Hii video ya jamaa anatishia polisi,ni mkakati mpya wa destabilization ya serikali ya awamu hii!!?

Hii video ya jamaa anatishia polisi,ni mkakati mpya wa destabilization ya serikali ya awamu hii!!?

Polisi hawana shida,

Aliyewatuma ndiye atafikiwa kwa namna ya ajabu sana.
Wapo wenye shida.

Utakuwa na wakati mgumu sana kunishawishi nikubali kwamba Jumanne Muliro hana shida; au ACP Awadh hana shida, na wengi wengine wa aina hiyo..

Hao waliokuwa wanaranda randa mitaani wakiuwa waTanzania kama wanyama, uniambie wao hawana shida kabisa, ila aliyewatuma? Wao hawana utashi wa kuamua matendo yao kwa vile tu wametumwa?.

Ndiyo, wapo polisi wengi ambao wanapata taabu kubwa sana kutumikishwa kutenda maovu katika utawala huu; lakini pia wapo wabovu kabisa kama hao waliotajwa hapo juu.

Lakini kuna mambo yanashangaza sana miongoni mwa waTanzania:

Chukulia kwa mfano maneno haya yaliyonukuliwa kwenye mada hii ya mkuu "RESILIENT KETO':

"Kama mkakati huo utatekelezwa, mbona hali itakuwa mbaya sana"? Kwani hali sasa hivi bila ya huo mkakati ipo sawa?

"Tumefikia pabaya sana kama taifa; ni rasmi tunavuka mstari wa uzalendo...." Hivi uzalendo ni kukubali uovu na kuunyamazia; au mleta mada ana maana gani hapa?

hawa wanaowaua waTanzania ili wabakie madarakani, ndio wanaojuwa uzalendo ni nini? Ukiwapinga hawa unakosa uzalendo?

Ni mambo ya kushangaza sana haya!
 
Hivi kuna kitu gani cha kustua au kushangaza kuhusu video hiyo?

Kama mauaji ya Oktoba hayakukustua au kukushangaza na kusikitisha; hii picha hapa ina kitu gani cha kustua watu?

Watawala wameamua kujisimika madarakani kwa nguvu, kwa kutumia mitutu ya bunduki. Sasa hilo liwe jambo la kawaida na kutostua, lakini kundi linalokataa ujambazi huo na kutafuta njia za kuondoka kwenye umateka ndio wawe wa kustusha au kushangaza?
 
Akimwagwa mavi njooni mlalamike hapa
Yule kijana amesema wao wako tayari Sasa kufa kwa halali kwa uhaini wa kweli siyo wa kusingizia.
Amesema sasa wanataka wafe wote na polisi. Yaani wauwane na polisi.
Kiufupi wamejiandaa kufa.
Puuzieni taarifa yao kama MO29 makosa yajirudie.
 
Vuta picha maiti za polisi wameuawa barabarani au kambini mwao ziki trend Kwa mitandao zikifuatiwa na matamko kama hayo ya black mask huko mtandaoni!

Hali itakuaje Kwa viongozi wetu ambao wamekua wakiwatumia polisi kama shielding ya matamko na power walizobeba kimamlaka dhidi ya wananchi wanaowaongoza!!?

Kama mkakati huo ukitekelezwa mbona Hali itakua mbaya sana aiseh!!?nyie mwaonaje!!?

Tumefikia pabaya sana kama taifa,ni rasmi tumevuka mstari was uzalendo na hatma ya taifa hili!!

Mungu atusaidie katika kipindi hiki kigumu tunachopitia!!
Ilikuwa hamu ya moyo wangu kuliona hili katika majira kama haya .Ungekuwa vizuri wangeanza hawa vibaraka Lucha Tui gallow bird kavulata HAYA LAND HOV MamaSamia2025
 
Back
Top Bottom