kajojo
JF-Expert Member
- Jun 9, 2012
- 2,946
- 5,470
Wanyoooshe baba wamezidi midomo. Watu kama Hao hawanaga shukraniHii tabia imekuwa sugu. Yaani mtu anakaa tu na halmashauri ya kichwa chake anaamua kuwa nimpigie jamaa yangu yupo Dar nikafikie kwake.
Mi nipo zangu home jana inaingia simu ya Abouu. Ananiuliza maisha vipi namwambia safi tunalisongesha. Maneno maneno mengi mwisho anasema nipo Dar nataka nije kwako nielekeze. Nikamuuliza wakati unapanga kuja ulinishirikisha? Unaamua tu kuja kwangu hata hujanitaarifu.
Jamaa ame mind kawaambia watu nimemkataa. Ninyi wa Mikoani mnadhani huku ni kama kwenu huko ambako hamna ratiba maalum. Mnajiamulia tu.
Mwaka juzi nlimwacha mtu stand kwa upuuzi kama huo. Kakaa zake Mbwinde mwisho kaamua kuja town a anipigia simu kuwa yupo Dar anataka aje home. Nlimwambia tu kuwa sipo home na familia tumesafiri.
Akaanza kuomba basi nimpatie pesa ya sehemu ya kulala anisubiri. Nilimwambia mwezi mzima sitokuwa home. Akataka nimtumie nauli. Nlizima na simu kabisa. Huu ni wendawazimu.
Halafu tukiwaakaribisha mnaenda kutusema kijijini kuwa huku tunaishi maisha mazuri sana hatuwajali watu wa vijijini. Mnaenda kutuponda sana kijijini kuwa tunatumia pesa vibaya.
Mimi walienda kusema nafuja sana pesa badala ya kuwasomesha watoto wao. Mtu kazaa watoto 13 anataka nimsomeshee... Mimi nina 3 tu. Bado wanaenda kusema nakuaje na watoto wachache ... Mwanaume gani. Mke amenikalia kichwani anarudi jioni kama mwanamke. Wanataka wife awafulie nguo zao. Na wanakuwa wakali akirudi awapatie chakula n.k sina hamu na ndugu kabisa.
Mmoja tumekaa naye mwaka mmoja amekuja nimsomeshe diploma. Akirudi toka chuo anaangalia TV mpaka saa 4 akipewa kazi basi za home siku yupo asaidie... Anasema anateswa sana hawezi soma. Nikasubiri likizo. Akaenda kwao kusalimi. Nikamwambia atafute chuo aendelee kusoma huko nitamlipia ada.
Alilia sana anataka arudi Dar. Nlimwambia huku wifi yako atakutesa hutapata muda wa kusoma. Akabembeleza sana nilimkatalia coz alishanipakaza sana kijijini na kumchafua sana wife. Na mtu mwenyewe ni ndugu wa mbali kabisa..