Hiki kidonda nateseka sana nikienda haja, mwenye kujua dawa ya kuharisha

Hiki kidonda nateseka sana nikienda haja, mwenye kujua dawa ya kuharisha

Pole sana;
  • Kula vyakula vinavyolainisha choo; matunda, mboga za majani, nafaka n.k​
  • Kunywa maji mengi​
  • Fanya mazoezi ya kutembea, ikiwezekana ya kuruka ruka​
  • Usichelewe kwenda haja pale unapojisikia​
  • Tumia maji ya uvugu vugu katika kujisafisha​
  • Kama tatizo ni kubwa sana, dokta atakupa dawa ya kulainisha choo​
  • Kama maumivu ni makali, unaweza kutumia paracentam, brufen n.k ili kupunguza maumivu​
  • Pia unaweza kutumia dawa ya tube, kupaka eneo la haja 'nitroglycerin ointment'​
  • Upasuaji uwe ni hatua ya mwisho kama njia zingine zitashindikana​
 
A.alaykum wakuu, ninaomba msaada wenu jamani kwani ninapitia magumu sana, niende moja kwa moja kwenye mada
.
Kama mwezi mmoja umepita kuna siku nilienda haja kubwa, wakati najikamua nikapata maumivu kama nimechanika na kweli kinyesi kikatoka na damu kidogo... Nilirudi nyumbani kujichunguza vizuri nikakuta kweli nimechanika kidonda ni kikubwa kimetokeza kwa nje kimeingia hadi ndani, halafu kuzunguka kidonda pamevimba kiasi kwamba kuna kama linyama limening'inia chini likubwa, yaaani utaweza useme ni uvimbe umepasuka nashindwa hata kuelewa

Siku inayofata Nilienda RABININSIA HOSPITAL tegeta, doctor akaniangalia pamoja na maelezo yangu ( maana hili tatizo limeanza muda, mwanzo nilikuwa napata vidonda kwa nje kuzunguka eneo la haja kubwa, siku naamka asubuhi nakuta tu kidonda, nakiuguza siku ingine nakuta tu, kila siku ni vidonda tu kuzunguka eneo la haja kubwa, nikatumia dawa iyo hali ya nje ikapona sasa tatizo likawa ndani ) ko kwa maelezo yangu haya dr akanambia nina tatizo la anal fiscure sijui, kwa kiswahili mipasuko ya m.kundu akanipa tu dawa za kutumia ila kisipopona niende wanifanyie upasuaji
.
Sasa kilichonifanya niwaombe msaada ndugu zangu hichi kidonda nateseka sana nikienda haja, yaaani napata maumivu makali mnoo pamoja na damu nadhani choo kinakwangua, naombeni mnisaidie mwenye kujua dawa ambayo nikibanwa haja nakunywa then niwe naharisha tu, yaaani maumivu yake acha kbs, nisaidieni jamani
Hiyo ni chanzo cha fistura kama ile ya wanawake, dawa ni oparesheni kama atakavyoshauri dakitari.
 
Sasa kwanini uweke hapa nenda hospital za private nzuri utapata huduma
 
Mkuu usifanye upasuaji kwanza, nakuhakikishia kuna mtu anaweza kutibu, ndugu yangu wa kiume alikua hata kusimamisha ni shida ila amepina, hiyo ni wazi Bawaziri

Mpigie huyu
0747933658, ila nadhani ni sheikh sheikh, mida ya swala huwa hapokei. Pole sana
 
Hilo tatizo haliwezi kukuisha bila ya kunywa dawa za kulainisha choo, nakushauri unywe dawa za kienyeji ambazo zimethibitishwa na mamlaka husika vilevile utumie dawa ile ya kuponesha bawasiri, ipo ya kujipaka sehemu yenye jeraha, dawa za asili ndio zinaponesha hilo tatizo kwa uhakika japo ni gharama, kwa ushauri wa harakaharaka tembelea matawi ya dk Mwaka
Asnate sana kwa ushaur
 
Pole sana;
  • Kula vyakula vinavyolainisha choo; matunda, mboga za majani, nafaka n.k​
  • Kunywa maji mengi​
  • Fanya mazoezi ya kutembea, ikiwezekana ya kuruka ruka​
  • Usichelewe kwenda haja pale unapojisikia​
  • Tumia maji ya uvugu vugu katika kujisafisha​
  • Kama tatizo ni kubwa sana, dokta atakupa dawa ya kulainisha choo​
  • Kama maumivu ni makali, unaweza kutumia paracentam, brufen n.k ili kupunguza maumivu​
  • Pia unaweza kutumia dawa ya tube, kupaka eneo la haja 'nitroglycerin ointment'​
  • Upasuaji uwe ni hatua ya mwisho kama njia zingine zitashindikana​
Asante saana
 
Back
Top Bottom