Hapo vipi?
Awali ya yote nadeclare yakwamba ni kisasi cha milele na shetani na lazima nitalipa kisasi juu yake. Nije kwenye mada husika ya kwamba ninaposema hii vita kati ya mwanadamu na shetani sio sawa na haki ni kwasababu zifuatazo.
1. Vita hii mwanadamu ni kiumbe ambacho kwa namna alivyoumbwa anauwezo wa kumbambana na kiumbee kwa umahiri, ubora, kiustadi na uwezo umkubwa kwa adui wake katika hali ya nyama na damu na sio katika ulimwengu wa roho, ndio maana ameweza kubuni na kitengeneza silaha kama, mishale, mikuki, mabomu, mabomu ya nyuklia nakadhalika.
Hivyo basi kujificha kwa shetani na kupewa uwezo wa kumuingia na kumshambulia na kumtesa mwanadamu katika ulimwengu wa roho pasipo mwanadamu kujua tayari ni vita isiyokuwa ya haki na usawa.
Nadhani ingekuwa shetani ni kiumbe chenye kutumia mwili na nyamba katika vita hii ni wazi asinge mweza mwanadamu ndio maana akajificha na kupewa uwezo wa kumuingia, kumtumia, kumtesa na kushambulia mwanadamu pasipo mwanadamu kujua ila anakuja kujua baadaye akiwa amesha umizwa na kuteswa na shetani kwa kutumia mapepo, majini, mizimu na wachawi.
Hii vita hata mdhaifu wa kwanza na wa mwisho angesimama upande wa shetani angeonekana mwenye nguvu,wakutisha na mwenye uwezo sana.
2. Hii vita ilikuwa kati ya Mungu na shetani kwa mujibu wa vitabu vyote vya dini Biblia na kuruani lakini anashambulia tena kwa mazingira yasiyokuwa ya haki na usawa ni mwanadamu...shetani ameshindwa huko mbinguni kwenye vita kati yake na jeshi la Mungu ambaye ni malaika, alafu anakuja kufanya vita ambayo sio ya haki na usawa..ndio maana nasema lazima nitalipiza kisasi huko kwenye ulimwengu wa roho milele juu yake.
NB. Kama kweli shetani anauwezo na anamuweza mwanadamu avae mwili na nyama kama Bwana Yesu alivyofanya then aje Duniani kupambana na mwanadamu..tunamsubiri na dhahiri anaonekana ni kiumbe dhaifu mno hatawezo kufanya hivyo kwasababu ya udhaifu wake.
Shetani Hana mamlaka juu yetu ikiwa tuna mahusiano mazuri na Mungu na vita ya ulimwengu wa roho haiko ivyo Kama unavyodhani, ili shetani akupige ni lazima apate uhalali ambao Mungu mwenyewe anaruhusu upigwe mfano,
Ayubu 1:6-11
[6]Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao.
Now there was a day when the sons of God came to present themselves before the LORD, and Satan came also among them.
[7]BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.
And the LORD said unto Satan, Whence comest thou? Then Satan answered the LORD, and said, From going to and fro in the earth, and from walking up and down in it.
[8]Kisha BWANA akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.
And the LORD said unto Satan, Hast thou considered my servant Job, that there is none like him in the earth, a perfect and an upright man, one that feareth God, and escheweth evil?
[9]Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha BWANA bure?
Then Satan answered the LORD, and said, Doth Job fear God for nought?
[10]Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi.
Hast not thou made an hedge about him, and about his house, and about all that he hath on every side? thou hast blessed the work of his hands, and his substance is increased in the land.
[11]Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako.
But put forth thine hand now, and touch all that he hath, and he will curse thee to thy face.
Ni kweli wanadamu kiuhalisia hatuwezi kufanya vita na shetani tukashinda, ila tumepewa kushinda kutokana na Roho mtakatifu/Nguvu za Roho mtakatifu kuwa ndani yetu NB. Kwa wale waliompokea Kristo
1 Yohana 4:4
[4]Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.
Ye are of God, little children, and have overcome them: because greater is he that is in you, than he that is in the world.
Mitizamo wako sio sahihi tafuta kupata maarifa zaidi ya ulimwengu wa roho. Mungu wetu ni muaminifu na hukumu zake ni za haki ndio maana shetani akikushitaki na akashinda kesi mbele za Mungu basi anapewa uhalali wa kukusurubu anavyotaka na Kama huna maarifa utateswa na shetani Hadi kufa kwako, ndio maana shetani akaitwa Mshitaki
Ufunuo wa Yohana 12:10,12
[10]Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
And I heard a loud voice saying in heaven, Now is come salvation, and strength, and the kingdom of our God, and the power of his Christ: for the accuser of our brethren is cast down, which accused them before our God day and night.
[12]Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.
Therefore rejoice, ye heavens, and ye that dwell in them. Woe to the inhabiters of the earth and of the sea! for the devil is come down unto you, having great wrath, because he knoweth that he hath but a short time.
Hitimisho ukitaka shetani asikushinde ni heri uwe upande wa Mungu ama uwe upande wake ukiwa vugu vugu ndo utamjua shetani ni hatari kiasi gan.
Ufunuo wa Yohana 3:15-16
[15]Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
I know thy works, that thou art neither cold nor hot: I would thou wert cold or hot.
[16]Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
So then because thou art lukewarm, and neither cold nor hot, I will spue thee out of my mouth.
NB. Mpokee Yesu kwa uzima wako hapa duniani na huko uendako baada ya kufa.