Hiki ndiyo kituko nlichowahi kukutana nacho makaburini usiku. Sitosahau

Hiki ndiyo kituko nlichowahi kukutana nacho makaburini usiku. Sitosahau

Haya makaburi ya kwa jongo hayana wachawi zaidi ya usiku kujaa waganga wa kienyeji wakiwa na wateja wao mfano mganga wa diamond uwa ndio eneo lake la kuwatibia wasanii na mbuzi wapo wengi sana wamejaa pale makaburini wanazaliana mpaka leo hawana mmiliki kwani wenyeji wana waogopa kuwachukua ,wanadai wamesomewa albadili.
Mimi kipindi cha ujana nimekatiza sana hapo katikati ya makaburi tena muda mbaya saa 8 mpaka saa 9 nikitoka kwenye muziki kurudi nyumbani zaidi nilikua nakutana na waganga wakiwa na wadada au wamama.mji huu watu wanaishi kwa mambo ya ajabu sana.
Hiyo ninayokwambia mimi imetokea miaka ya 90. Alafu haya mambo hutokea pale ambapo mtu hukutarajia.

Mimi mwenyewe kama unavyosema, nilikuwa napita sana usiku yani ndio ilikuwa njia yangu ya kila siku. Sasa siku ile nahisi vibwengo walikuwa washachoka kunivumilia kupita pale, wakaamua kutaka kuniteka ndo nikatoka nduki.
 
dah!
Ile mbio umetimka najaribu kuimagine Hussein Bolt sijui kama angeuona au kukukamata aise 🐒

kweli vibwengo sio vitu vya mchezo mchezo.....

napendekeza ikiwezekana vibwengo vitumike kuibuka vipaji vya wakimbiaji wenye kasi na spidi zaidi 🤓
Huenda huwa wanafanya mashindano hayo wenyewe kwa wenyewe baada ya kugundua kuwa sisi hatuwapendi na tunawaogopa 😂😂
 
20231114_163033.jpg
 
Nyie waoga sana, hakunaga hayo mambo. Tatizo mnayatengeneza vichwani mwenu, mnakuja kusimulia uongo.
Siri ya mtungi ijuayo kata. Wewe hauwezi kubali maana sio ulieona. Usiombe ukutane na vibwengo ndugu yangu kama ni chooni utasahau hata kuvaa chumi utoke nduki uchi.
 
Umeitaja hiyo Loha umenikumbusha mbali sana. 1993 ( std 2) 1994( std 3) 1995( std 4)

Mambo ya Amrish Puri na Mithun Chakraboth.

Movie yangu pendwa ilikuwaga Tridev( Oye Oye) Dance Dance, Disco Dancer, Vishwatmar, Andha Kanoon


Nolstagia is real
mwanangu umenitajia hayo majina umenikumbusha utoto aisee movie ya kwanza kuona ilikua disco dancer.... wahindi waliteka hisia za muafrika kipindi kile ...andha kanoon hafu kila movie amrish poor ndo jambazi kuu😂😂 aloo
 
Sio story kaka, huu mziki nilikutana nao live. Usiombe ukumbane nao ndugu yangu [emoji23][emoji23]
Sasa wewe ulijuaje kama wanajamba? Tena kwanini hukumfuata mbuzi uone anaelekea wapi? Tena alikuwa akivuta sigara kwahiyo alikimbia nao mdomoni? Yule si analiaga wakati anakimbia haikumdondoka?[emoji3][emoji3][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Siri ya mtungi ijuayo kata. Wewe hauwezi kubali maana sio ulieona. Usiombe ukutane na vibwengo ndugu yangu kama ni chooni utasahau hata kuvaa chumi utoke nduki uchi.
Ukiona mtu anapinga ujue naye yumo hataki watu wajue kama kuna mambo kama hayo.
 
Back
Top Bottom