Hii tabia imekuwa sugu; mtu anaamua tu aje Dar kukusalimia na afikie kwako

Uzi wako ni mrefu sana, kwa kifupi we ni maskini....
 
Kuna kipindi ndugu wa mke wangu walikua wengi mno home, nikiwa kijana mdogo kabisa ndio tunaanza maisha na wife.

Sijui walijua Mimi ni "Jesus" naweza walisha wote kwa kuombea tu Chakula kiji multiply.
Hongera sana kwa kupambana.
Binafsi napenda wageni, nipatapo changamoto ya mahitaji ya lazima kwa watu nilionao, hua akili inajikuza na kutafuta ufumbuzi kwa haraka,
Kwanza nisipate aibu.
Pili, wajisikie amani yapo na mtu sahihi.
Tatu, ni kipimo cha uwezo wangu wa maarifa. Wageni ni baraka.
 
Tatizo lenu watu wa Dar mkienda mikoani kwenu mnakua waongo sana, mnajisifia sana kila kitu duniani mnacho ninyi, mue wakweli
 
Huu uzi mzuri,umefungua baadhi ya watu,akili.Unapotoka mkoani,kwenda Dar,hatakama huendi kufikia kwa mtu,unaenda kufikia loji,labda ukae siku kadhaa,umalize mambo yako,urudi mkoani,jitahidi uwabebee hata debe la mchele,mihogo,mkungu wa ndizi nk. wakazi wa Dar.
Mpigie mwenyeji wako,aje AKIPATA muda,loji utakayokuwepo,mkabidhi hivyo vitu,bilashaka atafurahi hatakama hutofika kwake kutokana na kutingwa na shughuli zako,ila atafurahi.Inaonekana Dar,laifu siyo mchezo.
 
Tatizo ni kwama wakija mikoani wanatuaminisha wao kila kitu wanacho na maisha yao sio ya kula dona, wao ni piza, baga, yaani ni watu wa sosej, akila ndizi/mahindi basi ni ya kukaanga/kuchoma na anakula kwa chumvi na ndimu, sasa sisi ndio tunavutiwa na maisha mazuri ya Dar kwa Mjomba/Kaka, unajiuliza mi nikimchukulia mkungu wa ndizi si nitaenda kumchafulia kwake.
Hata hivi sasa tunawapigia simu tunaona bahari imehamia mitaani Dar, wanatuambia sio kweli, mvua ni ya kawaida na sisi tunaishi kwenye magorofa.
 
Shida hela....ila hata mimi hii siikubali
.mtu anavuruga maisha yake kwa kuzaa kupita kiasi sasa anataka akuharibie na wewe
 
Heheee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…