kuwatriti kama walivyo na labda kwa kuwavumilia baadhi ya tabia zinazovumilika.Yule dingi mtoto wa yule bibi,inasemekana alikua hana shida,ila mkewe ndo alionekana ana shida,matokeo yake yule dingi,akikuja kapata shida ya figo,na uwezekano wa kupewa na ndugu,ulikuwepo,lakini ndugu walikwepa hilo jukumu,dingi alifariki.Inasikitisha sana.Dingi yule anapigania afya yake,ndugu wanaongea yao,alifariki yule dingi.R.I.P niliwahi kwenda kwake,kumtembelea,pale Sinza,he was a good man indeed,nilipofika tumekaa tunaongea,kwasababu alijua mimi natokea kijijini kwake na anajua utamaduni wa kule,zililetwa ndizi za kupikwa,akamwambia mkewe,huyu hawezi kula hicho chakula,akafurahia,msongeeni ugali,nikasongewa ugali,nikala nikainjoi,jioni nikasepa zangu,kipindi hicho alikua anafanya dialysis.He was a a good man kwakweli.
 
Wacheni roho mbaya, hao wanakuja na kheri zao.

Wapokeeni bila masimango wala chuki, kwa bashasha na furaha. Siku tatu za mwanzo ni wageni, baada ya hapo waishi kama wenyeji.

Uislam mi mwema sana, haujaacha kitu. Uislam una miongozo mema kabisa ya maisha ya kila siku. Ukiifata huharibikiwi.
 
izo mambo kwa wachagga hamna iyo ki2!!!
 
Hata wewe πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…