Awamu ya sita
Member
- Apr 1, 2021
- 21
- 98
Huu ni ukweli kabisa ambao nimeushuhudia kwa macho yangu. Ni kuhusu walimu wanawake wanaokuwa wamepata nafasi ya kwenda kusimamia mitihani ya taifa kulazwa madarasani tena madarasa ambayo hayana madirisha au yenye madirisha yasiyowahakikishia ulinzi dada, wake na mama zetu.
Kituko kingine unakuta hata walimu wakuu hawajali chochote kuhusu usalama wa wasimamizi wao.
Mfano nimepita shule x katika halmashauri ya Chamwino nikakuta mwl wa kike analala peke yake darasani huku ofisini wanalala askari mgambo wawili. Katika mazingira haya je usalama wa huyu mwl wa kike ukoje??
Funzo kubwa hapa ni kwamba; Serikali pamoja na kufanya kazi nzuri kuhusu usalama wa mitihani, tunaomba itoe maelekezo kuhusu usalama pia wa wasimamizi wa mitihani hiyo. Leo tunazungumzia Chamwino lakini pengine jambo hili lipo mahali kwingine na sio tu kwa wanawake pekee.