Hiki kinachotokea kwa viongozi wakuu wa CWT (M/Kiti na Katibu wake) ni UONEVU wa waziwazi

Hiki kinachotokea kwa viongozi wakuu wa CWT (M/Kiti na Katibu wake) ni UONEVU wa waziwazi

Kama kunawizi wameufanya lazima washughulikiwe.Lakini kitendo cha kulazimisha kukubali uteuzi wa rais ni wa kipuuzi na kipumbavu.walimu walikataa uteuzi sababu ya kuona mambo ya hovyo yanayofanywa na huyu bibi huku wapuuzi wake wakimusifu.yaani wapuuzi kwa wapuuzi wanasifiana.utakubalije uteuzi kwa muuza nchi?
 
Uzuri JF ni anzisha uzi kaa pembeni acha wachangiaji wafata mkumbo wachangie bila hata kuujua ukweli... Mathamani aliondolewa na kikao halali Des 20 last year lakini bado alienda mahakamani... wenzie Seif na mwekahazina walikula mvua kwa ubadhilifu na matumizi mabaya ya ofisi. Nao wakapambana kesi ikafutwa.... wakalazimisha kurudishwa kwenye nafasi zao ila mkutano mkuu ukagoma... wameanzisha vita ya kumng'oa Japhet na wenzake... Kuna ujinga mwingi kiasi kwamba Bi tozo anatumika kwenye kuwaondoa waliopo kihali. Namshauri Rais atumie macho yake vizuri watu wabaki kufanya kazi. Pale ni majungu na fitina ndio vinaendelea na kwa jinsi walivyo wapuuzi tusubilie maafa.
 
Hawakuwa na busara unakataaje kazi unayotumwa na Mkuu wa nchi.Inabidi wajitathmini ikiwezekana wawapishe viongozi wengine waongoze hiyo Taasisi yao maana wao imewashinda.
Kwani lazima?....
Rais sio Mungu....Yupo wapi Nyerere, Mkapa, JPM...na waliobaki wapo njia moja...
Kila mtu apambane na hali yake...
 
Hao Cwt lazima waandamane kwa sababu wameonesha dharau kubwa kwa mh Rais .Mama alipanga kusolve mgogoro wao unaotokana na kugombea fedha za walimu Kiutu uzima lakini wao wakakomaza mafuvu kugomea teuzi za Udc hiyo ni dharau kubwa kwa mama.Kwa ushauri Serikali isiishie hapo tu kwa kuliacha hili suala la kudharau mamlaka ya uteuzi lipite ila waende mbele zaidi kwa kukifuta hicho kikundi cha wasaka ngawila kwa migongo ya vyama vya wafanyakazi
Tatizo la Watanzania tunaishi kwa mihemko, hatuna miongozo bali tunaishi ishi tu, uteuzi ni uteuzi tu unayo haki ya kuukubali au kuukataa. Inawezekena ulikuwa ni uteuzi wa kimagumashi wangeapishwa baada ya mwezi mmoja wanatenguliwa mwisho wa siku wanakosa pa kushika inabidi warudi kushika chaki.
 
Back
Top Bottom