Hii video kuhusu V8 ya Serikali inasikitisha sana

Hii video kuhusu V8 ya Serikali inasikitisha sana

Halafu Jana Kairuki bungeni anasema kuna mabilioni yametengwa kwa kununua magari ya serikali,
Haya yapo huku yanapigwa jua, jaman inaumiza mnooo, [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Acha waendelee kupiga tu
Wananchi wa nchii hii tumezidi unafki, hatuna jema.
Kiongozi aliyepambana na hali ya ufisadi ni mmoja tu JPM.
Matokeo katukanwa hadi kupotezwa huku sisi wananchi tukishangilia na kucheza wimbo mmoja na mafisadi wa kumsimanga.
Kwa hali hiyo unazani ni nani mwenye akili timamu anaweza kuhatarisha maisha yake kwa kuwatetea watu wasio na shukrani km wa TZ?
Ufisadi ndio chanzo kikuu cha machafuko popote pale.
Tukifika huko ndio akili itatukaa sawa.
Usha wahi kusoma report za CAG wakati wa magufuri? Zitafute usome then rudi humu
 
Huku raia sisi tukiendela kuimba ngonjera za kusikitika kwenye mitandao ya kijamiii, hawa watawala wao wanazidi kufanya yale wanauo penda, hakuna kitakacho badilika, hata katiba mpya haitabadili huu uhuni wa watawala, hawa viongozi kuanzia top hadi chini wanajuana hawa ni wana syndicate ya kupiga pesa za umma, na wanaratiba za kwenda majukwaani kutoa machozi ya mamba.

Hawa watawala wanashindana kutoa machozi ya mamba kuhadaa wajinga na ionekana jamaa wanajali sana wanancni na wako na wanancji lakini uhalisia ni kwamba wana syndicate ya kuimaliza nchi.

Raisi anatoa crocodile tears tu na kuhadaa umma, hakuna kitu, kwamba raisi anauchungu na hii nchi ni uongo mkubwa sana, raia tusipo simama wenyewe kulinda hii nchi kwa niaba ya vizazi vijavyo tutakuwa hatutendi haki.

Angalia gari kama hilo ni kodi zetu, ni kodi za wazazi wetu kule kijijini wanao isha life gumu lakini still wanakamuliwa na Serikali kodi ili wakanunue magari kama haya na baadae wanayatelekeza mtaani.

Hata katiba mpya haitabadilisha huu ujinga zaidi ya kuja kuwa show kwamba tumechoka.

View attachment 2587531
Asante Kwa taarifa nalifikisha sehemu husika...
#ASAP
 
Inasikitisha sana, mambo ya serikali ndivyo yalivyo...
 
Mimi naelewa Sana mkuu

Ilikua kawaida Gari Kuja kutuchukua kwenda kununua mahitaji pale mjini Kati kawaida tu [emoji23][emoji23]

Mambo ni mengi mzee alikua mtata Sana Kuna kipindi amestaafu wakawa wanakata kata umeme pale mtaa wake direct akampigia waziri ( simtaji Jina) anamwambia wewe kwanini mnakata umeme hapa kwangu anamfokea [emoji23], calmly waziri akamwomba msamaha na Muda mchache tanesco wakaja eeeh Nkasema hii hatari [emoji23][emoji23] hii nchi watu wana power na wana zi abuse hatari mno
Note : he was not my biological father, though related by blood
Kuna viongozi sijui huwa kuja nguvu gani, unakuta amestaafu lakini anaogopwa. Itakuwa Watanzania ni waoga sana!
 
Kuna viongozi sijui huwa kuja nguvu gani, unakuta amestaafu lakini anaogopwa. Itakuwa Watanzania ni waoga sana!
Kuna Wakati ccm ilitaka kuwapangia hawa wastaafu shuhuri maalum ili wasiingilie shuhuri za chama na Serikali wakiwa wamestaafu; mkwere akafanya mbinu zake yule Katibu mkuu wa ccm wa wakati huo, akawa NDUGAINIZED siku hizi anazubaa zubaa kwenye corridors huko Lumumba!
 
Kusema kweli Katiba Mpya ni muhimu sana kwasasa.

Hata kama ni nguo, huwezi kukaa na nguo uliyoinunua Mwaka 1977 hadi leo hii. Lazima itakuwa imepitwa na wakati lakini pia itakuwa na Vilaka vingi mno
Sasa katiba mpya na hio v8 vinausiana nini
 
Wakat zzk akiwa na akili zake kabisa zileeee za ukwel, aliwahi kusema kuwa nchi hii inahitaji rais mkali(dictetor) na akatoa na sababu kuwa viongozi hawaogop wala hawaongozwi kwa maadili wanajiongoza wenyewe. Mwisho wa kinukuu....

Baada ya utawala wa magu, naiona maana halisi ya ile sentesi, maana ktk kipindi cha 2015-21 haya mambo tuliyasahau kabisa, tulizunguzia agenda na kama wizi ulijitokeza hatua zilichukuliwa on the spot,

Leo hii kila mfanyakazi anakula kulingana na urefu wa kamba yake, huenda tukafika ila 2 tutakuwa tumechoka saaaana au tutakuwa taifa lisilojari mali za uma kwa maneno rahisi uzalendo utakuwa umeondoka kabisa.

Tuipende nchi yetu hatuna nchi nyingine inayoitwa TANZANIA ulimwenguni kote
 
Kusema kweli Katiba Mpya ni muhimu sana kwasasa.

Hata kama ni nguo, huwezi kukaa na nguo uliyoinunua Mwaka 1977 hadi leo hii. Lazima itakuwa imepitwa na wakati lakini pia itakuwa na Vilaka vingi mno
Mkuu katiba haiwezi kuwa suluhisho la wizi ila suluhisho ni uzalendo kwanza watu wawe na hofu na Mungu. Na huo muundo uanze kwenye ngazi ya familia, shule, na jamii kisha ndyo huku juu, lile somo la uzalendo lilikuwa la muhim mno kuanzia shule ya msingi, ila tatzo kila mtu mjuaji.
 
ndio maana nchi za uarabuni huwa ikifikia hivi Raia wanaingia Ikulu kila mtu anatoka na chake

kwa haraka nilikuwa nawaona wapuuzi ila ukitafakari wana akili sana, Li V8 kama hilo mtu kajichukulia ukute hata kwa 30 mils
30 millions yote hio, hio mtu kauziwa million 10 tu hapo hamna maajabu chuma imeandikiwa scrap value
 
Back
Top Bottom