Hii tabia imekuwa sugu; mtu anaamua tu aje Dar kukusalimia na afikie kwako

Hii tabia imekuwa sugu; mtu anaamua tu aje Dar kukusalimia na afikie kwako

Watu tunajisahaulisha haraka mno au pengine hatufikiri sawasawa, maisha ya Afrika Ni undugu,likikupata ndugu zako ndio wataokubeba
Huku Hakuna funeral companies kwamba ukifa itaenda lipia gharama uzikwe ,Ni Hao ndugu zetu tunaowanyanyapaa ndio wachimba kaburi
Ikitokea umeumwa Ni Hao Hao ndugu ndio watakua wauguzi
Indeed we need to be humble, mengine Ni umaskini kama walivyosema wachangiaji wengi
Hata Ulaya ukifa wanatafutwa Ndugu zako. Kama uliwatupa ndio utazikwa na City
 
Ukiona unachukia wageni ujuwe bado huna sehemu / chumba cha ziada mgeni kulala. Dsm wanachukia kwa sababu hakuna room za wageni. Kwenye changamoto kubwa ndiyo utajua umuhimu wa ndugu zako.

Mhubiri 5:11
Mali yakiongezeka, hao walao nao waongezeka na mwenyewe hufaidiwa nini, ila kuyatazama kwa macho yake tu?

When goods increase, they are increased that eat them: and what good is there to the owners thereof, saving the beholding of them with their eyes?
 
Umenikumbusha kuna siku sina hili wala lile mida ya 4 usiku inaingia simu "Oya mudi hapa, Mwanangu nipo Dar alafu aliepaswa kunipokea hapatikani" kilichotokea ile siku huyu jamaa Dar hatokuja tena kizembe
 
Unachokisema kinaweza kuwa ni sawa ila Taarifa ni muhimu zaidi... We huwezi ukanipigia tu simu from no where kwamba upo Mbezi stand ya Magu, kwanza nje ya yote ni kama unanikosea heshima sana as if unanimudu sana hivyo nitaku-ignore tuu na sitokupokea
 
Haya makaburi yaliyojaa misitu na magugu pori yaliyokomaa ndugu zao wako wapi?

Hawa yatima wanaodhulumiwa, kunyanyaswa na kutengwa mpaka kutelekezwa ndugu za wazazi wao wako wapi?

Hawa ombaomba na watoto wa mtaani wote hawana ndugu?

Tujifunze kuwa na mipaka na kuheshimu mipaka ya wenzetu, mawasiliano katika maamuzi yanayomuhusisha/yanatakayo muathiri mtu mwingine ni lazima.

Japo kumtelekeza ndugu kituoni sio vizuri, kheri umtafutie usafiri wa kurudi hapo hapo ama haraka iwezekanavyo.
Point Yako ni ipi hapo? Kwahiyo makabuli kuota nyasi ndo usipokee ndg zako au umtelekeze?
Una uhakika Watoto wote mitaani ni yatima? Hujui wengine wanaenda kisa wazazi wameshetengena wanazamia mjini?

Acheni roho mbaya za kimasimini Mimi nipo mjini Huwa nafurahi sana nikikutwa ndgu yangu kaja kunisalimia .kinachowasumbua ninyi ni vile kuishi maisha yasiyo yenu Wakati wee ni kanya boya tu unaishi maisha ya kina Aunt Ezekiel matokeo yake ndo kukimbia ndg zako!

Ishi maisha Yako hutojutia!! Kwani akija akaenda kusema ulimlaza njaa seburen ndo utapungukiwa zaidi?

Umaskini mbaya sana
 
Umenikumbusha kuna siku sina hili wala lile mida ya 4 usiku inaingia simu "Oya mudi hapa, Mwanangu nipo Dar alafu aliepaswa kunipokea hapatikani" kilichotokea ile siku huyu jamaa Dar hatokuja tena kizembe
Hawa wabush huwa wanarahisisha sana maisha. Mtu kama huyo unampokea. Unamwacha home anashinda na watoto. Keshokutwa unakuja sikia mtu kalawitiwa au kanajisiwa unalaumu. Kumbe unakaribisha watu ambao hawajui hata kilichowaleta Dar ni nini. Jirani yangu mmoja mtoto wake alinajisiwa na ndugu yake katoka kijijini amekuja town ili amtafutie kazi za kutumia nguvu. Jamaa anashinda home anakula vizuri. Watoto uncle uncle. Kumbe akaanza kukanajisi katoto ka mia 6 ka mwenye nyumba. Kuja kugundua too late.
 
Ni upumbavu kudhani unachowaza wewe na wengine wanawaza.. simu ni yangu mtu akinisumbua its either na mblock au nazima nipumzike. Acheni kuja kujipendekeza kwa mashemeji zenu. Mnatusumbua sana nyie wa bush.
Nani anakusumbua wewe kinachokusumbua wewe ni umaskini wako na gubu lako Kwa ndg zako
Mtu anakuja mara Moja Tena Kwa miaka kadhaa umzimie simu au umuache stendi ? Kama sio umaskini wa kiwango Cha lami Ninini? Mchukue mweleze abc akirudi atawaambia na wengine
 
Mbaya zaidi MTU akishakaa kwako siku akiondoka huko anakofikia Ni kumsema mkeo vibaya.

Mara jamaa kaolewa maana yule mke Ni mvivu. Mke mchoyo, mke anadharau n.k

Kumbukeni mke wangu Ni pambo la nyumba yangu, sio MTU wa kusonga ugali kwa ajili ya mijitu ya kijijini.

Mke wangu ashindwe kunilisha vipaja vya kuku kisa Kuna mgeni au mke wangu asiwe na Uhuru wa kujiachia nyumbani kwake kisa mgeni!

Kwendreni huko.
Mkuu kama mkeo ni pambo la ndani na mapambo yenyewe utayaitaje? Pole sana Kwa adhabu uliyo nayo
 
Mbona na nyie mnalalamika mkienda US au Ulaya, watanzania wanawazimia simu. Siwasapoti Ila taarifa ni muhimu pia zamani mgeni akija anakuja na zawadi kama chakula na sisi wa Kanda ya ziwa samaki.
Hapa watu wanshindwa kutofautisha woote amabao wanasema ndg zao wasipokelewe kisa hajatoa taarifa wengi maisha Yao ni tia maji tia maji yaani hawana uhakika Leo atakula Nini atavaa nn. Ova
 
Watu wa Dar mnachekesha sana
Mkija mikoni mara zote mnajisabu karibuni Dar ndg zangu tutembeleane sie tuko huko wewe ukija maswala ya nauli ya kurudi niachie Mimi maneno mengi ya kiswahili na kitapeli mtupu... mwisho mnatuachia na no Zenu za simu. Mtu analima mpunga wake anauza gunia2 ananunua nguo mpya na nauli anabakiza Ili aje matokeo yake unamzimia simu kisa hajakupa taarifa Sasa ulimkaribisha wa Nini ukiwa kwake Kijijini kwann usimchukue umwambie mara nyingine ukitaka kuja toa taarifa.

Watu wa mjini kumbukeni mnapokuwa mikoani ndg Zenu wanawajali sana kunavyombo vimenunuliwa special Kwa ajiri yenu hata baba wa familia hajawahaaai tengewe kumbukeni ninyi ndo Huwa mnakula majogoo na mbuzi wakubwa huko kijijn Tena kuku kienyeji pure achana na broiler wenu. Ninyi ndio Kila kitu mnasifia Cha Kijijin mara hii mihogo mizuri mitamu Ina unga ..maembe haya mazuri Sana Nina miaka kadhaa sijala embe tamu kama hili. Mkiaga hamkatai kubebeshwa mpunga,karanga au mahindi Ili Hali wewe ulikuja n mikate na sikonzi 3 tu garama ya ya3500.

Acheni roho mbaya
 
Point Yako ni ipi hapo? Kwahiyo makabuli kuota nyasi ndo usipokee ndg zako au umtelekeze?
Una uhakika Watoto wote mitaani ni yatima? Hujui wengine wanaenda kisa wazazi wameshetengena wanazamia mjini?

Acheni roho mbaya za kimasimini Mimi nipo mjini Huwa nafurahi sana nikikutwa ndgu yangu kaja kunisalimia .kinachowasumbua ninyi ni vile kuishi maisha yasiyo yenu Wakati wee ni kanya boya tu unaishi maisha ya kina Aunt Ezekiel matokeo yake ndo kukimbia ndg zako!

Ishi maisha Yako hutojutia!! Kwani akija akaenda kusema ulimlaza njaa seburen ndo utapungukiwa zaidi?

Umaskini mbaya sana

Kajifunze kwanza kuandika.
 
Kutembeleana naona kama ni umbea flani hivi mtu anataka kukusnitch. Huwa sipendi wageni wanaokuja nyumbani kwangu na kisha kuanza kusnitch mara ooh iki kitanda umenunua shingapi?? Sijui kodi hapa unalipa shingapi?? Alafu akitoka apo anaenda kukutangaza . Aisee sipendi Ndugu kujua ninapokaa
 
Watu wa Dar mnachekesha sana
Mkija mikoni mara zote mnajisabu karibuni Dar ndg zangu tutembeleane sie tuko huko wewe ukija maswala ya nauli ya kurudi niachie Mimi maneno mengi ya kiswahili na kitapeli mtupu... mwisho mnatuachia na no Zenu za simu. Mtu analima mpunga wake anauza gunia2 ananunua nguo mpya na nauli anabakiza Ili aje matokeo yake unamzimia simu kisa hajakupa taarifa Sasa ulimkaribisha wa Nini ukiwa kwake Kijijini kwann usimchukue umwambie mara nyingine ukitaka kuja toa taarifa.

Watu wa mjini kumbukeni mnapokuwa mikoani ndg Zenu wanawajali sana kunavyombo vimenunuliwa special Kwa ajiri yenu hata baba wa familia hajawahaaai tengewe kumbukeni ninyi ndo Huwa mnakula majogoo na mbuzi wakubwa huko kijijn Tena kuku kienyeji pure achana na broiler wenu. Ninyi ndio Kila kitu mnasifia Cha Kijijin mara hii mihogo mizuri mitamu Ina unga ..maembe haya mazuri Sana Nina miaka kadhaa sijala embe tamu kama hili. Mkiaga hamkatai kubebeshwa mpunga,karanga au mahindi Ili Hali wewe ulikuja n mikate na sikonzi 3 tu garama ya ya3500.

Acheni roho mbaya
Na aje kwangu kufanya nini?? Nimemuita mimi? Mnawabebesha lawama ndugu zenu walioko mjini kama mtu kakataa kuja kwake wewe unalazimisha nini? Si ubaki uko kwenu kijijini kama huna hela bali kwenu sio lazima uje mjini
 
Back
Top Bottom