Hiki kizazi mnaharibu sana Kiswahili "KUHEMEA" ndio maana yake nini?

 
Ndiyo maana nikasema huelewi unalozungumza. Omba ushauri haraka. Unaonekana uko nyuma ya wakati muda wote.
 
‘Kuhemea’ ni kiswahili cha kale sana, maana yake ni kukusanya mahitaji mbalimbali guluoni. Kwa kugha ya kisasa tunasema ‘Shopping’
 
Kiswahili cha Kanda ya Ziwa hicho. Kama ni mzaliwa wa Pwani au Kaskazini huwezi jua hicho kiswahili.
 
Ni neno la aibu sana kule kwetu iringa!

Maana linatumiwa sana kipindi cha njaa,
Linatumiwa wakati umetoka nyumbani kwenda mbali kutafuta chakula kwa ajili ya familia.

Mara nyingi unakuta umetoka kijiji komoja hadi kingine kufuata mahindi tu
 
Mimi mwenyewe nimelisikia na kulizoea. Ni la miaka mingi. Oni Sigara na BAKITA yako tusaidie.
 
Mkuu neno hemea ni la Kiswahili wala halijaharibu Kiswahili, likimaanisha toka mahali pako wakati wa shida ya njaa kwenda kwingine kutafuta chakula. Kamusi za Kiswahili sanifu zimeainisha.
 
Kuhemea ni kula slope kwa mtu mwingine kwasababu huna uwezo wa kujitunza

SHOPPING SIO KUHEMEA
Hii maana uliyotoa hapo nadhani mmekuwa mnaitumia huko kwenu. Mimi ni mzaliwa wa Mwanza miaka ya 80. Tangu nikiwa mdogo, hilo neno lilikuwa linatumika kumaanisha kutafuta/kununua mahitaji ya nyumbani.

Huenda ukawa ulikulia kwingine na huko kukawa na maana nyingine. Kwenye mazingira yetu, mtu alikuwa anasema anaenda kuhemea au anaenda kufanya mahemezi. Kwa kizazi cha kileo, ni rahisi sana kusikia mtu akisema anaenda 'shopping' badala ya 'kuhemea'. Nadhani umeelewa hoja yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…