Hii tabia ya Wanasiasa kujibishana na polisi isiachwe iote mizizi. Alianza Malima, Kigwangalla, Nape, Lissu na sasa Mbowe

Hii tabia ya Wanasiasa kujibishana na polisi isiachwe iote mizizi. Alianza Malima, Kigwangalla, Nape, Lissu na sasa Mbowe

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Ni vema wanasiasa wakapewa elimu ya kutii Sheria bila Shuruti kwa sababu mabishano kati ya Polisi na wanasiasa sasa yameanza kuzoeleka na hilo si jambo jema.

Huko nyuma tumewahi kuwaona akina Adam Malima, Dkt. Kigwangalla, Nape, Sugu, Lissu, Mdee na Bulaya na sasa ni kiongozi mkuu wa upinzani Mbowe.

Kama Taifa nadhani kura mahali tunakosea, Tujirekebishe!

Maendeleo hayana vyama.
 
Kule Shinyanga mkuu wa kituo katoka na bango la Magufuli huko akaenda nalo hadi nyumbani kwa Salome Makamba kisha akalichana halafu akamkamata Salome Makamba kwa kosa la kuchana bango la Magufuli. Ila kwa kuwa amefanya tukio hilo majira ya saa nne za usiku na wala hakuona watu waliokuwa wanamrekodi basi naamini alikuwa amebugia gongo. Sasa hao ndiyo polisi unaotaka waheshimiwe?
 
Yaani polisi akuburuze tu kwa kuwa ni polisi na sheria unaijua, hivi unawafahamu polisi wa nchi hii kweli polisi wa kutumika kisiasa hawa ambao hawana weledi,

Lisu wapeleke mchaka mchaka.
 
Tatizo ni hao Polisi kubishana na wanasiasa, sio kazi ya polisi kubishana na wanasiasa. Huo ni utovu wa nidhamu wa Polisi. Polisi kazi yao ni kulinda usalama wa wanasiasa na kupokea amri (kufokewa) halali kutoka kwa wanasiasa.
Duniani kote polisi ni kama mbw.! anayesubiri kupokea amri.
 
Kwa hiyo mikono yenu ya chuma ifanyekazi sio,sasa hapo Mimi na jiuliza mlipofikia kwa kukataliwa na jamii ya Tanzania so mtauwa wote. Mpotayari kubaki wenyewe, ili mfanye mtakavyo,?
 
Yani wewe ni mpumbavu sana yani polisi akuburuze tu kwa kuwa ni polisi na sheria unaijua, hivi unawafahamu polisi wa nchi hii kweli polisi wa kutumika kisiasa hawa ambao hawana weledi,

Lisu wapeleke mchaka mchaka.
Tii sheria bila shuruti!
 
Hivi wewe una akili au matope!
Polisi wa Tanzania hawasimamii Sheria, kazi yao kwa sasa msimu huu wa uchaguzi ni kulinda CCM ising'olewe madarakani!
Bila kuhoji vitendo vya kijinga na vinavyokiuka Sheria vinavyofanywa na polisi, wananchi watateswa Sana na polisi wa nchi hii.
 
Ni vema wanasiasa wakapewa elimu ya kutii sheria bila shuruti kwa sababu mabishano kati ya polisi na wanasiasa sasa yameanza kuzoeleka na hilo si jambo jema.

Huko nyuma tumewahi kuwaona akina Adam Malima, Dkt. Kigwangalla, Nape, Sugu, Lissu, Mdee na Bulaya na sasa ni kiongozi mkuu wa upinzani Mbowe.

Kama taifa nadhani kura mahali tunakosea, Tujirekebishe!

Maendeleo hayana vyama.
Wewe nawe ni wa kupuuzwa tu, hao Polisi wako nao ni binadamu hivyo wanapofanya makosa wachekewe tu kwa vile wamevaa magwanda na kushika bunduki zilizonunuliwa kwa kodi zetu kutulinda na siyo kutunyanyasa. Hivi unamkumbuka Abdalah Zombe na Askari wake walivyowafanyia wale wafanyabiashara wa madini toka Ulanga au ulikuwa hujazaliwa?

Hata ni huko kujipendekeza wakati mwingine itendee haki dhamira yako kwani naamini kabisa kuwa unajua kuwa unatetea ujinga ila ni ile hulka ya kiccm ya kujitoa ufahamu ndiyo inakuongoza
 
Polisi wakifanya kazi kwa kufuata Sheria na kanuni na kuacha kuchanganya kazi na ukada hayo majimbizano yatoke wapi. Kumbuka hii sio polisi state ni democratic state.
 
Ni vema wanasiasa wakapewa elimu ya kutii sheria bila shuruti kwa sababu mabishano kati ya polisi na wanasiasa sasa yameanza kuzoeleka na hilo si jambo jema.

Huko nyuma tumewahi kuwaona akina Adam Malima, Dkt. Kigwangalla, Nape, Sugu, Lissu, Mdee na Bulaya na sasa ni kiongozi mkuu wa upinzani Mbowe.

Kama taifa nadhani kura mahali tunakosea, Tujirekebishe!

Maendeleo hayana vyama.
Kinachoonekana hujui tofauti ya kubishana na kupishana kauli. Kauli za polisi hupishana sana Sheria ambazo ndio hitajiwa kuzitumia ktk utendaji wa kazi zao za kila siku. Na hapo ndipo anaejua Sheria hupishana nao. Pia elewa mfumo wa uajiri polisi haufuati taaluma, na mafunzo ya miezi 9 wanayopitia, hawaivi.

Polisi wengi uelewa wao wa Sheria ni mdogo, na ndio maana unapohoji atendalo hukwambia 'usinifundishe kazi' badala ya kukutajia kifungu Cha Sheria. Ingependeza polisi wetu mwanzo kabisa walau akawa na cheti cha Sheria.
 
Polis hawa wanaotumika na ccm kubaki madarakani.kile kitendo cha polis kuvamia kambi za wagombea wa upinzani na kuwabambikizia kesi kinatia aibu sana jeshi La polis

Kwa weledi linazidiwa hata na la Malawi alilindi chama linalinda nchi
 
Back
Top Bottom