Hii tabia imekuwa sugu; mtu anaamua tu aje Dar kukusalimia na afikie kwako

Hii tabia imekuwa sugu; mtu anaamua tu aje Dar kukusalimia na afikie kwako

Mkifa mitoto yenu inarudi mikoani kunyanyaswa......ndugu mliowaita wanoko hamuwataki wanachukua Mali zote ulizochuma....mke wa marehemu akishtaki,ndugu hutumia pesa za marehemu kushinda kesi....Hapo marehemu umelala kimya kaburini.Hii ndiyo dunia mkuu
Halafu cha ajabu wanawafukuza Nyumbani kwao ila ndo wasimamizi wa Mirathi yao wakifariki 😅😅😅
 
Yalinikuta Jumapili alikuja mtu wa aina hiyohiyo nyumbani tofauti ni kuwa huyu aliletwa na ndugu yangu, alichonikera ni vile alipofikishwa tu akawa na kidaftari chake ameandika namba za watu wake anaojua wapo Dar, akaomba simu yangu na kuanza kuwapigia mmoja hadi mwingine mbaya zaidi akawa anawaambia uongo kuwa yupo ameekaa kwangu kwa zaidi ya mwezi, kilichonikwaza zaidi siku iliyofuata nimerudi toka mihangaiko yangu jioni nakuta sebule imejaa hao rafiki zake kama kuna kikao cha kikoba wamechukua vinywaji kwa jirani bila kunishirikisha bill ipo kwangu.
🤣🤣🤣
 
Semina nzuri, ili angalau hayo yawezekane basi hebu tumia nafasi yako kumwomba asikubali kila jambo analopelekewa mezani maana wanamharibia na matokeo yake maisha yanakuwa magumu mwisho tunakimbiana mjiniView attachment 2800311
Punguza siasa mkuu. Tangu enzi za Yesu watu walilalamika kulipa kodi wakaambiwa cha kaisari mpeni kaisari. Kwahiyo Mama Samia hatakuwa kiongozi wa kwanza kulalamikiwa. Kama una maisha magumu pambana huku ukimwomba Mungu akufanyie wepesi.
 
Mbaya zaidi MTU akishakaa kwako siku akiondoka huko anakofikia Ni kumsema mkeo vibaya.

Mara jamaa kaolewa maana yule mke Ni mvivu. Mke mchoyo, mke anadharau n.k

Kumbukeni mke wangu Ni pambo la nyumba yangu, sio MTU wa kusonga ugali kwa ajili ya mijitu ya kijijini.

Mke wangu ashindwe kunilisha vipaja vya kuku kisa Kuna mgeni au mke wangu asiwe na Uhuru wa kujiachia nyumbani kwake kisa mgeni!

Kwendreni huko.
Kabisa.... kila mtu akae kwake. Mi nikienda nafikia Hotel kuepuka maneno. Wao wakija wanataka kufikia home.... kila mtu akae kwake.
 
Mbona na nyie mnalalamika mkienda us au ulaya watanzania wanawazimia simu. Siwasapoti Ila taarifa ni muhimu pia zamani mgeni akija anakuja na zawadi Kama chakula na sisi wa Kanda ya ziwa samaki.
Siku hizi anakuja kama alivyo ila anategemea aondoke tofauti na alivyokuja. Na hapo anapeleka maneno kijijini mabaya....
 
Kiukweli kwa maisha tuliyo nayo sasa inapendeza mgeni akija aje kwa taarifa.

Ni asiyeelewa tu namna dunia imefikia wapi kwa sasa ndo ataona ye mgeni akija tu kwake bila taarifa ni sawa.

Hawa hawa tunaowaamini wengi wamekuwa mwiba kwa baadhi ya familia hasa baada ya kuja bila kuwa na vya msingi vilivyowaleta.
Na wanaanza kubaka na watoto wetu.... ni bora akuambie mapema ujue atalala wapi. Unakimlaza sebuleni analalamika kuwa watoto wako wamelala vyumbani mwao yeye umemlaza sebuleni. Kumbe humwamini pia kumwachia watoto. Dunia ya sasa mawasiliano ni muhimu sana.
 
Jam

Jamaa mbona una hasira dhidi ya ndugu zako wallikufanya nini mpaka unawaitia Mijitu?

Mkuu Jaribu kuwa Mnyenyekevu basi.

Hao unaowadharau ipo siku utawakumbuka na hutawaona.

Kama huwezi kumsaidia mtu basi achana naye ila usimpe majina mabaya eti Mijitu.....Itakuwa wewe Kweli Umeolewa maana hizo hasira tu sio kidogo.
Watu wanajisahau sana
Nawakumbusha , tomorrow is mystery hakuna aijuae!

Unaowadharau sahivi ipo siku utawahitaji na hutawapata!
Maisha mzunguko
Cha mhimu mtu atoe taarifa kwanza Kwa mhusika na kuwe na sbb inayomfanya aje!
 
Back
Top Bottom