Hii video kuhusu V8 ya Serikali inasikitisha sana

Hii video kuhusu V8 ya Serikali inasikitisha sana

Kama unaona katiba mpya haiwezi kubadilisha kitu kinachokufanya ulalamike ni nini?.Unadhani ni nani wakuchukua hatua kama wewe unalalamika hadi rais wa nchi analalamika.Hapo ulipo kama mwananchi wakawaida huna nguvu yakubadilisha chochote,sasa badala uunge mkono katiba mpya itakayompa mwananchi nguvu nakupunguza nguvu za wanasiasa wewe unaikataa unadhani nani atakayeshuka toka mbinguni arekebishe mambo.Katiba bora ndio kimbilio lakunusuru hii nchi.Kama uelewi endelea kulalama.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Huu ujunga huu, wananchi tunaumia sana, tunaumizwa kwa kodi pamoja na mfumuko wa bei lakini wao wanaishi wanavyotaka tuu na mambo kama haya, hizo ni kodi zetu kabisa
 
Wapi??uongoo nyie mtatuletea vita kama kama congo ,msumbiji ndio maana tunawachora tunawapa CCM nchi
Kwan congo walifikaje uko?.Au unadhani waliowafikisha uko hizo nchi ni vyama vya upinzani. ni serikali zao zilishindwa kusimamia rasilimali za nchi kama kinachoendelea sasa nchini.Ata hapa iko siku yatatufika ya hao unaowabeza.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Unashangaa V8...

Wakati kuna midege yetu imepaki kwa sababu za kiufundi na kushikiliwa na mabepari...
 
Mama ni dhaifu, ila tunafanyaje? kweli tuendelee kumtegemea yeye? kwa haki hii?
kwani hao mnaowaita wezi mtawaondoa kwa kuchagua watu kuyoka mbinguni au hawahawa binadamu ambao mkiwachagua nao watafanya hayahaya
 
Mkuu katiba haiwezi kuwa suluhisho la wizi ila suluhisho ni uzalendo kwanza watu wawe na hofu na Mungu. Na huo muundo uanze kwenye ngazi ya familia, shule, na jamii kisha ndyo huku juu, lile somo la uzalendo lilikuwa la muhim mno kuanzia shule ya msingi, ila tatzo kila mtu mjuaji.
Katiba ni muhimu sana kwasababu itajenga taasisi zitakazojisimamia na wananchi watapata njia yakufwatilia kwasababu mamlaka itakua kwa wananchi.ukikaa ukasubiri uzalendo wawatu utasubiri sana.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Hata ukitaka kukubali Kwamba Waliopewa dhamana wanatimiza wajibu wao lakini hali halisi inatuumbua.
Tumuombe Mungu ainusuru nchi hii pakusemea hakuna.
Duh ! Yaani pakusemea hakuna na pakulalamikia hakuna pia NOBODY CARES !!!
 
Sio kila kitu kitaweza kuonekana jambo la muhimu Mama ameruhusu uhuru wa habari ili aweze kujua yanayoendelea mtaani pia maana mengine anaweza asiambiwe lakini kwa maoni mbali mbali toka mtaani anapata habari na kuchukua hatua.
Kama utashi ukiwepo wa kuchukua hatua itakuwa ni jambo jema !! Mpaka sasa naona ubao wa magoli unasoma 3 - 1 wapigaji wanaongoza !
 
She doesn't even have a clue what she is supposed to do.
Atajuaje wakati hakuwa na nia na wala haijui nchi vizuri ukiwa makamu kuna mambo huwezi jua na kuna picha huwezi ziona kwa mapana yake. Mm nishashuhudia hio gari hapo toka ina namba zake mpka now imetolewa na siku moja nimepita night sikukuta hiyo gari asubuhi ipo na pamefagiliwa tairi zisionekane siku si nyingi itafutwa namba za vioo watu watajipigia mnada bubu
 
Back
Top Bottom