Hii tabia imekuwa sugu; mtu anaamua tu aje Dar kukusalimia na afikie kwako

Acha uoga wa kijinga. Mtu ashindwe kuishi maisha yake kwa kuhofia atakufa siku moja? Kuna ambaye hatokufa? Kama una mali unashindwa hata kuandaa wosia juu ya warithi wa mali zako?
 
Duuuh! nilirudi kijijini kwetu,nikakuta stori ya bibi mmoja,alienda kwa mwanae mjini,alinyanyasika Sana,hadi akaomba arudi kijijini kwenye maisha ya shida.Watu wa mjini msiwadharau watu wa kwenu,chakula tu au malazi ni nongwa...?
Anyway mnasubiriwa,mkifa mkazikwe huko vijijini,ambako wachimba kaburi mtawakuta haohao mnaowajandia,wasije makwenu.
 
Umeandika yote kwa usahihi lakini chanzo cha yote ni UMASIKINI NA BAJETI ULIYO NAYO ISIYONYUMBULIKA.

Mtu kuja kwako lazima atoe taarifa hili naunga hoja kwa 100% ndiyo mfumo wa maisha.

Lakini mtu anapokuja bila taarifa ameshakuja tayari, hatuangalii madhaifu ya kuja bila taarifa muda huo tunakabiliana na shida ya kuja kwake bila taarifa.

Mtu msitaarabu na mwenye uwezo na bajeti ya ziada ambaye hayana dhiki na umasikini, atamkaribisha mgeni atampeleka nyumbani, atampa maji,chakula na mengineyo, haijalishi utamlaza sebuleni, kwenye ukumbi wa nyumba, jikoni kwenye korido siku kwanza ipite.

Kukicha au ucku ule ule unamwambia nashukru umekuja lakini ulijisahau kuja bila kuniambia.

Kwangu hakuna nafasi kwa sasa ya kutunza mgeni hatakama nafasi ipo utatumia lugha ya kiutu.

Hivo utakaa hizi cku 3 kwa shida ili tutafute nauli urudi au kama una nauli ya kurudi itabidi urudi siku fulani.

Kama wote hamna nauli hilo sasa ni tatizo ambalo mtajadili kama familia wewe na ndugu zako huko alikotoka kuwa huku hakuna nafasi ya yeye kukaa na wote maisha ni magumu, uzeni mbuzi huko, kuku, bata, njiwa au gunia la mahindi mtume nauli arudi nyumbani.

KUMZIMIA MTU SIMU, KUMKIMBIA STAND NI DALILI ZA UBABAISHAJI, UJANJA UJANJA, UELEWA MDOGO NA UPUUZI.

Pokea simu mwambie ukweli bila kupepesa macho full stop.

Mwisho.

Umasikini ni kitu kibaya sana unaweza kuongozwa na umasikini huo ukahisi uko sahihi maamuzi yako kumbe tu ni umasikini.
 
Ninafikiria ni kwa jinsi gani ninaweza kuwa na roho ya kumtelekeza ndugu au rafiki yangu stendi??!!.... kwa jinsi nilivyokuzwa ni kuwa kutompokea kabisa kiasi cha kutompa hata hifadhi ya usiku mmoja ni dhambi kubwa na ikigundulika ni kesi nzito kuanzia kwa baba na mama mzazi. Tujitahidi tu kuwa wakarimu kwa wageni wetu bila kuchotwa sana na tamaduni za magharibi. Wewe mwache aje kisha mlaze hata bafuni kuliko kumtelekeza kabisa. Haya maisha hayana mjanja... mambo kama ajali, kesi mahakamani, magonjwa au jela yanaweza kubadili kabisa title yako na ukawa tegemezi kwa unaowatelekeza stendi.
 
Acha uoga wa kijinga. Mtu ashindwe kuishi maisha yake kwa kuhofia atakufa siku moja? Kuna ambaye hatokufa? Kama una mali unashindwa hata kuandaa wosia juu ya warithi wa mali zako?
Kinacholeta shida ni umaskini. Watu wengi wa mji ni maskini sana kiasi kwamba wanachokipata hakitoshelezi hata kwa familia zao tu. Pia utakuta baba, mama na watoto wanaishi chumba kimoja. Yaani balaa.
 
Semina nzuri, ili angalau hayo yawezekane basi hebu tumia nafasi yako kumwomba asikubali kila jambo analopelekewa mezani maana wanamharibia na matokeo yake maisha yanakuwa magumu mwisho tunakimbiana mjini
 
Tusameheni wakuu...

Siku nyingine tukitaka kuja huko Daslaam tutatoa taarifa mapema.

Saint Anne
 
Jamaa amezingua sana....ila msamehe bure tu, hajui atendalo.
 
Siku watakapoamua kukusafirisha hao ndio wachimba kaburi wagawa chakula kwenye msiba wako be humble brother..
 
Kama anakubana kwanini usimtimue..

Umaskini ni janga.
 
Mkuu usikimbie majukumu 😅😅..
Mpokee tu, kama mlivyokuwa mnaishi vizuri huko kijijini ishini vizuri tu na huko Mjini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…