Hiki kizazi mnaharibu sana Kiswahili "KUHEMEA" ndio maana yake nini?

Hiki kizazi mnaharibu sana Kiswahili "KUHEMEA" ndio maana yake nini?

Kujumua
nimekutana nayo iringa ikiwa na maana amenunu kwa bei ndogo bei ya jumla kwa ajili ya kwenda kuuza kwa bei kubwa kidogo apate faida.(Kuchuuza/mchuuzi)KUJUMUA KWA maana ya mfanya biashara
Neno moja linaweza likawa na maana zaidi ya moja .
Hilo neno lipo toka zamani ni nsamiati wa kusema natafuta kula, kama kuku anavyotafuta kula, anahemea.
Anataka kwenda "kupumulia" sokoni 🤣Sasa hapo hujaelewa nini kuhemea=kupumulia=kupolute
 
najua neno boda boda limerasmishwa kwwnye kamusi za kiswahili na kingereza.
nimeweka kama mfano usio halisi ,kwa kuwa maneno mapya yaliyotungwa na bakita ,binafsi siyakumbuki kwa kuwa ni mageni na kwangu ni magumu kwa vile hatuyatumii katika jamii yetu kuwasiliana ni mapya.au hayajazoeleka na wengi wetu.
Kiasi kwamba ukilisikia kwa mara ya kwanza unapata linakupa ukakasi.Kana kwamba jamii nzima miaka yote mlikuwa mnakosea kutumia maneno mliyokuwa mkiyatumia na kuwasilina au hamuijui au hakuwahi kuijua lugha yenu wenyewe ya kiswahili ISIPOKUWA bakita pekee ndio wenye kujua lugha ya kiswahili.
Ndio maana nikashauri ingefaa,wanapotunga maneno ni vizuri kutumia yale yaliyozoeleka na yanayotumika na sehemu kubwa ya jamii katika kuwasiliana.
Ndiyo maana nikasema huelewi unalozungumza. Omba ushauri haraka. Unaonekana uko nyuma ya wakati muda wote.
 
‘Kuhemea’ ni kiswahili cha kale sana, maana yake ni kukusanya mahitaji mbalimbali guluoni. Kwa kugha ya kisasa tunasema ‘Shopping’
 
Yaani nakutana na mfanyakazi wangu mmoja leo namuuliza ulikuwa wapi time niliyokuwa nakutafuta ananiambia boss nilitoka kuhemea nikamuuliza kuhemea ndio maana yake nini maana tayari kichwani nilishawaza mambo ya hovyo akaniambia kuhemea ni kwenda kununua mahitaji ya nyumbani yaani sikumuelewa hivi neno kuhemea ni kununua mahitaji ya nyumbani?
Kiswahili cha Kanda ya Ziwa hicho. Kama ni mzaliwa wa Pwani au Kaskazini huwezi jua hicho kiswahili.
 
Ni neno la aibu sana kule kwetu iringa!

Maana linatumiwa sana kipindi cha njaa,
Linatumiwa wakati umetoka nyumbani kwenda mbali kutafuta chakula kwa ajili ya familia.

Mara nyingi unakuta umetoka kijiji komoja hadi kingine kufuata mahindi tu
 
Mimi mwenyewe nimelisikia na kulizoea. Ni la miaka mingi. Oni Sigara na BAKITA yako tusaidie.
 
Mkuu neno hemea ni la Kiswahili wala halijaharibu Kiswahili, likimaanisha toka mahali pako wakati wa shida ya njaa kwenda kwingine kutafuta chakula. Kamusi za Kiswahili sanifu zimeainisha.
 
Kuhemea ni kula slope kwa mtu mwingine kwasababu huna uwezo wa kujitunza

SHOPPING SIO KUHEMEA
Hii maana uliyotoa hapo nadhani mmekuwa mnaitumia huko kwenu. Mimi ni mzaliwa wa Mwanza miaka ya 80. Tangu nikiwa mdogo, hilo neno lilikuwa linatumika kumaanisha kutafuta/kununua mahitaji ya nyumbani.

Huenda ukawa ulikulia kwingine na huko kukawa na maana nyingine. Kwenye mazingira yetu, mtu alikuwa anasema anaenda kuhemea au anaenda kufanya mahemezi. Kwa kizazi cha kileo, ni rahisi sana kusikia mtu akisema anaenda 'shopping' badala ya 'kuhemea'. Nadhani umeelewa hoja yangu.
 
Back
Top Bottom