Mambo mengine ni kuendekeza uchoyo tu jamani tufike sehemu tuongee ukweli kabisa, unamkimbiaje ndugu yako?? Rafiki yako?? Eti tu kisa maisha yako hayajakaa sawa?? Mimi Nina chumba na sebule na mgeni akija namfuata mbezi namtandikia godolo sebulen mim na nke wangu tunalala chumbani, kama mgeni ni mwanaume asubuh naamsha naye kwenye mishe mishe zangu, kama ni wa kike anabak na wifi yake, huyo mgen atakaa siku alizopanga yeye kukaa sio nimpangie maana hata safari sikumpangia. Akiomba nimzungushe town navunja ratiba zangu ili asafishe macho.
Kumbuka kila ntu anapenda kuja dar na hasa akiwa na ndugu huku anakuwa huru kwasababu anajua ana mwenyeji tuwe wapole tu chakula tuuuu kisitutoe imani, kama Ni kusemana sijui kumsema mke hayo hayawezi kuisha kwanini sisi hatuwawesemi??? Mbona kuyaandika hayo tayari umewasema?? Kuna mwanamke aliyeolewa akakosa kusemwa??