Hiki kizazi mnaharibu sana Kiswahili "KUHEMEA" ndio maana yake nini?

Kujumua
nimekutana nayo iringa ikiwa na maana amenunu kwa bei ndogo bei ya jumla kwa ajili ya kwenda kuuza kwa bei kubwa kidogo apate faida.(Kuchuuza/mchuuzi)KUJUMUA KWA maana ya mfanya biashara
Neno moja linaweza likawa na maana zaidi ya moja .
 
Mkuu Hyrax , naona leo umeamua kulipingana neno sahihi kabisa la Kiswahili.

NB: Halafu hii sentensi yako imekaaje? Mbona ni ndeeeefu na wala haionekani wapi umeweka japo kituo kimoja au mkato? Yaani ni mwendo wa vurugu mechi! Nadhani ugonjwa unao wewe. Inasikitisha kwamba huuoni.
 
Ungekuwa unazungumza kwa mayakini (facts), kamwe usingeweka huo mfano. Naweza kusema kisahihi kwamba wewe ndiye uko nyuma ya wakati.
 
Kuna maneno mawili unachanganya: kuemea na kuhemea. Haya mawili ni sahihi, yenye maana tofauti kabisa.
 
 
ni kweli sijaweka mifano halisi ya maneno ya kiswahili yaliyotungwa na BAKITA .
kwakuwa ni maneno magumu ambayo siyakumbuki ambayo ni tofauti na maneno yanayotumika na jamii mtaani katika mawasiliano.
Nikiyakumbuka nita yashare hapa.
Una hakika neno bodaboda halijasanifiwa na kuingizwa kwenye lugha rasmi ya Kiswahili? Hilo ndilo swali langu.
 
Una hakika neno bodaboda halijasanifiwa na kuingizwa kwenye lugha rasmi ya Kiswahili? Hilo ndilo swali langu.
nimesema sijaweka mfano halisi

Ni kweli sijaweka mfano halisi wa maneno yaliyorasimishwa na BAKITA kutumika .,ambayo kiukweli ni mageni na ni magumu na yapo tofauti na maneno yaliyozoeleka na jamii kwa maana ileile na yanayotumiwa na jamii kuwasiliana.
 
Una hakika neno bodaboda halijasanifiwa na kuingizwa kwenye lugha rasmi ya Kiswahili? Hilo ndilo swali langu.
najua neno boda boda limerasmishwa kwwnye kamusi za kiswahili na kingereza.
nimeweka kama mfano usio halisi ,kwa kuwa maneno mapya yaliyotungwa na bakita ,binafsi siyakumbuki kwa kuwa ni mageni na kwangu ni magumu kwa vile hatuyatumii katika jamii yetu kuwasiliana ni mapya.au hayajazoeleka na wengi wetu.
Kiasi kwamba ukilisikia kwa mara ya kwanza unapata linakupa ukakasi.Kana kwamba jamii nzima miaka yote mlikuwa mnakosea kutumia maneno mliyokuwa mkiyatumia na kuwasilina au hamuijui au hakuwahi kuijua lugha yenu wenyewe ya kiswahili ISIPOKUWA bakita pekee ndio wenye kujua lugha ya kiswahili.
Ndio maana nikashauri ingefaa,wanapotunga maneno ni vizuri kutumia yale yaliyozoeleka na yanayotumika na sehemu kubwa ya jamii katika kuwasiliana.
 
Wewe ni wa kizazi kipi! Neno kuhemea si jipya ni la tangu enzi za Adamu na Hawa likiwa na maana ya kutafuta chakula cha siku kwa watu walio masikini.
Nadhani wewe umezaliwa Marekani na umekuja hapa na kuishi maisha ya mboga nne, kwa hali hii si ajabu wewe kutolijua neno "kuhemea".
 
Hilo neno si la kizazi hiki, bali la kizazi kile. Ninakaribia miaka 40 na hilo neno nimekua nalisikia likiwa na maana ya kununua mahitaji ya nyumbani. Kizazi hiki wanasema 'shopping/kununua groceries'.
"Shopping" ni neno linalotumiwa na watu wenye uwezo wa manunuzi ya kila kitu.
"Kuhemea" ni neno linalotumiwa na masikini wanapotafuta chakula cha siku, hauwezi kuhemea vitu au vifaa.
 
Hilo neno lipo toka zamani ni nsamiati wa kusema natafuta kula, kama kuku anavyotafuta kula, anahemea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…