Hii video kuhusu V8 ya Serikali inasikitisha sana

Hii video kuhusu V8 ya Serikali inasikitisha sana

Chadema tukishika hatamu tutawafilisi wote hao hata wakikimbilia nje ya Nchi tutatumia Interpol kuwakamata na kuwarudisha ili wakanyee debe.
Unazungumzia chadema wale waliokatiwa chajuu na lowassa 2015 wakauza chama, na wanaolamba asali sasa hivi, au wengine?
Chadema uliyo nayo kichwani ni ile ya enzi za Dr Slaa, hii ya sasa hivi wala tusidanganyane bwashee, hakuna chochote cha maana.
 
Huwa ninajiuliza kama vishirika vidogo kuviendesha vinatushinda tunawezaje kuendesha serikali yooote?? Ukweli nikwamba hatuwezi kujitawala japo hatutakiwi kutawaliwa...
Hatuwezi tanesco,tanapa,ttcl,atcl,trc,tamesa... taja mashirika yooote nimadudu matupu Sasa liserikali looote tutaliwezea wapi? Kisa wanasiasa wanavaa masuti,wanalindwa namapolisi na kupiga mdomo saaana watu wanadhani wanaakili!!!!
Ushauri wangu kila wizara iundiwe kitengo maalumu cha "Sheria na udhibiti ubora" Ili kupitia kila maamuzi na utekelezaji wa wizara na kutoa ripoti ya utekelezaji kila mwezi....wezi wote wafungwe bila kuangalia walikuwa na cheo gani mbona sisi hukuchini mnatufunga tukiiba kidogo tuu??? Shame on you!!! Wanafiki wakubwa!
MH. RAIS TAKUKRU NAYO IVUNJILIWE MBALI HARAKA KWANI NI KUPOTEZA PESA,MUDA NA NGUVU KUWA NA KITENGO KISICHO NA TIJA YOYOTE... NCHI INAIBIWA MMMNO WAO WANASTAREHE KWENYE MABAA KUJISIFU,KUTISHIA NA KULEWA
 
Wakoloni weupe pia walikuwa wakisema hivyo hivyo kuhusu TANU kuwa hawawezi kushika Dola ati ni chama cha wanywa kahawa.
Nchi inahitaji kiongozi mmoja tu mwenye akili awe rais nakuhakikishia chadema wakishika hii nchi tutajuta kuzaliwa Tanzania

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Huku raia sisi tukiendela kuimba ngonjera za kusikitika kwenye mitandao ya kijamiii, hawa watawala wao wanazidi kufanya yale wanauo penda, hakuna kitakacho badilika, hata katiba mpya haitabadili huu uhuni wa watawala, hawa viongozi kuanzia top hadi chini wanajuana hawa ni wana syndicate ya kupiga pesa za umma, na wanaratiba za kwenda majukwaani kutoa machozi ya mamba.

Hawa watawala wanashindana kutoa machozi ya mamba kuhadaa wajinga na ionekana jamaa wanajali sana wanancni na wako na wanancji lakini uhalisia ni kwamba wana syndicate ya kuimaliza nchi.

Raisi anatoa crocodile tears tu na kuhadaa umma, hakuna kitu, kwamba raisi anauchungu na hii nchi ni uongo mkubwa sana, raia tusipo simama wenyewe kulinda hii nchi kwa niaba ya vizazi vijavyo tutakuwa hatutendi haki.

Angalia gari kama hilo ni kodi zetu, ni kodi za wazazi wetu kule kijijini wanao isha life gumu lakini still wanakamuliwa na Serikali kodi ili wakanunue magari kama haya na baadae wanayatelekeza mtaani.

Hata katiba mpya haitabadilisha huu ujinga zaidi ya kuja kuwa show kwamba tumechoka.

View attachment 2587531
Inakera sana.

 
Chadema tukishika hatamu tutawafilisi wote hao hata wakikimbilia nje ya Nchi tutatumia Interpol kuwakamata na kuwarudisha ili wakanyee debe.
Upuuzi,Tanzania Ina tatizo la kijamii walio Nje wakiingia nao wanafanya hivyo hivyo..

Yaani tukiweza tuimarishe taasisi tuu.
 
spika yupo kwa ajili ya kumlinda rais bungeni

kila makosa yanayofanyika wanajificha kwenye kichaka cha JPM
haina ubishi serikali imefeli ni vile tu hakuna wa kuongea hadharani maana mpaka wale wapinzani feki wameonjeshwa asali
Wanamkomoa marehemu ila kiuhalisia tunaokomolewa ni sisi wananchi
 
Afu tamisemi wanaomba bajeti ya kununua kama hayo mapya 100 🤣🤣🤣 tz Mai kantriii
 
Kuna baadhi ya hao wanaolalamikiwa huwa wanajiweka wenyewe kwenye madaraka make ukigoma analetwa kwa nguvu utasikia amepita bila kupingwa.uwezo wetu wa kuwakataa bado ni mdogo bila kupata katiba mpya iendayayo na nyakati hizi.
Ni nani aliyewaweka madarakani hao ndugu unaowalalamikia???
 
Kuna hujuma kubwa sana nyuma yaaaaa ila Mungu huyu hawezi acha hili lipite bila watu wachache kuadhibiwa kwa uovu huu. Tiss yetu angalile haya ipo siku mtasema kudaiwa kaz mlifanya nyie hamna ushirika na serikali ama kiongozi nyie ndio jamuhuri msichoke hata kama mnachoshwa
Mtu yeyote ambaye kwake suluhu ya kwanza ni kumuachia mungu huwa namuona kiumbe wa ajabu
 
Katika nchi yetu dhana ya uwajibikaji haipo kabisa, who cares as long as ni mali ya umma. Hao tunaowaitaga mabeberu hawanaga ujinga kama huu wa kuchezea mali za umma kabisa. Sasa ukichanganya na taarifa ya CAG unahisi kutapika.

Pamoja na mabaya yao machache ila tuna mengi zaidi ya kujifunza kutoka kwao na ndiyo maana wamesonga mbele.

Kuna mdau mmoja hapa alisema anaanza mkakati wa kukwepa kodi sababu anaona kodi anayolipa haimsaidii na inatumika hovyo hovyo na wachache, anaumia mno.
 
Doh mwamba ana sikilizia upepo kwanza kikinuka ana irudisha kisipo nuka ndo ime ishaaa iyoo. kufikia kesho haita kuwepo hapo..
 
Anakuja choko anakwambia kikubwa uhuru wa kujieleza ni mkubwa awamu hii.

Hii nchi ina laana nawaambia.
 
Maandamano ya amani ya kuwaonyesha wezi wetu kuwa tuna ghadhabu na tozo zetu yaandaliwe na uongozi wa Upinzani.

Mimi nitakuwa mstari wa mbele kabisa karibu na Mwamba na Lissu.

Mkuu na maandamano ya kushangilia kifo cha jpm utakaa mstari wa mbele au bado huelewi mpaka sasa???
 
Hujuma ya mali za Umma ni pamoja na kutelekezwa,mitaani magari ya Serikali na taasisi zake.
-Wajumbe wa shina, Wenyeviti wa Serikali za mtaa,madiwani, wawe wazalendo,wapeleka taarifa kwenye Mamlaka husika baada wanapo vitendo Kama hivi mitaani kwao (magari yetu,ya Serikali yameegeshwa siku nyingi na wajanja wanaanza hujuma ya kuondoa plate number nk.)
-Wananchi huwa tunajiuliza,kama Viongozi wetu wa Serikali ya mtaa na wao wamefanya syndicate na wabadhilifu hawa wa Serikali Kuu.
- Watendaji wanaohusika,(Idara inayomiliki) gari namba STL 4442 inayoonyeshwa katika clip ya video - wajitafakari.

Ushauri
1). Wahusika waondoe magari hayo na kupelekwa sehemu mahususi.
2). Mamlaka ya uteuzi wa wahusika, iwachukulie hatua za kinidhamu Wahusika wote.
3). Serikali kuu itoe waraka kwa wajumbe wa mashina na wenyeviti na watendaji wa Serikali ya mtaa na kata kufichua vitendo vyote vya kuhujumu mali za Serikali kwa Mamlaka husika.
4).Jeshi la Polisi,lenye Majukumu ya kulinda usalama wa raia na mali zao ,liwe linalinda mali za Umma au Serikali.
5). Serikali itoe tamko la kumpongeza mtoa tàarifa hii na kuwaomba Wananchi kufichua vitendo aina hii,kwa uwazi na ukweli
 
Halafu Angela Kairuki anaomba pesa anunue magari mapya
 
Acha waendelee kupiga tu
Wananchi wa nchii hii tumezidi unafki, hatuna jema.
Kiongozi aliyepambana na hali ya ufisadi ni mmoja tu JPM.
Matokeo katukanwa hadi kupotezwa huku sisi wananchi tukishangilia na kucheza wimbo mmoja na mafisadi wa kumsimanga.
Kwa hali hiyo unazani ni nani mwenye akili timamu anaweza kuhatarisha maisha yake kwa kuwatetea watu wasio na shukrani km wa TZ?
Ufisadi ndio chanzo kikuu cha machafuko popote pale.
Tukifika huko ndio akili itatukaa sawa.
 
Kwani V8 zimeanza kununuliwa awamu hii jamani?Acheni kumwonea macho kumchuzi...
 
Back
Top Bottom