Hiki ndiyo kituko nlichowahi kukutana nacho makaburini usiku. Sitosahau

Hiki ndiyo kituko nlichowahi kukutana nacho makaburini usiku. Sitosahau

Niaje waungwana,

Hiki kisa, au tukio lilintokea miaka mingi kidogo. Enzi zile za kwenda kuangalia movie katika vibanda vya video. Sasa siku hiyo nilienda kuangalia video katika banda moja nililokuwa napenda kwenda kuangalia.

Banda hilo lilikuwa maeneo ya Manzese Midizini kwa mama fulan jina kapuni, na mimi home ni maeneo ya Magomeni mikumi jijini Dar es salaam.

Njia yangu kubwa kutoka home hadi Midizini, ilikuwa kagera kimamba, nakatiza daraja la mbao, napandisha pale Mburahati Mianzini, napasua Makaburi ya Mburahati kwa jongo hadi midizini. Na kurudi i was doing the same thing kwa kufuata njia ile ile niliyokuja nayo.

Ratiba yangu kwa siku ilikuwa ni shule kwanza, nlipotoka shule, nlielekea mazoezini (mpirani), baada ya kutoka mpirani ndo nikawa naenda sasa kujipoza vibandani kumuangalia Dharmendra, Amita Bachan, Rambo, Anord, Bruce Lee nk.

Ratiba yangu ya mwisho baada ya kutoka huko katika banda la video, ilikuwa ni kwenda katika maskani yetu fulan ambayo ni ya uncle wangu kujifunza mchezo wa karate. Uncle ndo alikuwa masta wetu. Hivyo nilijiamini sana kwamba hakuna kitu au mjinga yeyote anaeweza kunifanyia ushen.z.i mbele yangu. Karate na ngumi ni michezo ambayo humfanya mchezaji ajiamini sana, kwamba anaweza kupambana na mtu yoyote, mahali popote na kwa muda wowote.

Basi bwana siku hiyo nimemaliza kumuangalia Dharmendra mida ya usiku, nakumbuka ilikuwa movie fulan inaitwa LOHA. Tukatoka kila mtu akawa anaelekea kwao. Mimi nikawa natambaa mdogo mdogo kuelekea home.

Nilivyofika katika makaburi ya mburahati kwa jongo kama kawaida yangu, nikageuka nyuma kuangalia huku na huko, sikuona mtu ananifuata nikaendelea na safari yangu.

Sasa nimesogea sogea hadi katikati ya makaburi, kwa mbele nikaona kitu kama mbuzi mweupe, lakini kilichonishangaza na kunitia hofu ni kwamba yule mbuzi alikuwa kama vile amekaa kwenye kitu anavuta sigara, nikafikicha macho kama vile siamini ninachokiona.

Nikaendelea kusogea taratibu ili nihakikishe kuwa ninachokiona ni chenyewe au.

Kusogea nikasikia mbuzi anakohoa, ikabidi nigeuke ili nitoke nduki maana niliona pale hata karate zangu haziwezi kunisaidia.

Sasa wakati nageuka nikaona nyuma yangu kuna kundi la watu wamebeba jeneza wanakuja upande wangu halafu juu ya jeneza kuna mtu kakaa na yeye anavuta fegi, halafu kila jamaa wakipiga hatua, yeye anajamba.

Nikaona nyuma hakufai bora huku huku nilipotaka kupakimbia. Nikageuka na kuanza kutoka nduki kuelekea kwa mbuzi anaevuta sigara. Ghafla nikaona na mbuzi na yeye anatoka nduki na sigara yake.

Akili ikanijia nikaacha kukimbia ule upande anakimbilia mbuzi, nikaelelea upande wangu.

Breki ya kwanza ikawa Magomeni Mapipa, yani sikumbuki hata mikumi home nilipapita saa ngapi, au kule Mapipa nilifika fikaje fikaje.

Nikarudi nyumbani salama. Toka siku hiyo sikurudi tena kwenda video usiku, na ukawa mwisho wa kuendekeza movie.

Ni nani mwngine ambae ashawahi kukumbana na songombingo la aina hiyo?

Aisee it was scary
Hii Chai peleka Facebook.
 
Mimi bwana Kuna siku nimepita makaburini mchana na jua linawaka,ghafla nikatokewa na watoto mapacha wanachekaaaaaa,wamekaaa juu ya kaburi ati![emoji23][emoji23]
Hao walikuwa vibwengo tu my brother. Dawa yao ilikuwa bakora za kichwa wote wangetoka nduki pamoja 😂😂😂
 
Umeitaja hiyo Loha umenikumbusha mbali sana. 1993 ( std 2) 1994( std 3) 1995( std 4)

Mambo ya Amrish Puri na Mithun Chakraboth.

Movie yangu pendwa ilikuwaga Tridev( Oye Oye) Dance Dance, Disco Dancer, Vishwatmar, Andha Kanoon


Nolstagia is real
Loha ameigiza Dharmendra na Amrish Puri sio Mithun Chakrabot
 
Hata wao zipo ndo maana Hadi movies wanaziectia.
Sisi huwa tunaishia kwenye kusimulia tu
Asante brother kwa kumuelewesha mtu asieijua dunia. Kujua kusoma na kuandika kuna mfanya ajione muerevu.

Hapo ndo nakumbuka ule msemo wa mjinga akierevuka, muerevu hukaa mashakani 😂😂😂
 
Haya makaburi ya kwa jongo hayana wachawi zaidi ya usiku kujaa waganga wa kienyeji wakiwa na wateja wao mfano mganga wa diamond uwa ndio eneo lake la kuwatibia wasanii na mbuzi wapo wengi sana wamejaa pale makaburini wanazaliana mpaka leo hawana mmiliki kwani wenyeji wana waogopa kuwachukua ,wanadai wamesomewa albadili.
Mimi kipindi cha ujana nimekatiza sana hapo katikati ya makaburi tena muda mbaya saa 8 mpaka saa 9 nikitoka kwenye muziki kurudi nyumbani zaidi nilikua nakutana na waganga wakiwa na wadada au wamama.mji huu watu wanaishi kwa mambo ya ajabu sana.
 
Nilikuwa timamu boss, ila vibwengo waiamua kunionesha kuwa na wao wapo, baada ya kuchoka kunivumilia kila siku nilipokuwa napita pale.
dah!
Ile mbio umetimka najaribu kuimagine Hussein Bolt sijui kama angeuona au kukukamata aise 🐒

kweli vibwengo sio vitu vya mchezo mchezo.....

napendekeza ikiwezekana vibwengo vitumike kuibuka vipaji vya wakimbiaji wenye kasi na spidi zaidi 🤓
 
Hata walioenda kwa mkaburu miaka hio waliinjoi sana.
Kwakweli maisha ya kuinjoi yalikuwa miaka ya 90 kurudi nyuma
Huu ulioandika hapa ni ukweli mtupu, sema watoto wa miaka ya 2000 kuja juu hawawezi kukuelewa.
 
Anaitwa nani huyu staa?(huyu alienyoa kama A-Team)
Kazi yake kubwa ilikuwa ku act kama villain.
Huyo anaitwa mzee Ashanti jina lake halisi nimelisahau.

Huyu alikuwa aki act adui alaf sterling Dharmendra lazima banda la video lijae watu siku hiyo.
 
ikabidi nigeuke ili nitoke nduki maana niliona pale hata karate zangu haziwezi[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
Karate mbele ya mbuzi anavuta sigara huku anabanja, si bora nitoke nduki 😂😂
 
Back
Top Bottom