Hiki ndiyo kituko nlichowahi kukutana nacho makaburini usiku. Sitosahau

Hiki ndiyo kituko nlichowahi kukutana nacho makaburini usiku. Sitosahau

Niaje waungwana,

Hiki kisa, au tukio lilintokea miaka mingi kidogo. Enzi zile za kwenda kuangalia movie katika vibanda vya video. Sasa siku hiyo nilienda kuangalia video katika banda moja nililokuwa napenda kwenda kuangalia.

Banda hilo lilikuwa maeneo ya Manzese Midizini kwa mama fulan jina kapuni, na mimi home ni maeneo ya Magomeni mikumi jijini Dar es salaam.

Njia yangu kubwa kutoka home hadi Midizini, ilikuwa kagera kimamba, nakatiza daraja la mbao, napandisha pale Mburahati Mianzini, napasua Makaburi ya Mburahati kwa jongo hadi midizini. Na kurudi i was doing the same thing kwa kufuata njia ile ile niliyokuja nayo.

Ratiba yangu kwa siku ilikuwa ni shule kwanza, nlipotoka shule, nlielekea mazoezini (mpirani), baada ya kutoka mpirani ndo nikawa naenda sasa kujipoza vibandani kumuangalia Dharmendra, Amita Bachan, Rambo, Anord, Bruce Lee nk.

Ratiba yangu ya mwisho baada ya kutoka huko katika banda la video, ilikuwa ni kwenda katika maskani yetu fulan ambayo ni ya uncle wangu kujifunza mchezo wa karate. Uncle ndo alikuwa masta wetu. Hivyo nilijiamini sana kwamba hakuna kitu au mjinga yeyote anaeweza kunifanyia ushen.z.i mbele yangu. Karate na ngumi ni michezo ambayo humfanya mchezaji ajiamini sana, kwamba anaweza kupambana na mtu yoyote, mahali popote na kwa muda wowote.

Basi bwana siku hiyo nimemaliza kumuangalia Dharmendra mida ya usiku, nakumbuka ilikuwa movie fulan inaitwa LOHA. Tukatoka kila mtu akawa anaelekea kwao. Mimi nikawa natambaa mdogo mdogo kuelekea home.

Nilivyofika katika makaburi ya mburahati kwa jongo kama kawaida yangu, nikageuka nyuma kuangalia huku na huko, sikuona mtu ananifuata nikaendelea na safari yangu.

Sasa nimesogea sogea hadi katikati ya makaburi, kwa mbele nikaona kitu kama mbuzi mweupe, lakini kilichonishangaza na kunitia hofu ni kwamba yule mbuzi alikuwa kama vile amekaa kwenye kitu anavuta sigara, nikafikicha macho kama vile siamini ninachokiona.

Nikaendelea kusogea taratibu ili nihakikishe kuwa ninachokiona ni chenyewe au.

Kusogea nikasikia mbuzi anakohoa, ikabidi nigeuke ili nitoke nduki maana niliona pale hata karate zangu haziwezi kunisaidia.

Sasa wakati nageuka nikaona nyuma yangu kuna kundi la watu wamebeba jeneza wanakuja upande wangu halafu juu ya jeneza kuna mtu kakaa na yeye anavuta fegi, halafu kila jamaa wakipiga hatua, yeye anajamba.

Nikaona nyuma hakufai bora huku huku nilipotaka kupakimbia. Nikageuka na kuanza kutoka nduki kuelekea kwa mbuzi anaevuta sigara. Ghafla nikaona na mbuzi na yeye anatoka nduki na sigara yake.

Akili ikanijia nikaacha kukimbia ule upande anakimbilia mbuzi, nikaelelea upande wangu.

Breki ya kwanza ikawa Magomeni Mapipa, yani sikumbuki hata mikumi home nilipapita saa ngapi, au kule Mapipa nilifika fikaje fikaje.

Nikarudi nyumbani salama. Toka siku hiyo sikurudi tena kwenda video usiku, na ukawa mwisho wa kuendekeza movie.

Ni nani mwngine ambae ashawahi kukumbana na songombingo la aina hiyo?

Aisee it was scary
Alikua harmonize huyo. Si umesema alikua anavuta sigara huku akakohoa
 
Nilikuwa nandesha BAISKERI Saa 5 usiku nipo kasi bonde la mkwajuni natoka magomeni naitafuta MWANANYAMALA
Mbele wakapita watu wamebeba jeneza
Nikakumbuka story za VIJIWENI
nikasema hapa sifungi brake nitakufa Kwa ajari mbaya nikapita katikati ya mazishi
sielewi ilikuwaje ila kuja kushituka nipo VIJANA SOCIAL HALL
MANGO GARDEN walikuwa TWANGAPEPETA nikaenda kucheza muziki
Una uhakika hao waliokuwa mango garden walikuwa ni twanga pepeta kweli


Isiwe na hao hao jamaa walijigeuza kuna Ali Choki πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Yaan mbuzi na sigara yake akaona isiwe tabu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Kumbe hata mzuka sometimes unakimbia mizuka mienzake nlishangaa sana πŸ˜‚πŸ˜‚
 

i say​

i will never ever forget it​

Hii "i say" haikua na ulazima hapo..statement ya pil hapo ilikua inajitosheleza kabisaa
 
ikabidi nigeuke ili nitoke nduki maana niliona pale hata karate zangu haziwezi[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Back
Top Bottom