Hiki kizazi mnaharibu sana Kiswahili "KUHEMEA" ndio maana yake nini?

Hiki kizazi mnaharibu sana Kiswahili "KUHEMEA" ndio maana yake nini?

Hyrax

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2023
Posts
964
Reaction score
2,675
Yaani nakutana na mfanyakazi wangu mmoja leo namuuliza ulikuwa wapi time niliyokuwa nakutafuta ananiambia boss nilitoka kuhemea nikamuuliza kuhemea ndio maana yake nini maana tayari kichwani nilishawaza mambo ya hovyo akaniambia kuhemea ni kwenda kununua mahitaji ya nyumbani yaani sikumuelewa hivi neno kuhemea ni kununua mahitaji ya nyumbani?
 
miaka ile ya njaa familia mbalimbali zilikua zikijigawa kwenda kuhemea chakula maeneo mbalimbali. Njaa haina adabu aise.

maeneo mengi hapakua na chakula cha bure, ilikua lazima kufanya kazi hatimae ndio mpewe chakula na kurejea nyumbani.

mliowaacha nyumbani, wakiulizwa wazazi wenu wamekwenda wapi. Jibu lilikua ni kwamba wameenda kuhemea 🐒
 
nilianza kulisikia Iringa ,na baadhi ya maeneo mengine mengi,ni kama limekuwa rasmi sasa.
Kwa upande wangu naona bora haya maneno yanayozuka yenyewe miongoni / katikati ya jamii kuliko yale baadhi ya maneno wanayoyaunda baraza la kiswahili Tz.BAKITA ofisini kwao halafu wanayarasimisha na kutuletea users mtaanj tuyatumie,mengine yamekaa kama vituko hata kuyatamka lakini unaambiwa ndio kiswahili fasaha.Na ndiyo yanachangia kufanya lugha ionekane ngumu.
Nafikiri lugha inavyokuwa inatakiwa izuke ijianzishe yenyewe miongoni mwa jamii.
USHAURI WANGU KWA BAKITA
Maneno kama haya yanayotumiwa sana na jamii ambayo yamezuka yenyewe na jamii inayakubali na sehemu kubwa ya jamii inayatumia katika kuwasiliana iyaingize katika lugha ya kiswahili iyarasmishe.
Tuchukulie mfano (USIOHALISI maana maneno mapya yaliyotungwa na bakita ni magumu na siyakumbuki kwa vile hayazoekeka kutumika katika jamii yetu kwa kuwasiliana.)
BODA BODA-piki piki ya abiria
BODA WANGU, au yule BODA-dereva wa boda
Hii ndio lugha inayotumiwa mtaani.
Sasa( bakita )wakikaa ofisini wakainda neno lao jipya wakija na neno tofauti neno au lugha tofauti na lugha au neno linalotumika mtaani na jamii/jina ambalo sehemu kubwa ya jamii imelizoea na inalitumia,Inaonekana ni kutuko au kichekesho.
inakuwa ngumu kulipokea na kulitumia katika uhalisia linabaki kwenye makaratsi ila si kutumika katika kuwasiliana na kufanya lugha ya SW kuwa ngumU na tofauti na inayotumika katika MAWASILIANO/KUWASIKIANA
ktk jamii,yani kunakuwa na lugha inayobaki kwenye makaratasi na inayotumika mtaani na sehemu kubwa ya jamii.Na hizi lugha mbili zikikutana zinakuwa gongana.ILA NI VIZURI KUCHUKUA ILE INAYOTUMIKA NA SEHEMU KUBWA YA JAMII KTK KUWASILIANA,ILIYOTOKANA NA SEHEMU KUBWA YA JAMII.
 
N
Yaani nakutana na mfanyakazi wangu mmoja leo namuuliza ulikuwa wapi time niliyokuwa nakutafuta ananiambia boss nilitoka kuhemea nikamuuliza kuhemea ndio maana yake nini maana tayari kichwani nilishawaza mambo ya hovyo akaniambia kuhemea ni kwenda kununua mahitaji ya nyumbani yaani sikumuelewa hivi neno kuhemea ni kununua mahitaji ya nyumbani?
Kakosea kutamka tu ila ni KUEMEA kwa maana ya kufanya manunuzi ya mahitaji ya nyumbani.
 
Duu kumbe bora hata umeuliza labda tutapata majibu,
Nimejiuliza sana hili neno. Je ni rasmi?

Lakini pia nikajiuliza kwa niniwasema kuhemea?
Nikawaza labda kile kitendo cha kwenda kununua vitu vilivyosambazwa chini, unaviinamia hivyo ni kama vile unavihemea/pumulia, Maana hii hutumika hasa kwenye manunuzi ya sokoni specifically vitu vya kula mf matunda, mboga, viungo n.k mostly vinatandazwa chini hasa huko kwa hao wenzetu.

BTW ni neno ambalo silipendi kabisa, maana hata unayemuuliza kwa nini mnaita kuhemea hana jibu, Kuna haja gani ya kuleta msamiati complicated, bora hata ingekua neno la kilunga, neno sokoni mbona lipo wazi tuu kwa kila mtu,
 
Pande za mbeya nilikutana na neno kujumua likiwa na maana sawa na kuhemea
Neno kujumua nilisikia mara ya kwanza kwenye wimbo wa Rayvanny, Chuma Ulete.

"Nyama tu, nikupe milioni kwani unapika kenge.
Si jana tu, nimelipa pochi na doti za vitenge.
Viatu juu, ulivyojumua kama una duka Mwenge"

Mpaka leo nahisi linamaanisha kununua vitu kwa wingi hasa kulenga kuuza rejareja.
 
Back
Top Bottom