Hii tabia imekuwa sugu; mtu anaamua tu aje Dar kukusalimia na afikie kwako

Tafuta hela ndugu ili utamani kula na ndugu zako wakati wote... haya malalamiko yako ni ishara ya umaskini
Nikisoma na kuangalia sura yako ilivyokauka kama goti la kiwete... Sikuoni ukiwa na lolote pako pakavu utiliwe mchuzi. Unajipapatua lakini unanuka jasho tu na kikwapa. Na midomo yako imekauka utandani mikono ya mchoma mkaa.
 

Wewe uchoyo na roho mbaya tu vinakusumbua badilika.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Daslama tamuu bhana.
Siyo lazima wote tuende DSM [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Nakumbuka way back 2007/8 nikiwa nimemaliza std 7,nilikuja DSM Kwa mara ya kwanza ..ilikuwa mahafali ya sister hapo jalalani kwenu[emoji23]

Aisee nilishangaa magorofa...nilikuwa nahesabu simalizi[emoji1787]

Tulikaa wiki tunazunguka tu feri,Kariakoo,yaani nikasema nikirudi kijijini watanikoma..
Ukifika unajidai umebadilika kabisa hadi ongea[emoji23][emoji23][emoji23]

Wenzio wanakutamani umetoka Dar.



Ndugu zenu wakija DSM msiwafukuze..maisha ndo hayahaya.
Hata wakija bila sababu muwapokeee...wengine wanataka kupata exposure..
Kama tulivyopokewa,basina sisi tupokee wenzetu.
 
Umesema kwelii kabisaa....

Watu waliokuja dar kipind aaah walikuja dar


Kwanza wanakufanya km funny....

Mimi nilishangaa friji ukifunga linawaka, Mara kuwasha tv.... Em acheni bhn...

Siku hz unakuja dar kila kitu unacho uko mkoan
 
Umesema kwelii kabisaa....

Watu waliokuja dar kipind aaah walikuja dar


Kwanza wanakufanya km funny....

Mimi nilishangaa friji ukifunga linawaka, Mara kuwasha tv.... Em acheni bhn...

Siku hz unakuja dar kila kitu unacho uko mkoan
[emoji38][emoji38][emoji38]
Mambo ya Tv tayari yalikuwepo..nakumbuka miaka ya 2000 Baba anakuja na TV nyumbani aisee hatukulala.

Hapo ndio mziwanda unakabidhiwa rimoti,hakuna watu kushikashika hovyo,,enzi hizo tukaanza na Antena..deki za mikanda ile Mkubwa..
Tukaja kununua ungo..mambo ya kulipia hayakuwepo.


Ila Mimi maghorofa tu ndo nilishangaa Daslama aisee
Ukizingatia kule Mbeya miaka hiyo kulikuwa hakuna ghorofa refu hata moja.[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Nilihesabu ghorofa nikawa simalizi..
Sister ananisubiri.

Akatupeleka kupanda lift[emoji23]
Ni kivumbi.

Tukaenda feri kushangaa Panton.

Hapo ukirudi kijijini Toka Dar,wenzio wanakuja kukushangaa umetoka Dar...


Nyie,hebu tuwapokee ndugu zetu jamani.
Kikubwa watoe tu taarifa ili tufix ratiba za vibarua vya kausha damu.
 
Chumba kimoja na sebule....
Bila taarifa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
Oky hata ukitoa taarifa
SITAKI WAGENI
Si bora hata hiyo sebule ipo. Wengine tunakaa self... [emoji1787][emoji1787]

Mara ba demu anaweka weka kambi mara siku 3 mara siku 1 mara wiki.

Na mwingine yupo standa...

Jamani tupeane taarifa hata 1wk before
 
Una tabia za kimasikini we mwalimu
 
kila mtu aishi kwake kwa taratibu zake...Binafsi kwangu kwa ndugu/mtu yeyote anayenifahamu apige simu afikie kwangu muda wowote ule hata kama siku za kawaida huwa hatupigiani simu mara kwa mara ingawa wasukuma mmezidi.!!!
Hongera sana mkuu.

Kuna level ya mkuu, kuna level ya maisha ukifika you can have this freedom.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…