Wapo wenye shida.
Utakuwa na wakati mgumu sana kunishawishi nikubali kwamba Jumanne Muliro hana shida; au ACP Awadh hana shida, na wengi wengine wa aina hiyo..
Hao waliokuwa wanaranda randa mitaani wakiuwa waTanzania kama wanyama, uniambie wao hawana shida kabisa, ila aliyewatuma? Wao hawana utashi wa kuamua matendo yao kwa vile tu wametumwa?.
Ndiyo, wapo polisi wengi ambao wanapata taabu kubwa sana kutumikishwa kutenda maovu katika utawala huu; lakini pia wapo wabovu kabisa kama hao waliotajwa hapo juu.
Lakini kuna mambo yanashangaza sana miongoni mwa waTanzania:
Chukulia kwa mfano maneno haya yaliyonukuliwa kwenye mada hii ya mkuu "RESILIENT KETO':
"Kama mkakati huo utatekelezwa, mbona hali itakuwa mbaya sana"? Kwani hali sasa hivi bila ya huo mkakati ipo sawa?
"Tumefikia pabaya sana kama taifa; ni rasmi tunavuka mstari wa uzalendo...." Hivi uzalendo ni kukubali uovu na kuunyamazia; au mleta mada ana maana gani hapa?
hawa wanaowaua waTanzania ili wabakie madarakani, ndio wanaojuwa uzalendo ni nini? Ukiwapinga hawa unakosa uzalendo?
Ni mambo ya kushangaza sana haya!