Hii tabia imekuwa sugu; mtu anaamua tu aje Dar kukusalimia na afikie kwako

Wengine wachawi wanaleta mikosi , nuksi majumbani mwa watu. Unawapokea wa nini?? Waache stendi na ujinga wao na ushamba, wanadhani mjini maisha ni marahisi
 
Ata aje mara ya kwanza kwangu simpokei. Utaendaje kwenye nyumba ya mtu bila kuitwa.. unajipangia mwenyewe kuja kwangu bila ridhaa yangu kwangu hutofika utaishia huko huko stendi
 
Vipi unazungumziaje wageni wachawi wanaoleta nuksi, mikosi, na chumaulete kwenye nyumba za watu.??

Kwa maisha ya sasa hivi usipende kumuamini mtu hata Ndugu zako usiwaamini , ukijifanya unajuwa kuwasaidia sana watakufanya shamba la nini kila mtu atataka afikie kwako. Mwisho wa siku unapigwa zongo la uchawi.
 
Mbona na nyie mnalalamika mkienda US au Ulaya, watanzania wanawazimia simu. Siwasapoti Ila taarifa ni muhimu pia zamani mgeni akija anakuja na zawadi kama chakula na sisi wa Kanda ya ziwa samaki.
Asee kwa ugumu wa maisha ulaya mm huwa nawapigia ndugu nikiwa nshalipia air bnb kabisa .kule huwa nafata yangu sio kukaa bure nawauliza lini watakuwa huru nije tule dinner .mchana nanunua groceries za kutosha kama nyama viungo pombe ndo nawatembelea Kisha naita tax narudi lala kwangu

Hata nikienda mkoani ni same .nampigia rafiki tukutane hotel nlipofikia .yy ndo ataamua kama aje na mkewe na watoto
 
Hiyo access na pesa za marehemu wanaipata wapi?
 
Mchawi ana alama Gani mkuu?tuanzie hapo
 
Nadhani msingi mkuu wa watu kufanya hivi sio hali ya umasikini kwani tulio wengi tumekulia na kuishi kwenye umasikini na hivyo hatuoni tabu kugawana hichi kidogo kwa jamaa zetu.......

Ukakasi unakuja kwenye mabadiliko ya tabia na nyoyo za wanadamu....... ulimwengu huu wa sasa tumeshuhudia na tunaendelea kushuhudia matukio mengi ya ajabu yanayokuacha kinywa wazi yanayofanywa na watu tunaowaita ndugu na jamaa wa karibu kwenye makazi yetu.......

Hebu fikiria umemkaribisha mdogo wako ili umpe msaada wa kimaisha mara ghafla unakuta amekuharibia mtoto wako wa kiume.......

Kwa Dunia imeharibika na moyo wa mtu ni kiza kinene basi watu tumejawa shaka kiasi kwamba imekuwa kheri zaidi ujifungie ndani na familia yako........

Kwa nyakati hizi ni salama zaidi kwako ukimsaidia mtu hata akiwa mbali kuliko akiwa karibu ingawa sio wote wana tabia mbaya.......

Vile vile pamoja na yote haya tuwe makini na vinywa vyetu katika kuwanenea watu maana maisha ni safari ndefu na hakuna ajuaye kesho kitamtokea Nini.......

Tujiweke mbali na maneno ya kejeli na dharau kwa ndugu jamaa na marafiki zetu kwani ya Mungu ni mengi na sio wote wenye tabia mbovu.......

Hatupaswi kuishi kama kisiwani bali tunapaswa kushirikiana na watu lakini umakini unatakiwa kutokana na nyakati tulizo nazo.........
 

Una roho nzuri,Mungu asikupungukie
Mkono utoao hupokea zaidi[emoji1488]
 
Atakuwa msukuma huyo......samahani lkn watani zangu
 
Shida kubwa watu hawana nguvu za Mungu. Kama una nguvu za Mungu utaishi na kila mtu hapa duniani. Ukiogopa uchawi utaishi kwa hofu sana. Jambo kubwa watu bado ni maskini ila wanajiona matajiri kwa sababu ana nyumba na gari. Kama una financial freedom utamuona mgeni ni kama fursa ya kukuinua zaidi.
Jiulize toka unakuwa, ulitumia pesa yako pekee katika malezi yako utotoni hadi ukubwani?.
 
Huko dar mpo bize na nini hasa???

Maana naona kitu kinachowapa ubize zaidi ya gombania daladala,
Nakubali....imagine Mtu anaamka saaa kumi na moja lakini hadi saa mbili asubuhi bado yuko bize na Daladala za kwenda Posta na hajapata......kurudi tena hivyo hivyo daily.
Mtu kwa siku anapoteza kuanzia masaa 2 hadi 6 ktk harakati za kwenda na kurudi kazini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…