Hiki ndiyo kituko nlichowahi kukutana nacho makaburini usiku. Sitosahau

Hiki ndiyo kituko nlichowahi kukutana nacho makaburini usiku. Sitosahau

Tumetoka jisomea kama saa 5 usiku hivi, tukawa tunapita maeneo ya makaburi. Tulikuw wa nne, na kulikuwa na mbalamwez usiku. Cha ajabu nikuw tupo wanne ila vinvuli vipo vitano, nikawaambia wenzangu kinvuli cha tano cha nan? Wote tukahamaki !! Tukasema isiwe kesi tunyooshe mkono juu afu tuone kama kivuli cha ni nan? Hee si kimvuli cha 5 kikanyoosha.

Tukasema bhas kilammoja aanze tembea wengine tusimame wakwanza akaenda mbele na kimvuli chake kikamfuata, wapili, na hata watatu. Wa mwisho mim ile niende mbele si nikaona nna fuata na vimvuli viwili na sio vile viwili kwamba kuna mianga mbalimbali hapana. Cha kushangaza baadae kimvuli kikaaanza kuwa kirefuu oya nasema oyaa hizo nduki tulikimbia sio nchii hii ya kufungwa na morocco [emoji4]. Kama bolt hussein tuu tulikimbia sana
 
Umeitaja hiyo Loha umenikumbusha mbali sana. 1993 (std 2) 1994 (std 3) 1995 (std 4)

Mambo ya Amrish Puri na Mithun Chakraboth.

Movie yangu pendwa ilikuwaga Tridev (Oye Oye) Dance Dance, Disco Dancer, Vishwatmar, Andha Kanoon

Nolstagia is real
duuh watu ni wakongwe sana humu inabdi tuwe tunawaamkia aisee
heshima yako🤣
 
Nje ya mada.
Naomba kuuliza. Hivi wale wanaoimba live band, wanavaaga vitu fulan kama earphones masikioni... nini vitu gani vile?? Au ni ear phones??
 
Niaje waungwana,

Hiki kisa, au tukio lilintokea miaka mingi kidogo. Enzi zile za kwenda kuangalia movie katika vibanda vya video. Sasa siku hiyo nilienda kuangalia video katika banda moja nililokuwa napenda kwenda kuangalia.

Banda hilo lilikuwa maeneo ya Manzese Midizini kwa mama fulan jina kapuni, na mimi home ni maeneo ya Magomeni mikumi jijini Dar es Salaam.

Njia yangu kubwa kutoka home hadi Midizini, ilikuwa kagera kimamba, nakatiza daraja la mbao, napandisha pale Mburahati Mianzini, napasua Makaburi ya Mburahati kwa jongo hadi midizini. Na kurudi i was doing the same thing kwa kufuata njia ile ile niliyokuja nayo.

Ratiba yangu kwa siku ilikuwa ni shule kwanza, nlipotoka shule, nlielekea mazoezini (mpirani), baada ya kutoka mpirani ndo nikawa naenda sasa kujipoza vibandani kumuangalia Dharmendra, Amita Bachan, Rambo, Anord, Bruce Lee nk.

Ratiba yangu ya mwisho baada ya kutoka huko katika banda la video, ilikuwa ni kwenda katika maskani yetu fulan ambayo ni ya uncle wangu kujifunza mchezo wa karate. Uncle ndo alikuwa masta wetu. Hivyo nilijiamini sana kwamba hakuna kitu au mjinga yeyote anaeweza kunifanyia ushen.z.i mbele yangu. Karate na ngumi ni michezo ambayo humfanya mchezaji ajiamini sana, kwamba anaweza kupambana na mtu yoyote, mahali popote na kwa muda wowote.

Basi bwana siku hiyo nimemaliza kumuangalia Dharmendra mida ya usiku, nakumbuka ilikuwa movie fulan inaitwa LOHA. Tukatoka kila mtu akawa anaelekea kwao. Mimi nikawa natambaa mdogo mdogo kuelekea home.

Nilivyofika katika makaburi ya mburahati kwa jongo kama kawaida yangu, nikageuka nyuma kuangalia huku na huko, sikuona mtu ananifuata nikaendelea na safari yangu.

Sasa nimesogea sogea hadi katikati ya makaburi, kwa mbele nikaona kitu kama mbuzi mweupe, lakini kilichonishangaza na kunitia hofu ni kwamba yule mbuzi alikuwa kama vile amekaa kwenye kitu anavuta sigara, nikafikicha macho kama vile siamini ninachokiona.

Nikaendelea kusogea taratibu ili nihakikishe kuwa ninachokiona ni chenyewe au.

Kusogea nikasikia mbuzi anakohoa, ikabidi nigeuke ili nitoke nduki maana niliona pale hata karate zangu haziwezi kunisaidia.

Sasa wakati nageuka nikaona nyuma yangu kuna kundi la watu wamebeba jeneza wanakuja upande wangu halafu juu ya jeneza kuna mtu kakaa na yeye anavuta fegi, halafu kila jamaa wakipiga hatua, yeye anajamba.

Nikaona nyuma hakufai bora huku huku nilipotaka kupakimbia. Nikageuka na kuanza kutoka nduki kuelekea kwa mbuzi anaevuta sigara. Ghafla nikaona na mbuzi na yeye anatoka nduki na sigara yake.

Akili ikanijia nikaacha kukimbia ule upande anakimbilia mbuzi, nikaelelea upande wangu.

Breki ya kwanza ikawa Magomeni Mapipa, yani sikumbuki hata mikumi home nilipapita saa ngapi, au kule Mapipa nilifika fikaje fikaje.

Nikarudi nyumbani salama. Toka siku hiyo sikurudi tena kwenda video usiku, na ukawa mwisho wa kuendekeza movie.

Ni nani mwngine ambae ashawahi kukumbana na songombingo la aina hiyo?

Aisee it was scary
utoke shule, ukacheze mpira, uende muvi, kisha karate
uongo wa hali ya juu
kwanza kutoka mikumi hadi manzese siyo mchezo ,ni mbali kinoma
 
Ukiona hivyo ujue Mungu yuko upande wako.

Kipindi fulani nilienda Rufiji mwisho kabisa katika kijiji fulani kinaitwa mloka. Kutokana na ubovu wa barabara na mvua ilinyesha nyingi tukafika kule usiku kama saa 6 hivi.

Japo ilikuwa usiku na tuliruhusiwa kulala ndani ya gari, lakini mimi sikutaka kulala ndani ya gari, nikaona bora niende kulala katika gesti ya karibu alafu asubuhi niendelee mpaka kijijini. Gesti ya pale stand ilijaa hivyo nikapata nyingine ya pembeni kidogo na stand.

Nimeoga nikaingia ndani kujipumzisha huku nachungulia chungulia JF kama ilivyo kawaida yetu members. Ilipofika mida ya 7 na nusu nikaanza kuhisi nywele kusisimka, alaf kama vile nahisi nimekaa na watu ila siwaoni. Nikawa siijali ile hali nikahisi labda ni hali ya mchoko tu anbayo imesababisha akili nayo ichoke. Baadae nikaona mlango wangu unafunguliwa, na wakati nilifunga kwa ndani. Ila baada ya kufunguliwa sikuona mtu anaingia. Nikanyanyuka taratibu kuelekea mlangoni ili kuchungulia na kujua ni nani aliefungua mlango ule.

Sikuona mtu nikaufunga, nikarudi kitandani. Ghafla nikaona kitanda changu kishakuwa upande mungine wa dirisha, nikasema msinitanie, nikatoka nje nikaenda kukaa katika kibaraza kilicho karibu na dirisha langu alafu nikachukua sim nikaweka movie ya X (porn) nikaweka kasauti kakubwa kidogo, nikawa naongea mwenyewe nasema kama kuna mtu anataka kuangalia na mimi hii movie ruhusa.

Kumbe wale jamaa wakiwa katika mambo yao huwa hawapendi mambo ya kijinga jinga namna hiyo. Nikasikia bonge la msonyo alafu eneo likawa kimya. Mimi sikurudi ndani wala sikulala. Ilipofika saa 11 alafajir, nikaoga na kuondoka zangu kuelekea kijijini.

Nilipowaeleza wenyeji wangu, wakasema jamaa walikuwa wanakuja kukupima, ila wakagundua kuwa wanaempima mwenyewe ameshavurugwa tayari na maisha. So wakaamua kwenda kumtafuta mnyonge mungine kule katika gest ya stand 😂😂😂
Haya mambo hatari sana😂
 
Kaka hao masizimwe ni vibwengo, majini, mizuka au misukule?
Maana mpaka leo sijajua wale walikuwa ni viumbe gani 😂😂😂
🤣🤣🤣We Toka lini mbuzi Kavita kafegi ulitaka kuuvaaa mtumbwi wa vibwengo Mshukuru Mungu kujupa akili yakupita njia yako maana ndio ulikua unaondoka hivo iliwainikuta. Iyo miaka ile tunasoma nawai namba shule mwali mwenyew mwananzo mwisho fimbo haambiwi kumbe nimeamka saa tisa nasema saa kumi na mbili nilikutana na jitu ilo mitaa ya shule mzee chini linakwato za ng'ombe aseee nikicheki juu sioni mwisho ilibidi tukatafute mlinzi wapi yupo kumbe nae alikiona weeee tangu siku ile tulilipoti kwa mkuu washule ikatangazwa sikuwai kuwaishule tn ilibidi nikubaliane na viboko🤣
 
Huyo mbuzi mwenye ako na fegi kwa bedroom ya dead body nadhani was young lunya smoking weed
 
kuna mwamba mmoja alikuwa kama wewe, haamini uchawi. unashindwaje kuamini uchawi upo kama unaamini shetani yupo na Mungu yupo? kilichotokea, kuna siku zile za popo bawa wamesafiri kwenda zenji, aliamka suruali kwa nyuma ina kitu kama utelezi wa yai. alivurugwa akili si mchezo.
Popobawa ni proof nyingine ya ufinyu wa akili za watanzania.
Hizo ni pranks tu watu walimfanyia akaingia kingi
 
Tumetoka jisomea kama saa 5 usiku hivi, tukawa tunapita maeneo ya makaburi. Tulikuw wa nne, na kulikuwa na mbalamwez usiku. Cha ajabu nikuw tupo wanne ila vinvuli vipo vitano, nikawaambia wenzangu kinvuli cha tano cha nan? Wote tukahamaki !! Tukasema isiwe kesi tunyooshe mkono juu afu tuone kama kivuli cha ni nan? Hee si kimvuli cha 5 kikanyoosha.

Tukasema bhas kilammoja aanze tembea wengine tusimame wakwanza akaenda mbele na kimvuli chake kikamfuata, wapili, na hata watatu. Wa mwisho mim ile niende mbele si nikaona nna fuata na vimvuli viwili na sio vile viwili kwamba kuna mianga mbalimbali hapana. Cha kushangaza baadae kimvuli kikaaanza kuwa kirefuu oya nasema oyaa hizo nduki tulikimbia sio nchii hii ya kufungwa na morocco [emoji4]. Kama bolt hussein tuu tulikimbia sana
Mauza uza ni mengi tu duniani. Ila kama mtu hajakumbana nayo inakua vigumu kukubali.

Pole kwa kuchapwa tatu. Ndo ukubwa huo 😂😂
 
Nje ya mada.
Naomba kuuliza. Hivi wale wanaoimba live band, wanavaaga vitu fulan kama earphones masikioni... nini vitu gani vile?? Au ni ear phones??
Ngoja wajuzi waje watoe jibu.
 
Back
Top Bottom