Hiki kiarabu kina maana gani?

Hiki kiarabu kina maana gani?

Ni kwanini hao watu hawarogi kwa kuandika kwa lugha ya Kiswahili unayoifahamu?

Ua hiyo ndio lugha ya Urozi?
Cc Mzizimkavu,
Wanaloga tu hamna chochote.
Ushawahi kusikia, kusoma albadir kwenye bibilia?
Hiyo karatasi akiitia kwenye maji hayo maneno yakiyeyuka ukimwagiwa hayo maji au ofisini, njiani,nyumbani cha moto utakiona.
Inategemea na mnyama na ubaya unaemtuhumu.
Ukitaka afe mtu itasomwa mara 30 unatoa sadaka madrasa utasomewa dua ikitoka hapo unaoga maji yamewekwa hiyo karatasi huku unanuia.
Kesho humkuti mgomvi wako popote.
Na ukiweka ndani hujatumia akikua huyo unae.
Elimu Dunia 🙌
 
Neno la kuirembaremba inaitwa du'a neno kavu lisilo na marembo ni unaitwa uchawi
Screenshot_20241228-083428_Video Player.jpg
 
Huo ni USHIRIKINA, choma moto mzee, tujitahidi kufanya ibada na maombi sisi wenyewe.
Laiti mngejua kuwa dua kupokelewa ina vipengele kadhaa lakini kimoja wapo ni USAFI wa muombaji, kwa dunia ya leo unaweza kwenda kwa sheikh kuomba dua kumbe sheikhe mwenyewe ni mchawi anaruka usiku, ni mshenzi anagonga mke wa mtu, kumbe ni anamla ndogo mtu, kumbe ni dhulumati, kadhulumu mali za yatima. Unategemea dua itapokelewa hiyo.

Tujitahidi kufanya ibada, tusome kidogo tujue dua zinapokelewaje..
Mfano funga sunna zako, jioni unapofuturu piga dua yako,
mola yupo karibu zaidi na mja wake pale anaposujudu,
Amka usiku fanya ibada, omba dua lako.
Chukua zawadi, chakula n.k(sadaka) tafuta watoto wa madrasa haswa wakiwa yatima itanoga, ambao hawajabalehe, ambao hawajaanza kufanya madhambi, dua zao huwa powerful.

Huko kwingine mnajiongezea dhambi tu. Ukishaweka akili kuwa hiki kikaratasi ndio kinanisaidia, hii pete ndio msaada tayari umekufuru tayari umefanya SHIRIKI
 
Nilikuwa Nina shida Fulani, itabidi nikamuone shekhe ndio anaweza kunisaidia, ila baada ya kunisomea Dua , akanipa hili karatasi kama niweke kwenye wallet

Naomba tasfiri yake wakuu, isije ikawa nimepewa jini kijanja, maana napata hela, sijui zinapo ishia
Hapo hio sio dua ya kukukinga wala kukusaidia, hiyo karata haitokufaisha chochote ni sawa na kulala na msahafu ndani ili wachawi wasikuroge msahafu haukukingi na chochote ispokuwa ukisoma yaliyomo ndani allah atakulinda sio kwa kukaa nao tu kama hiriz hausaidii.
 
Huo ni USHIRIKINA, choma moto mzee, tujitahidi kufanya ibada na maombi sisi wenyewe.
Laiti mngejua kuwa dua kupokelewa ina vipengele kadhaa lakini kimoja wapo ni USAFI wa muombaji, kwa dunia ya leo unaweza kwenda kwa sheikh kuomba dua kumbe sheikhe mwenyewe ni mchawi anaruka usiku, ni mshenzi anagonga mke wa mtu, kumbe ni anamla ndogo mtu, kumbe ni dhulumati, kadhulumu mali za yatima. Unategemea dua itapokelewa hiyo.

Tujitahidi kufanya ibada, tusome kidogo tujue dua zinapokelewaje..
Mfano funga sunna zako, jioni unapofuturu piga dua yako,
mola yupo karibu zaidi na mja wake pale anaposujudu,
Amka usiku fanya ibada, omba dua lako.
Chukua zawadi, chakula n.k(sadaka) tafuta watoto wa madrasa haswa wakiwa yatima itanoga, ambao hawajabalehe, ambao hawajaanza kufanya madhambi, dua zao huwa powerful.

Huko kwingine mnajiongezea dhambi tu. Ukishaweka akili kuwa hiki kikaratasi ndio kinanisaidia, hii pete ndio msaada tayari umekufuru tayari umefanya SHIRIKI
Nielekeze ndugu yangu!

Hapo nimesoma nimeona kaandika suratul Nasri (Idhajaa anasirullahi wal fat hu) akaandika mpaka akaishia kwenye fii dinillahi..

Baada ya hapo akaandika jina la Mungu. Yaani ya Allah! Kaliandika mara 11. Yaani Ya Allah! Ya Allah mpaka idadi ikafikia mara 11.

Baada ya hapo akamalizia sehemu ya aya "Afuwaja".

Baada ya hapo akachora jedwali! Upande mwengine kaandika herufi ya waw ya kiarabu. Kisha akachora symbol kama ya ua.

Huko kwengine kwa upande mwengine wa jedwali kaandika " Allahumma" mara 4.

Kisha kwa chini akaandika maneno yafuatayo "Mola wangu wewe ndiye mpaji na mimi ni mwombaji......" maneno ya kuomba.

Chini yake hapo akamswalia Mtume kisha akaweka na vialama vya nyota na alama alama nyengine.

Umeweka tahadhari kuwa ni ushirikina. Nisaidie kwa hapo ushirikina kinamna gani? Kwa maana na mimi nikiona kama hayo mahali pengine niweze kuwaelimisha watu.
 
Aya za Qu'ran na mengine yasioeleweka .
Nisaidie tafadhali kama yapi?

Nafahamu kiasi kiarabu.

Nimesoma hapo nimeona ni maombi ambayo alianza kuandika aya ya surat naswri.

Kwenye fii dinillah..kabla ya kumalizia llahi akaandika Ya Allah! Yaa Allah mara 11. Kisha akamalizia llahi.

Kwenye jedwali kaandika herufi waw! Kisha upande wa kushoto kaandika Allahumma mara 4.

Kisha chini kaandika maombi ya kuomba kwa mpaji ya kwamba hakuna mpaji kama wewe hali ya kuwa wewe mpaji na mimi ni mwombaji.

Akaandika kumswalia Mtume hapo chini kisha akamalizia na alama ya nyota na nyenginezo.

Lengo langu nisaidie ili nielewe zaidi. Ushirikina hapo upo wapi? Ni hayo maneno? Ni hilo jedwali? Ni hivyo vialama? Ni hiyo Aya? Au ni nini? Au ni vyote kwa pamoja?
 
Nielekeze ndugu yangu!

Hapo nimesoma nimeona kaandika suratul Nasri (Idhajaa anasirullahi wal fat hu) akaandika mpaka akaishia kwenye fii dinillahi..

Baada ya hapo akaandika jina la Mungu. Yaani ya Allah! Kaliandika mara 11. Yaani Ya Allah! Ya Allah mpaka idadi ikafikia mara 11.

Baada ya hapo akamalizia sehemu ya aya "Afuwaja".

Baada ya hapo akachora jedwali! Upande mwengine kaandika herufi ya waw ya kiarabu. Kisha akachora symbol kama ya ua.

Huko kwengine kwa upande mwengine wa jedwali kaandika " Allahumma" mara 4.

Kisha kwa chini akaandika maneno yafuatayo "Mola wangu wewe ndiye mpaji na mimi ni mwombaji......" maneno ya kuomba.

Chini yake hapo akamswalia Mtume kisha akaweka na vialama vya nyota na alama alama nyengine.

Umeweka tahadhari kuwa ni ushirikina. Nisaidie kwa hapo ushirikina kinamna gani? Kwa maana na mimi nikiona kama hayo mahali pengine niweze kuwaelimisha watu.
Kuweka kikaratasi hicho kutembea nacho kama hirizi hauoni kama ni njia ya shirki ? kwamba anaweka tu akiamini kuwa hiko kikaratasi ndio kinatatua shida zake.

Na hiyvo vitu vingine kwenye vilivyoongezwa unajua maana yake na kwa nini vimewekwa hapo ?
 
Nilikuwa Nina shida Fulani, itabidi nikamuone shekhe ndio anaweza kunisaidia, ila baada ya kunisomea Dua , akanipa hili karatasi kama niweke kwenye wallet

Naomba tasfiri yake wakuu, isije ikawa nimepewa jini kijanja, maana napata hela, sijui zinapo ishia
Nafikiri hayo mambo kawaulize watu wenye elimu zao kwa sababu kila mahali kuna watu wao! Hatuwezi kuhukumu jambo ambalo hatuna uwelewa nalo kamili.

Kila fani ina watu wake. Hilo suala ni watu wenye fani ya elimu ya Tiba.

Nabii Yaaqoubu A.S baada ya kupata upofu, Nabii Yusuf A.S ambaye ni mwanae kipindi hicho yupo Misri aliwapatia ndugu zake kanzu yake na kumwambia ajifutie usoni. Akifanya hivyo ataona!

Nabii Yaaqoub A.S akafanya hivyo na akaona! Kwenye Qur'an Surat Yusuf imeelezea hili.

Unaweza ukajiuliza kinachotibu ni nini? Ina maana hakumuombq Mungu? Au Manabii wa Mungu wote wawili wamefanya ushirikina?

Jawabu ni hapana! Isipokuwa kuna mambo yanaitwa kuwa kitu kinaitwa baraka na tawassuli.

Hivyo nikagundua elimu ni pana. Nakuwa muoga sana kuhukumu watu wanafanya ushirikina kwa suala ambalo sina elimu nalo.

Cha kufanya wauline watu wenye elimu hiyo ya Tiba.
 
Wanaloga tu hamna chochote.
Ushawahi kusikia, kusoma albadir kwenye bibilia?
Hiyo karatasi akiitia kwenye maji hayo maneno yakiyeyuka ukimwagiwa hayo maji au ofisini, njiani,nyumbani cha moto utakiona.
Inategemea na mnyama na ubaya unaemtuhumu.
Ukitaka afe mtu itasomwa mara 30 unatoa sadaka madrasa utasomewa dua ikitoka hapo unaoga maji yamewekwa hiyo karatasi huku unanuia.
Kesho humkuti mgomvi wako popote.
Na ukiweka ndani hujatumia akikua huyo unae.
Elimu Dunia 🙌
Mambo sio rahis hivo km mnavosumulia
 
Kuweka kikaratasi hicho kutembea nacho kama hirizi hauoni kama ni njia ya shirki ? kwamba anaweka tu akiamini kuwa hiko kikaratasi ndio kinatatua shida zake.

Na hiyvo vitu vingine kwenye vilivyoongezwa unajua maana yake na kwa nini vimewekwa hapo ?
Kaangalie kwenye Bukhari, Sunan Abu Dawud na Tirmidhi.

Abdallah ibn Amr ambaye ni sahaba wa Mtume alikuwa anaandika dua ambazo ni maneno ya Mtume ambazo alizisikia mwenyewe kutoka kwa Mtume anaandika kwenye karatasi na kuziweka kwenye mfumo ambao kwa kiswahili tunasema ni hirizi. Na kisha kuwavisha watoto wake shingoni kama ulinzi.

Ndiyo maana nauliza, tunavyosema shirki tuna elimu nalo?

Mimi elimu ya tiba sina! Ila ninachousia tuwe na uelewa wa kutosha kwenye masula ya elimu hususani kwenye kuhukumu halali na haramu.

Narudi tena kwako! Kuweka karatasi ni haramu kama hirizi? Kama ni haramu sahaba wa Mtume amefanya hivyo ambaye ni mwanafunzi wa Mtume.

Sahaba mwengine Ally naye alikuwa anaandika kombe kama shifaa.

Shiriki ni nini?
 
Nilikuwa Nina shida Fulani, itabidi nikamuone shekhe ndio anaweza kunisaidia, ila baada ya kunisomea Dua , akanipa hili karatasi kama niweke kwenye wallet

Naomba tasfiri yake wakuu, isije ikawa nimepewa jini kijanja, maana napata hela, sijui zinapo ishia
Matapeli wanakwambia ni nypta za bahati.

Hao hao wenyewe bahati hawana
 
Back
Top Bottom