akajasembamba
JF-Expert Member
- Dec 24, 2010
- 1,179
- 1,794
Majority ya ndugu wakitoka kwako kuishi ni lawama tu na kukuchafua hawanaga shukurani hata kidogo, wakati ulijinyima na wanao kwa ajili yao.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nikisoma na kuangalia sura yako ilivyokauka kama goti la kiwete... Sikuoni ukiwa na lolote pako pakavu utiliwe mchuzi. Unajipapatua lakini unanuka jasho tu na kikwapa. Na midomo yako imekauka utandani mikono ya mchoma mkaa.Tafuta hela ndugu ili utamani kula na ndugu zako wakati wote... haya malalamiko yako ni ishara ya umaskini
Nyie mmekaribisha au mmekimbizwa?Watu wenye asili ya huko mikoani mnaokuja Mzizima huku mnanyanyasa saaana ndugu zenu,
Nyie tumewakaribisha bila ubaguzi ajabu nyie mnabagua ndg zenu wanaotaka kuja kusafisha macho hukuu
Hii tabia imekuwa sugu. Yaani mtu anakaa tu na halmashauri ya kichwa chake anaamua kuwa nimpigie jamaa yangu yupo Dar nikafikie kwake.
Mi nipo zangu home jana inaingia simu ya Abouu. Ananiuliza maisha vipi namwambia safi tunalisongesha. Maneno maneno mengi mwisho anasema nipo Dar nataka nije kwako nielekeze. Nikamuuliza wakati unapanga kuja ulinishirikisha? Unaamua tu kuja kwangu hata hujanitaarifu.
Jamaa ame mind kawaambia watu nimemkataa. Ninyi wa Mikoani mnadhani huku ni kama kwenu huko ambako hamna ratiba maalum. Mnajiamulia tu.
Mwaka juzi nlimwacha mtu stand kwa upuuzi kama huo. Kakaa zake Mbwinde mwisho kaamua kuja town a anipigia simu kuwa yupo Dar anataka aje home. Nlimwambia tu kuwa sipo home na familia tumesafiri.
Akaanza kuomba basi nimpatie pesa ya sehemu ya kulala anisubiri. Nilimwambia mwezi mzima sitokuwa home. Akataka nimtumie nauli. Nlizima na simu kabisa. Huu ni wendawazimu.
Halafu tukiwaakaribisha mnaenda kutusema kijijini kuwa huku tunaishi maisha mazuri sana hatuwajali watu wa vijijini. Mnaenda kutuponda sana kijijini kuwa tunatumia pesa vibaya.
Mimi walienda kusema nafuja sana pesa badala ya kuwasomesha watoto wao. Mtu kazaa watoto 13 anataka nimsomeshee... Mimi nina 3 tu. Bado wanaenda kusema nakuaje na watoto wachache ... Mwanaume gani. Mke amenikalia kichwani anarudi jioni kama mwanaume. Wanataka wife awafulie nguo zao. Na wanakuwa wakali akirudi awapatie chakula n.k sina hamu na ndugu kabisa.
Mmoja tumekaa naye mwaka mmoja amekuja nimsomeshe diploma. Akirudi toka chuo anaangalia TV mpaka saa 4 akipewa kazi basi za home siku yupo asaidie... Anasema anateswa sana hawezi soma. Nikasubiri likizo. Akaenda kwao kusalimia. Nikamwambia atafute chuo aendelee kusoma huko, nitamlipia ada.
Alilia sana anataka arudi Dar. Nilimwambia huku wifi yako atakutesa hutapata muda wa kusoma. Akabembeleza sana nilimkatalia coz alishanipakaza sana kijijini na kumchafua sana wife. Na mtu mwenyewe ni ndugu wa mbali kabisa..
HAWA WAGENI WENGINE NDO HUNAJISI WATOTO NA UNDUGU UNAISHIA HAPO HAPO. MNAHARIBIANA FUTURE. KILA MTU AKAE KWAKE. DUNIA YA SASA IMANI IMEKWISHA. TUSAIDIANE KATIKA SHIDA LAKINI SI KUVAMIANA TU NYUMBANI KWA KISINGIZIO CHA UKARIMU. NDUGU WENYEWE IMANI IMEWATOKA. ANGALIA WANAOBAKWA, NAJISIWA AU LAWITIWA. MHUSIKA UTAKUTA BABA, BAMDOGO, MJOMBA, COUSIN NA JIRANI KWA MBALI KIDOGO.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Daslama tamuu bhana.Mtoto ulikuwa unakimbilia Daslama kwA nini Coca
Kaa huko Mbinga[emoji23]
Yuko Ban.Kafanyaje tena maana kwa matukio nimemshindwa kila siku lokapu
Naomben id yake nyingineYuko Ban.
Siyo lazima wote tuende DSM [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Daslama tamuu bhana.
Umesema kwelii kabisaa....Siyo lazima wote tuende DSM [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Nakumbuka way back 2008 nikiwa nimemaliza std 7,nilikuja DSM Kwa mara ya kwanza ..ilikuwa mahafali ya sister hapo jalalani kwenu[emoji23]
Aisee nilishangaa magorofa...nilikuwa nahesabu simalizi[emoji1787]
Tulikaa wiki tunazunguka tu feri,Kariakoo,yaani nikasema nikirudi kijijini watanikoma..
Ukifika unajidai umebadilika kabisa hadi ongea[emoji23][emoji23][emoji23]
Wenzio wanakutamani umetoka Dar.
Ndugu zenu wakija DSM msiwafukuze..maisha ndo hayahaya.
Hata wakija bila sababu muwapokeee...wengine wanataka kupata exposure..
Kama tulivyopokewa,basina sisi tupokee wenzetu.
[emoji38][emoji38][emoji38]Umesema kwelii kabisaa....
Watu waliokuja dar kipind aaah walikuja dar
Kwanza wanakufanya km funny....
Mimi nilishangaa friji ukifunga linawaka, Mara kuwasha tv.... Em acheni bhn...
Siku hz unakuja dar kila kitu unacho uko mkoan
Umenena,kumbe shida ni chakula[emoji23],Ndiyo ni misos,kwa hyo bakini huko huko mikoani. Kama unakuja mjini fikia Nyumba ya wageni.SAWA?
Tafuta hela upunguze makasiriko nduguNikisoma na kuangalia sura yako ilivyokauka kama goti la kiwete... Sikuoni ukiwa na lolote pako pakavu utiliwe mchuzi. Unajipapatua lakini unanuka jasho tu na kikwapa. Na midomo yako imekauka utandani mikono ya mchoma mkaa.
Si bora hata hiyo sebule ipo. Wengine tunakaa self... [emoji1787][emoji1787]Chumba kimoja na sebule....
Bila taarifa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
Oky hata ukitoa taarifa
SITAKI WAGENI
Una tabia za kimasikini we mwalimuMkifa mitoto yenu inarudi mikoani kunyanyaswa......ndugu mliowaita wanoko hamuwataki wanachukua Mali zote ulizochuma....mke wa marehemu akishtaki, ndugu hutumia pesa za marehemu kushinda kesi....Hapo marehemu umelala kimya kaburini. Hii ndiyo dunia mkuu
Mentality ya kimasikini hii na kuendekeza ujinga na upumbavuTuwe wanyenyekevu tunapopata mafaniko tusione wengine ni takataka hawafai.
Ukifa ndio watamfariji mkeo na watoto wako
Hongera sana mkuu.kila mtu aishi kwake kwa taratibu zake...Binafsi kwangu kwa ndugu/mtu yeyote anayenifahamu apige simu afikie kwangu muda wowote ule hata kama siku za kawaida huwa hatupigiani simu mara kwa mara ingawa wasukuma mmezidi.!!!
Sasa Tarime kuna chakula gani au shida tuSisi wa mkoani tunapenda wageni, njooni tu bila taarifa. Hiyo inaonyesha kuwa basic needs hasa chakula ni shida kwa watu wa dasalaam
Huku chakula ni tele, hasa huku Tarime, hatupimii mtu chakula.
Ujamaa ndo sababu Tanzania ni masikiniHii ni dalili za maisha magumu sana. Mungu akunusuru, maana kulala na kula sio kitu cha kumzimia mtu simu.
Salamu mtu anapaswa aje kwa wakati maalumu, aje na matumizi yake.Tutafuteni hela ndugu ni baraka hasa wanao kuja kukusalimia ni maisha magumu na vipato vidogo vinatufanya tuwe na roho mbaya.Lakini hakuna kitu kizuri km ndugu kutembeleana