Hii tabia imekuwa sugu; mtu anaamua tu aje Dar kukusalimia na afikie kwako

Hii tabia imekuwa sugu; mtu anaamua tu aje Dar kukusalimia na afikie kwako

Hawa wabush huwa wanarahisisha sana maisha. Mtu kama huyo unampokea. Unamwacha home anashinda na watoto. Keshokutwa unakuja sikia mtu kalawitiwa au kanajisiwa unalaumu. Kumbe unakaribisha watu ambao hawajui hata kilichowaleta Dar ni nini. Jirani yangu mmoja mtoto wake alinajisiwa na ndugu yake katoka kijijini amekuja town ili amtafutie kazi za kutumia nguvu. Jamaa anashinda home anakula vizuri. Watoto uncle uncle. Kumbe akaanza kukanajisi katoto ka mia 6 ka mwenye nyumba. Kuja kugundua too late.
Wengine wachawi wanaleta mikosi , nuksi majumbani mwa watu. Unawapokea wa nini?? Waache stendi na ujinga wao na ushamba, wanadhani mjini maisha ni marahisi
 
Nani anakusumbua wewe kinachokusumbua wewe ni umaskini wako na gubu lako Kwa ndg zako
Mtu anakuja mara Moja Tena Kwa miaka kadhaa umzimie simu au umuache stendi ? Kama sio umaskini wa kiwango Cha lami Ninini? Mchukue mweleze abc akirudi atawaambia na wengine
Ata aje mara ya kwanza kwangu simpokei. Utaendaje kwenye nyumba ya mtu bila kuitwa.. unajipangia mwenyewe kuja kwangu bila ridhaa yangu kwangu hutofika utaishia huko huko stendi
 
Ukiona unachukia wageni ujuwe bado huna sehemu / chumba cha ziada mgeni kulala. Dsm wanachukia kwa sababu hakuna room za wageni. Kwenye changamoto kubwa ndiyo utajua umuhimu wa ndugu zako.

Mhubiri 5:11
Mali yakiongezeka, hao walao nao waongezeka na mwenyewe hufaidiwa nini, ila kuyatazama kwa macho yake tu?

When goods increase, they are increased that eat them: and what good is there to the owners thereof, saving the beholding of them with their eyes?
Vipi unazungumziaje wageni wachawi wanaoleta nuksi, mikosi, na chumaulete kwenye nyumba za watu.??

Kwa maisha ya sasa hivi usipende kumuamini mtu hata Ndugu zako usiwaamini , ukijifanya unajuwa kuwasaidia sana watakufanya shamba la nini kila mtu atataka afikie kwako. Mwisho wa siku unapigwa zongo la uchawi.
 
Mbona na nyie mnalalamika mkienda US au Ulaya, watanzania wanawazimia simu. Siwasapoti Ila taarifa ni muhimu pia zamani mgeni akija anakuja na zawadi kama chakula na sisi wa Kanda ya ziwa samaki.
Asee kwa ugumu wa maisha ulaya mm huwa nawapigia ndugu nikiwa nshalipia air bnb kabisa .kule huwa nafata yangu sio kukaa bure nawauliza lini watakuwa huru nije tule dinner .mchana nanunua groceries za kutosha kama nyama viungo pombe ndo nawatembelea Kisha naita tax narudi lala kwangu

Hata nikienda mkoani ni same .nampigia rafiki tukutane hotel nlipofikia .yy ndo ataamua kama aje na mkewe na watoto
 
Mkifa mitoto yenu inarudi mikoani kunyanyaswa......ndugu mliowaita wanoko hamuwataki wanachukua Mali zote ulizochuma....mke wa marehemu akishtaki, ndugu hutumia pesa za marehemu kushinda kesi....Hapo marehemu umelala kimya kaburini. Hii ndiyo dunia mkuu
Hiyo access na pesa za marehemu wanaipata wapi?
 
Vipi unazungumziaje wageni wachawi wanaoleta nuksi, mikosi, na chumaulete kwenye nyumba za watu.??

Kwa maisha ya sasa hivi usipende kumuamini mtu hata Ndugu zako usiwaamini , ukijifanya unajuwa kuwasaidia sana watakufanya shamba la nini kila mtu atataka afikie kwako. Mwisho wa siku unapigwa zongo la uchawi.
Mchawi ana alama Gani mkuu?tuanzie hapo
 
Nadhani msingi mkuu wa watu kufanya hivi sio hali ya umasikini kwani tulio wengi tumekulia na kuishi kwenye umasikini na hivyo hatuoni tabu kugawana hichi kidogo kwa jamaa zetu.......

Ukakasi unakuja kwenye mabadiliko ya tabia na nyoyo za wanadamu....... ulimwengu huu wa sasa tumeshuhudia na tunaendelea kushuhudia matukio mengi ya ajabu yanayokuacha kinywa wazi yanayofanywa na watu tunaowaita ndugu na jamaa wa karibu kwenye makazi yetu.......

Hebu fikiria umemkaribisha mdogo wako ili umpe msaada wa kimaisha mara ghafla unakuta amekuharibia mtoto wako wa kiume.......

Kwa Dunia imeharibika na moyo wa mtu ni kiza kinene basi watu tumejawa shaka kiasi kwamba imekuwa kheri zaidi ujifungie ndani na familia yako........

Kwa nyakati hizi ni salama zaidi kwako ukimsaidia mtu hata akiwa mbali kuliko akiwa karibu ingawa sio wote wana tabia mbaya.......

Vile vile pamoja na yote haya tuwe makini na vinywa vyetu katika kuwanenea watu maana maisha ni safari ndefu na hakuna ajuaye kesho kitamtokea Nini.......

Tujiweke mbali na maneno ya kejeli na dharau kwa ndugu jamaa na marafiki zetu kwani ya Mungu ni mengi na sio wote wenye tabia mbovu.......

Hatupaswi kuishi kama kisiwani bali tunapaswa kushirikiana na watu lakini umakini unatakiwa kutokana na nyakati tulizo nazo.........
 
Mambo mengine ni kuendekeza uchoyo tu jamani tufike sehemu tuongee ukweli kabisa, unamkimbiaje ndugu yako?? Rafiki yako?? Eti tu kisa maisha yako hayajakaa sawa?? Mimi Nina chumba na sebule na mgeni akija namfuata mbezi namtandikia godolo sebulen mim na nke wangu tunalala chumbani, kama mgeni ni mwanaume asubuh naamsha naye kwenye mishe mishe zangu, kama ni wa kike anabak na wifi yake, huyo mgen atakaa siku alizopanga yeye kukaa sio nimpangie maana hata safari sikumpangia. Akiomba nimzungushe town navunja ratiba zangu ili asafishe macho.

Kumbuka kila ntu anapenda kuja dar na hasa akiwa na ndugu huku anakuwa huru kwasababu anajua ana mwenyeji tuwe wapole tu chakula tuuuu kisitutoe imani, kama Ni kusemana sijui kumsema mke hayo hayawezi kuisha kwanini sisi hatuwawesemi??? Mbona kuyaandika hayo tayari umewasema?? Kuna mwanamke aliyeolewa akakosa kusemwa??

Una roho nzuri,Mungu asikupungukie
Mkono utoao hupokea zaidi[emoji1488]
 
Yalinikuta Jumapili alikuja mtu wa aina hiyohiyo nyumbani tofauti ni kuwa huyu aliletwa na ndugu yangu, alichonikera ni vile alipofikishwa tu akawa na kidaftari chake ameandika namba za watu wake anaojua wapo Dar, akaomba simu yangu na kuanza kuwapigia mmoja hadi mwingine mbaya zaidi akawa anawaambia uongo kuwa yupo ameekaa kwangu kwa zaidi ya mwezi, kilichonikwaza zaidi siku iliyofuata nimerudi toka mihangaiko yangu jioni nakuta sebule imejaa hao rafiki zake kama kuna kikao cha kikoba wamechukua vinywaji kwa jirani bila kunishirikisha bill ipo kwangu.
Atakuwa msukuma huyo......samahani lkn watani zangu
 
Vipi unazungumziaje wageni wachawi wanaoleta nuksi, mikosi, na chumaulete kwenye nyumba za watu.??

Kwa maisha ya sasa hivi usipende kumuamini mtu hata Ndugu zako usiwaamini , ukijifanya unajuwa kuwasaidia sana watakufanya shamba la nini kila mtu atataka afikie kwako. Mwisho wa siku unapigwa zongo la uchawi.
Shida kubwa watu hawana nguvu za Mungu. Kama una nguvu za Mungu utaishi na kila mtu hapa duniani. Ukiogopa uchawi utaishi kwa hofu sana. Jambo kubwa watu bado ni maskini ila wanajiona matajiri kwa sababu ana nyumba na gari. Kama una financial freedom utamuona mgeni ni kama fursa ya kukuinua zaidi.
Jiulize toka unakuwa, ulitumia pesa yako pekee katika malezi yako utotoni hadi ukubwani?.
 
Huko dar mpo bize na nini hasa???

Maana naona kitu kinachowapa ubize zaidi ya gombania daladala,
Nakubali....imagine Mtu anaamka saaa kumi na moja lakini hadi saa mbili asubuhi bado yuko bize na Daladala za kwenda Posta na hajapata......kurudi tena hivyo hivyo daily.
Mtu kwa siku anapoteza kuanzia masaa 2 hadi 6 ktk harakati za kwenda na kurudi kazini
 
Back
Top Bottom