Hii video kuhusu V8 ya Serikali inasikitisha sana

Hii video kuhusu V8 ya Serikali inasikitisha sana

Daah mbona hawa viongoz wanaiba sanaaa
Kule bunda wameiba vifaa vya hospital

Ile hii tabia ya kulinda na kuteteana ndiyo itaangamiza taifa

Kuoneana aibu tabia mbaya sana na ya ovyoo
Shaur yenu
Sema "Shauri yetu " kwani tuliingizwa cha kike tulipo weka alama ya ndio upande wa chama chetu maarufu siku ya kupiga kura.
 
Daah mbona hawa viongoz wanaiba sanaaa
Kule bunda wameiba vifaa vya hospital

Ile hii tabia ya kulinda na kuteteana ndiyo itaangamiza taifa

Kuoneana aibu tabia mbaya sana na ya ovyoo
Shaur yenu
ndio maana nchi za uarabuni huwa ikifikia hivi Raia wanaingia Ikulu kila mtu anatoka na chake

kwa haraka nilikuwa nawaona wapuuzi ila ukitafakari wana akili sana, Li V8 kama hilo mtu kajichukulia ukute hata kwa 30 mils
 
Huku raia sisi tukiendela kuimba ngonjera za kusikitika kwenye mitandao ya kijamiii, hawa watawala wao wanazidi kufanya yale wanauo penda, hakuna kitakacho badilika, hata katiba mpya haitabadili huu uhuni wa watawala, hawa viongozi kuanzia top hadi chini wanajuana hawa ni wana syndicate ya kupiga pesa za umma, na wanaratiba za kwenda majukwaani kutoa machozi ya mamba.

Hawa watawala wanashindana kutoa machozi ya mamba kuhadaa wajinga na ionekana jamaa wanajali sana wanancni na wako na wanancji lakini uhalisia ni kwamba wana syndicate ya kuimaliza nchi.

Raisi anatoa crocodile tears tu na kuhadaa umma, hakuna kitu, kwamba raisi anauchungu na hii nchi ni uongo mkubwa sana, raia tusipo simama wenyewe kulinda hii nchi kwa niaba ya vizazi vijavyo tutakuwa hatutendi haki.

Angalia gari kama hilo ni kodi zetu, ni kodi za wazazi wetu kule kijijini wanao isha life gumu lakini still wanakamuliwa na Serikali kodi ili wakanunue magari kama haya na baadae wanayatelekeza mtaani.

Hata katiba mpya haitabadilisha huu ujinga zaidi ya kuja kuwa show kwamba tumechoka.

View attachment 2587531
Kwangu mimi siyo kero tu, ni maumivu ya kodi yangu.
Kila nikifanya transaction nakatwa kodi kumbe kuna watu wanachezea kodi yangu hivi!?.
Anyway.
IPO SIKU TUTAELEWANA TU.
 
Gari imetegwa Apo wanafanya mchakato wa kadi kutok umilk wa serikali hadi mtu binafs

Asee inaumiza yaan sisi wa Tz tunawez kusimamia nn

Kwa Teknojia yote lakn mtu anafany wiz/mwenendo mchafu kama huu
 
Maandamano ya amani ya kuwaonyesha wezi wetu kuwa tuna ghadhabu na tozo zetu yaandaliwe na uongozi wa Upinzani.

Mimi nitakuwa mstari wa mbele kabisa karibu na Mwamba na Lissu.
 
Ni sahihi Chief ingawa kinachotuumiza ni kutoiwajibisha Serikali, for Years imekuwa inarudia makosa hayo hayo.

Poor Tanzanian 🙆‍♂️
Serikali tulioiweka madarakani, chini ya Dhamana ya kumwamini Mh. Rais; na ambaye ndiye huunda Serikali (cf. Walivyokuwa wanaNadi sera zao)kama haitekelezi wajibu wake, ina maana Mh.Rais aliahidi uongo. Hapo Serikali inaweza kuwajibishwa kadri ya Utaratibu kwamba sisi wananchi tunatengua Ukubali wetu kwa kupiga kura ya kutokuwa na Imani naye tena. Tunapiga kura hiyo kupitia bunge(Wawakilishi wetu)?
 
Hilo haliwezekani, Rais wa Tanzania kwa Mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Sasa ni Alfa na Omega.

Ndiyo maana kuna mmoja wa Waheshimiwa miaka ile aliwahi kumfananisha na Mungu Almighty.

Tuna hali mbaya sana kwa kweli
 
Gari imetegwa Apo wanafanya mchakato wa kadi kutok umilk wa serikali hadi mtu binafs

Asee inaumiza yaan sisi wa Tz tunawez kusimamia nn

Kwa Teknojia yote lakn mtu anafany wiz/mwenendo mchafu kama huu
Ingefaa na ninashauri(na uwezo huo upo) magari Serikali yafungwe vifaa microchips kufuatilia mwenendo wa magari ya Serikali kama wanavyofuatilia mwenendo wa tembo huko porini.
 
Hilo haliwezekani, Rais wa Tanzania kwa Mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Sasa ni Alfa na Omega.

Ndiyo maana kuna mmoja wa Waheshimiwa miaka ile aliwahi kumfananisha na Mungu Almighty.

Tuna hali mbaya sana kwa kweli
Aisee! Sasa ndo naelewa ni kwa nini jamaa hapo juu alianza na mabadiliko ya kuleta Katiba Mpya.
 
Back
Top Bottom