Hiki ni kiwango kilichopitiliza cha Ukatili kwa watoto

Kabisa. Hawa ndiyo wakiwa viongozi wanaamuru mtu ashushwe kwenye bus na kuuawa.
Ndo ivo wao si walilelewa hivyo.

Binafsi sipendelei malezi ya kumdunda hovyo mtoto, kuna time unampiga hata hajui ni kwanini unampiga.
Nae ana mawazo yake, ana maswali kibao angependa kukuuliza ila anaogopa kipigo.
 
Tz inajamii ya watu wanafiki,kazi kulaumu serikali na kusubiri kila kitu ifanyiwe na serikali.

One of the dumbest community in this world!!!
Mkuu unatoka nje ya mada, hapo unafiki uko wapi??
 
Mkuu usishuhudie uongo, hao unaowaita wazungu hayo malezi yao sio kua wameanza 2000's, ni muda mrefu wako hivyo.

Na bado wametupiga gape, gunduzi zinatoka kwao, tunapata misaada toks kwao pamoja na hayo unayoita malezi mabovu.

Wao wameshajua kua kupiga na kufoka hovyo sio lazima kwa mtoto.
Sasa hayo malezi ya vipigo si yapo toka tunapata uhuru, yametufikisha wapi??.
Kama kawaida yetu Afrika kutumia nguvu bila akili, ndo hapo tumepigwa gape.
 
Umeongea kwa unafiki mkubwa,sasa ulitaka aache makalio inje?
 
Atembelee mashuleni hasa za bweni uone jinsi wanafunzi wananyooshwa fimbo za mapajani dazeni dazeni kama kweli tunataka kupunguza ukatili.
Kwa nini lkn? Labda mimi sina wtt manunda lkn kwa ninavoishi nao sijaona sababu ya kuwapiga.
Kuna watu wana ila tu na mikono yao ni kama inawashawasha. Mie Nishaona wazee wengine wanapiga hadi vitoto vya miaka miwili au mitatu. Huwa napata uchungu sema unaogopa kusema kwa mtt asie wako usije ukageuziwa kibao ukaambulia matusi toka kwa mzazi
Mimi always nipo against na violence hasa kwa wtt.
 
Kwahyo mtoto afanye ujinga na bado awe confident cyo!
Ni mtazamo wako mkuu .. Mtoto akikosea kuna namna nzuri zaidi ya kumcorrect kwa kumuonyesha uchaguzi sahihi na madhara ya anachofanya ..

Ukitaka kunielewa muache mtoto mdg nakitu unachoogopa wewe yeye hawez ogopa sababu hana fear ndani yake wewe ndio humfundisha aogope yaani unamcondition na kuinstall pattern zako
 
Wamefanya kosa gani ambalo HALIZUNGUMZIKI MEZANI?
 
Kwaiyo unataka kutulinganisha Waafrika na Wazungu kwenye suala la Maadili??

Malezi yao ndio yamewafikisha hapo walipo na kwa Macho ya Sisi tulio na akili timamu tunawaona Wapo nyuma katika suala la maadili na Malezi.

Mtoto wa Kizungu wa Miaka miaka 9-15 kumtambulisha Boyfriend wake au girlfriend wake Kwa wazazi wake ni jambo la kawaida kwao ila sio kawaida kwetu.

Familia kwenda beach na Vichupi Wote Baba,, mama,, watoto wote vichupi kwa wazungu sio Shida ila Sisi kwetu hilo jambo sio normal.

Na Kupitia hayo na mengineyo mengi mimi napata ujasiri kusema kuwa Maadili yetu wa Afrika yameyatangulia yale ya wazungu.

Huwezi kuwa na akili timamu alafu ukasifu kuwa vile wanavyoishi wazungu ni NAMNA BORA YA MALEZI NA MAADILI LABDA KAMA TAYARI UMESHAKUWA MZUNGU NA WEWE.

Labda ujue kuwa Wazungu nao sio kwamba Wanaridhika na makuzi ya Watoto wao ila NOW WAZAZI WANAWAOGOPA WATOTO KUTOKANA NA SHERIA ZISIZO NA KIWANGO WALA MIPAKA.

NA NDIO MAANA UINGEREZA IDADI YA VITUO VYA KUBADILI TABIA VINAONGEZEKA PIA MATUKIO YA AJABU AJABU WANAYOFANYA WATOTO KAMA VILE KUTUMIA SILAHA KUSHAMBULIA WENZAO,, KUWADHALAU WALIMU YANAONGEZEKA SIMPLY BECAUSE WATOTO HAWANA ADABU TENA.

MTOTO NI MTOTO TUU ANA UTOTO,,, AKILI YAKE SIO KAMA YA MTU MZIMA KUNA SEHEMU YA KUZUNGUMZA NAE ALAFU KUNA SEHEMU YA KUMUADHIBU KWA ADHABU ITAKAYOACHA ALAMA YA MAUMIVU.

SASA UKISEMA ETI UUMPE MACHAGUO MTOTO JUA TUU ATAISHIA KUBAYA SABABU HATA SISI TULIKUWA NA VIJITABIA KAMA SIO WAZAZI WETU KUTUMIA NJIA WALIZOTUMIA,,, LEO HII TUSINGEKUWA TUNASIMAMA MBELE ZA WATU NA TUKASIKILIZWA.
 
Hata biblia imeandika "Mtoto usimnyime mapigo"
Watoto wanapaswa kuhadhibiwa wanapokosea cha muhimu adhabu isipitilize ikageuka ukatili kwa Mtoto
Binafsi sio mwislamu ila suala la adhabu kwa Mtoto akizingua naliunga mkono
 
Unajifananisha na wazungu kimaadili ilhali mila na desturi zenu hazifanani.

Umeandika maelezo mengi kuwakandia wazungu, vituo vya kubadili tabia kutokuwepo nchini kwako haimaanishi ndio mna tabia njema, ndio maana nakwambia wale wako mbele yenu.

Hospitali, shule na vifaa vyake vinawashinda kupatikana nchi nzima ndio mtaweza kujenga vituo vya kurekebisha tabia??
Hapa nchini kuna nyumba za kulea wazee wasiojiweza?? Vipi wazee wa namna hiyo hawapo??

Kwahiyo kutokua na hivyo vituo haimaanishi ndo mna tabia njema sana ila ni uwezo hamna.
 
Unajifananisha na wazungu kimaadili ilhali mila na desturi zenu hazifanani.
Hizo mila na tamaduni ndio Zinazofanya Sisi tuwapige Gap Wazungu katika suala la Maadili. Mila na Tamaduni zetu zipo imara kulinda Maadili. Na Utofauti unaonekana kadri tunavyozichukua hizi tamaduni za kibeberu maadili na Malezi yanapolomoka na Wala hayajawa Bora kuliko Zamani.
Vituo sisi vya kazi gani Wakati kila Nyumba ni kituo tosha.

Vituo vinaanza kujengwa Now huku bongo baada ya Muhimili wa familia kubomolewa na sasa Watoto wanajilea wenyewe.
Hapa nchini kuna nyumba za kulea wazee wasiojiweza?? Vipi wazee wa namna hiyo hawapo??
Unazungumza usichokujua kafanye utafiti wako tena. Hizo nyumba au vituo vipo chini ya mamlaka za Ustawi wa jamii. At least kila mkoa hivo vituo vipo.
Kwahiyo kutokua na hivyo vituo haimaanishi ndo mna tabia njema sana ila ni uwezo hamna.
Naona unajitoa kwenye Uafrika. Ndio maana napata tabu kukuelewesha.
 
Tukubali kutokubaliana ndgu, labda maana ya maadili ni tofauti kwa kila mmoja.
Nijuavyo malezi mazuri huleta matokeo mazuri, tabia za ubinafsi, rushwa, ufisadi, wizi, ujambazi, matumizi ya dawa za kulevya, ulevi kupindukia, matukio ya kikatili yote hayo ni matokeo ya malezi mabovu.

Sasa sijui hayo maadili mema ya watu wako yanapositive impact gani kwa jamii.
Au haupo Tz mkuu??
 
Kwa hiyo wanawake na wanaume malaya walikuwa hawachapwi viboko wakiwa wadogo??
 
Ni wendawazimu kumchapa mwanafunzi kw sababu amekosea maswali au hajafikisha marks za kiwango fulani.
 
Hawa watoto kwa kuanzia hata hawakupaswa kuwa hapo, walitakiwa kuwa wanacheza au wanajifunza vitu vya uhalisia vya maisha badala ya dini za kale na lugha ambayo hawaielewi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ