Hiki ndiyo kituko nlichowahi kukutana nacho makaburini usiku. Sitosahau

Hizi ishu zinatokea ila hiyo image unavyoona ni ubongo wako mwenyewe tu unakudanganya kwa vile una hofu ya kufirikia kitu fulani kwa sana[emoji28][emoji28][emoji28]...Hii inasababishwa na akili za kitoto
No huwezi kusema ni hofu wakati jamaa anasema kwake kupita hapo ilikua kama torati,ni sehemu alishazoea kupita so hakua na hofu nayo
 
No huwezi kusema ni hofu wakati jamaa anasema kwake kupita hapo ilikua kama torati,ni sehemu alishazoea kupita so hakua na hofu nayo
Kumbe umenielewa mkuu, nahisi huyo mungine hakusoma vizuri akaelewa nilichoandika.
 


β€œRatiba yangu kwa siku ilikuwa ni shule kwanza, nlipotoka shule, nlielekea mazoezini (mpirani), baada ya kutoka mpirani ndo nikawa naenda sasa kujipoza vibandani kumuangalia Dharmendra, Amita Bachan, Rambo, Anord, Bruce Lee nk"

Kwa ratiba hii, silipi school fee, nenda tu uanze maisha.
 
Ilikuwa balaa, nahisi walitaka nizubae kidogo ili iwe rahisi kunifikia na kuniteka [emoji23][emoji23][emoji23]
No wangetaka kukufika wala wasingeshindwa pia wangetaka ukutane nao kule ulipokimbilia walikua na uwezo huo,sema tuu waliamua kukuonyesha kuwa wapo viumbe wa aina hio
 


Hemu tuambie ulisoma mpaka degree ngapi? Maama kwa hiyo ratiba hukupaswa kuwa mwanafunzi.
 
Jf Raha tupu apa wacha nikatafute utumbo πŸ˜„
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ uwe makini usije kuuziwa utumbo wa kenge. Asilimia kubwa ya binadamu wa leo wametoboka roho, hakuna anaejali mungine πŸ˜‚πŸ˜‚
 
No wangetaka kukufika wala wasingeshindwa pia wangetaka ukutane nao kule ulipokimbilia walikua na uwezo huo,sema tuu waliamua kukuonyesha kuwa wapo viumbe wa aina hio
Nafikiri lengo lilikuwa hilo hilo ulilosema. Maana kama kupita nilikuwa napita sana tu. Na nahisi walikuwa wananiona.

Ila siku hiyo pengine walitaka kunionesha kuwa wapo na huwa wananiona sana nikipita.
 
Hivi viumbe vya majini Huwa niga nao story sana,SEMA hawataki mambo ya kiwaki
 
Nafikiri lengo lilikuwa hilo hilo ulilosema. Maana kama kupita nilikuwa napita sana tu. Na nahisi walikuwa wananiona.

Ila siku hiyo pengine walitaka kunionesha kuwa wapo na huwa wananiona sana nikipita.
Yeah mimi binafsi nashukuru sijawahi kukutana na hayo mauzauza na naomba nisikutane nayo mpaka siku nakufa ila naamini hivi viumbe vipo sana tuu
 
Vitu vya ajabu vipo sana ,nakumbuka kipindi nipo kidato cha tatu mwaka 2005 shule x maeneo ya shiyanga.
Baada ya kutoka kwenye kipindi kile cha usiku mida kama ya saa nne kasoro hivi ,kwenye mabweni kuna uwanja wa mpira wa kikapu na baada ya uwanja unavuka barabara kuna kipori fulani

Sasa kwenye pori hilo tulikuwa tunapenda kwenda kujisaidia kama unavyojua vyoo vya shule kukuta vichafu ni jambo la kawaida kwa kipindi kile,hivyo kuna baadhi hatukupendelea kujisave toilet hasa mida ya usiku.
Tulikuwa na tabia ya kualikana kwenda pori kujisave ,sa siku hiyo nikakosa wadau ,ikabidi niliunge mwenyewe nikazama pori peke angu,

Nilienda nikavuka barabara,nikavuka kiwanja cha mipira wa kikapu ,huyooo pori .
Nilijisaidia ,ile nipo hatua ya kumaliza nikashangaa naona gari linapita mle porini,yani kulingana na hali ya pori kwa gari kupita haiwezekani,pana miti ,mashimo ,mawe,visiki nk.

Ila pamoja na hali yote hiyo ile gari ilipita hadi kwenye miti ,inakuwa kama inaigonga miti lakini inazidi kutokomea.
Niliduwaa sana pale chini nilipokuwa nimechuchumaa kwa mana ilipita mbele yangu upande wa kule nilikotoka.

Nilichomoka mbie kutoka huko pori hadi kwenye dom langu.Niliogopa sana ,sikujua kabisa maana ya ile gari iliyo kuwa imejaa watu ikipita kwenye sehemu yenye vikwazo vya miti na vichaka vyote bila tatizo utazani ipo kwenye lami.
Tangu siku hiyo sikurudia kwenda porini kujisaidia.
 
Shule, mpira, video, karate?
Niliandaa maisha yang katika pande zote muhim kama vile elimu na michezo.

Sema ndo hivyo binadam tunapanga yetu na Mungu nae anapanga yake hivyo nilipishana na malengo yangu. Kama wewe mtu mzima utakuwa umeifungua code niliyoweka hapa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…