Yalinikuta Jumapili alikuja mtu wa aina hiyohiyo nyumbani tofauti ni kuwa huyu aliletwa na ndugu yangu, alichonikera ni vile alipofikishwa tu akawa na kidaftari chake ameandika namba za watu wake anaojua wapo Dar, akaomba simu yangu na kuanza kuwapigia mmoja hadi mwingine mbaya zaidi akawa anawaambia uongo kuwa yupo ameekaa kwangu kwa zaidi ya mwezi, kilichonikwaza zaidi siku iliyofuata nimerudi toka mihangaiko yangu jioni nakuta sebule imejaa hao rafiki zake kama kuna kikao cha kikoba wamechukua vinywaji kwa jirani bila kunishirikisha bill ipo kwangu.