Hiki ndiyo kituko nlichowahi kukutana nacho makaburini usiku. Sitosahau

Hiki ndiyo kituko nlichowahi kukutana nacho makaburini usiku. Sitosahau

Makaburini: Ni sehemu iliyojaa upweke na ukiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiki kisa kimenivunja mbavu zangu 😂😂😂
 
Hizi story ndo zinaendelea kufanya jamii za waafrika kuendelea kua wajinga wa fikra na maskini wakati mataifa mengine yanapiga hatua,
By the way huu uzi unatakiwa upelekwe jokes
kuna mwamba mmoja alikuwa kama wewe, haamini uchawi. unashindwaje kuamini uchawi upo kama unaamini shetani yupo na Mungu yupo? kilichotokea, kuna siku zile za popo bawa wamesafiri kwenda zenji, aliamka suruali kwa nyuma ina kitu kama utelezi wa yai. alivurugwa akili si mchezo.
 
Nilikuwa nandesha BAISKERI Saa 5 usiku nipo kasi bonde la mkwajuni natoka magomeni naitafuta MWANANYAMALA
Mbele wakapita watu wamebeba jeneza
Nikakumbuka story za VIJIWENI
nikasema hapa sifungi brake nitakufa Kwa ajari mbaya nikapita katikati ya mazishi
sielewi ilikuwaje ila kuja kushituka nipo VIJANA SOCIAL HALL
MANGO GARDEN walikuwa TWANGAPEPETA nikaenda kucheza muziki
😂 ungefunga breki kesho ugeuke sad story vijiweni
 
Niaje waungwana,

Hiki kisa, au tukio lilintokea miaka mingi kidogo. Enzi zile za kwenda kuangalia movie katika vibanda vya video. Sasa siku hiyo nilienda kuangalia video katika banda moja nililokuwa napenda kwenda kuangalia.

Banda hilo lilikuwa maeneo ya Manzese Midizini kwa mama fulan jina kapuni, na mimi home ni maeneo ya Magomeni mikumi jijini Dar es salaam.

Njia yangu kubwa kutoka home hadi Midizini, ilikuwa kagera kimamba, nakatiza daraja la mbao, napandisha pale Mburahati Mianzini, napasua Makaburi ya Mburahati kwa jongo hadi midizini. Na kurudi i was doing the same thing kwa kufuata njia ile ile niliyokuja nayo.

Ratiba yangu kwa siku ilikuwa ni shule kwanza, nlipotoka shule, nlielekea mazoezini (mpirani), baada ya kutoka mpirani ndo nikawa naenda sasa kujipoza vibandani kumuangalia Dharmendra, Amita Bachan, Rambo, Anord, Bruce Lee nk.

Ratiba yangu ya mwisho baada ya kutoka huko katika banda la video, ilikuwa ni kwenda katika maskani yetu fulan ambayo ni ya uncle wangu kujifunza mchezo wa karate. Uncle ndo alikuwa masta wetu. Hivyo nilijiamini sana kwamba hakuna kitu au mjinga yeyote anaeweza kunifanyia ushen.z.i mbele yangu. Karate na ngumi ni michezo ambayo humfanya mchezaji ajiamini sana, kwamba anaweza kupambana na mtu yoyote, mahali popote na kwa muda wowote.

Basi bwana siku hiyo nimemaliza kumuangalia Dharmendra mida ya usiku, nakumbuka ilikuwa movie fulan inaitwa LOHA. Tukatoka kila mtu akawa anaelekea kwao. Mimi nikawa natambaa mdogo mdogo kuelekea home.

Nilivyofika katika makaburi ya mburahati kwa jongo kama kawaida yangu, nikageuka nyuma kuangalia huku na huko, sikuona mtu ananifuata nikaendelea na safari yangu.

Sasa nimesogea sogea hadi katikati ya makaburi, kwa mbele nikaona kitu kama mbuzi mweupe, lakini kilichonishangaza na kunitia hofu ni kwamba yule mbuzi alikuwa kama vile amekaa kwenye kitu anavuta sigara, nikafikicha macho kama vile siamini ninachokiona.

Nikaendelea kusogea taratibu ili nihakikishe kuwa ninachokiona ni chenyewe au.

Kusogea nikasikia mbuzi anakohoa, ikabidi nigeuke ili nitoke nduki maana niliona pale hata karate zangu haziwezi kunisaidia.

Sasa wakati nageuka nikaona nyuma yangu kuna kundi la watu wamebeba jeneza wanakuja upande wangu halafu juu ya jeneza kuna mtu kakaa na yeye anavuta fegi, halafu kila jamaa wakipiga hatua, yeye anajamba.

Nikaona nyuma hakufai bora huku huku nilipotaka kupakimbia. Nikageuka na kuanza kutoka nduki kuelekea kwa mbuzi anaevuta sigara. Ghafla nikaona na mbuzi na yeye anatoka nduki na sigara yake.

Akili ikanijia nikaacha kukimbia ule upande anakimbilia mbuzi, nikaelelea upande wangu.

Breki ya kwanza ikawa Magomeni Mapipa, yani sikumbuki hata mikumi home nilipapita saa ngapi, au kule Mapipa nilifika fikaje fikaje.

Nikarudi nyumbani salama. Toka siku hiyo sikurudi tena kwenda video usiku, na ukawa mwisho wa kuendekeza movie.

Ni nani mwngine ambae ashawahi kukumbana na songombingo la aina hiyo?

Aisee it was scary
😂😂😂😂😂 Wakipiga hatua,alie kaa juu ya jeneza anafanyeje?🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
kuna mwamba mmoja alikuwa kama wewe, haamini uchawi. unashindwaje kuamini uchawi upo kama unaamini shetani yupo na Mungu yupo? kilichotokea, kuna siku zile za popo bawa wamesafiri kwenda zenji, aliamka suruali kwa nyuma ina kitu kama utelezi wa yai. alivurugwa akili si mchezo.
Popo bawa hupenda kuwashughulikia watu wa aina ya huyo anaebisha 😀😀😂
 
😂😂😂😂😂 Wakipiga hatua,alie kaa juu ya jeneza anafanyeje?🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Nasikia puu puu puu nikaona isiwe shida acha niokoe nafsi kwanza
 
Alikuwa peke yake, lakini angefunga break angeshangaa gari imetokea kwa nyuma yake na kumgonga ghafla. Asubuhi tungesikia jamaa amekutwa amefariki njiani.
Hizi mambo zipo sana nakumbuka kama wiki mbili zimepita nilikuwa mkoani, muda ni saa 8 usiku sijalala nipo jf napitia nyuzi ghafla nikasikia mlio wa kitu kimedondoka kutoka juu, nikashtuka nikaangaza ni nini sikuona na kwa mazingira yale hakukuwa na chochote kile zaidi ya kitanda na kochi. Nikaangalia pc ipo kwenye kochi nikabaki najiuliza bila majibu ni nini kimedondoka na kutoa kishindo ili hali pale hakukuwa na chochote kinachoweza kutodondoka kutoka juu? Sikuogopa nikasema mi nalindwa na Mungu jichanganyeni nikaendelea na jf then nikalala.
 
Hapo ulipokuwepo wazee wa kazi walikuwa wanataka kupatumia kwa mambo yao. Sasa inasemekana kuwa wanga huwa hawafanyi mambo yao sehemu yenye mwanga wa taa. Ndomaana wanapoona mtu amekaa usiku anaangalia tv au kuchat na sim, kama na yeye akiwa na kinga ya Mungu, watachofanya ni kumvanyia vitimbi kama hivyo ili wamtie hofu azime tv au sim.

Na akishazima tv au sim hata kama ana hofu haitochukua dakika 5 singizi zito litampitia ghafla, akija kushtuka kumekucha tayari na wazee wa kazi tayari wameshafanya mambo yao na kuondoka. Mshana Jr
 
Sikuruhusu hilo maana nilichelewa sana kulala na taa ilikuwa on muda wote kabla ya kulala.
 
Enzi zangu nilivyokua napenda ujinga ujinga siku moja Nilikua dodoma Area A nikawa naenda kupanda daladala kwaajili ya kuelekea Fourways njiani kuna sehem moja kuna makaburi ilikua ni jion giza limeanza kuingia, wakati nakatiza pale makaburini nyuma yangu nikaona wadada wawili wanatembea haraka kuniwahi ili tuvuke wote

Walivyofika wakawa wanatembea nyuma yangu tukasalimiana wakaniambia bora hata wameniona maana walikua wanaogopa kuvuka makaburini peke yao mi nikawajibu msijali hata mimi nilivyokua hai kama nyie nilikua naogopa sana kupita makaburini

Walikimbia hadi mimi mwenyewe nikaogopa nikaanza kukimbia pia
 
Sikuruhusu hilo maana nilichelewa sana kulala na taa ilikuwa on muda wote kabla ya kulala.
Kwa vile hukupata hofu ya kuzima taa, basi walibadili mpango wao. Wakaenda sehemu nyingine yenye giza kuendelea na kikao chao.
 
Back
Top Bottom