Hiki ni kitu cha ajabu sana nimekiona kwa macho yangu

Hizi imani za kijinga huwa sizifagilii. kuna kipindi nilikuwa na njaa vibaya mno halafu jua kali. nikapita mahali fulani, kuna mnazi chini yake nikaona embe jipya kabisa tena limeiva. nikawaza tu kuwa hili kuna mtu kaungusha kisha nikafanya yangu na mpaka leo mambo safi
 
Yesu yupi wakukanyaga mafuta ya upako? huko ndiyo mtamtapeli kabisa ninyi wachungaji wasanii.

Yesu Kristo wa Nazareti. achana kabisa na biashara ya kukanyaga mafuta au matope au maji au chochote. Amini na kubatizwa, jifunze neno ulishike usikubali kuburuzwa. Soma uelewe na Mungu atakusimamia utajua lipasalo.
 
Sawa mkuu!!asante kwa ushauri
Kumuita Mchungaji aje aombee nyumba yako bila wewe mwenyewe kukubali kutubu na kubadilika ni kupoteza wakati.
1.Tubu dhambi zako
2.Mpokee Yesu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako
3.Acha dhambi na matendi maovu
4.Tafuta Mchungaji au watu sahihi wa imani muombe pamoja, sio wakuombee. Lazima na wewe uwe na imani thabiti
5.Endelea kufurahia maisha pasipo kutishwa na nguvu za giza, Yesu ni mkuu kuliko nguvu za giza na wachawi wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fanya dua, kifupi muombe Mungu kwa maana ya kuswali na kufunga..kama umepanga unaweza taratibu ukahamia mitaa ya watu wastaarabu..
 
Chumvi ya mawe imejaaliwa nguvu kubwa ya anti uchawi, hivyo chukua ushauri ule wa jamaa kuhusu kumwagia chumvi ya mawe.

Kisha Tambua uchawi ni Imani yako uliyonayo. Jikurubishe katka maombi pia jitahidi sana kutoa sadaka. Ikitokea umeota unakula Basi uliamka chukua majani ya mbaazi utafune.

HAKUNA kids kabla ya siku uliyopangiwa, labda wakijtahidi wakuchukue msukule.

UKIONA MCHAWAI ANAKUTISHA UJUE KAKUSHINDWA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…