Hiki ni kiwango kilichopitiliza cha Ukatili kwa watoto

Hiki ni kiwango kilichopitiliza cha Ukatili kwa watoto

Mwanangu humchapi hivyo na madrassa ndo basi tena,toka nizaliwe sijawahi piga kiumbe Cha kike Leo mwanangu unampigaje hivyo.
Zamani mzee wetu alikua anatupiga sana, ila mwisho wa siku aliacha alipoona tunaelewa zaidi kwa maneno kuliko viboko na adhabu za kijeshi.
Viboko vinakupa usugu, itafika time hutaviogopa.
 
Tulichambue Jambo Hili Bila kudhihirisha chuki au Mapenzi Yetu katika Dini Zetu.

Ukatili Ni nini?? Unaweza Kutafsiri ukatili kuwa ni kila Adhabu ya Viboko anayopewa Mtoto??
Au ukatili unapimwa kwa reaction ya mfanyiwaji bila kuangalia aina ya adhabu na Ukubwa wake??

Basi sisi kama wazazi wote ni wakatili Sisi Tunawaadhibu watoto wetu Kwa bakora zaidi ya Hivyo.

Huyo mwalimu Ametoa Adhabu ya Bakora za Mikononi ##Tano hadi Sita kwa Kila mwanafunzi (Hatujui kosa ni Nini labda tungejua kosa gani wamefanya Hao watoto labda tungeiona hiyo adhabu kuwa ni Ya kawaida tuu.

Shule za Serikali na binafsi adhabu ya Viboko bado ipo tena wanafunzi wanapigwa kwelikweli.

Nakumbuka nikiwa Shule Mwalimu alikuwa anaweza kumuadhibu mwanafunzi hadi bakora 20 yes 20 na ni kawaida tuu kwa walimu wa shule za Serikali sisemi ni sawa lakini Ni namna ya njia ya Kuwanyoosha Vijana iliyochaguliwa na Wahusika.

Ikiwa ni Hivyo jee Suala ya Bakora 5 au sita tena za Mkononi sehemu Salama kabisa itafsiriwe ni Ukatili!!! Labda kama tunataka kuwalea Watoto wetu kizungu alafu baade waje watushitaki ukimkalipia au ukimfokea kama walivyo watoto wa kizungu nowdays.

Jee tunataka tufike huko???
 
Kusema ukweli utandawazi umeharibu maadili hivi hapo kina kipi cha ajabu? Kipindi tunasoma sisi mwalimu wetu alikuwa anakuvua kaptura unabaki na chupi ndo anakushushia mvua ya fimbo lakn hakuna kulalamika.
Lakin sasa hiv mnataka mtoto akikosea apetiwe petiwe acheni mambi yenu bwana nyie ndiyo mnasababisha maadili yanaporomoka
Mwalimu wenu wa madrasa ndo alikuwa anavua nguo anabaki na kaptura?
 
Labda hujapita maeneo mengi huko mitaani hasa mitaa inayofanana na hiyo video hapo juu, hizo fimbo hapo juu ni cha mtoto tena ni fimbo ambazo shule za msingi za serikali ndo huchapwa kama hivyo, watoto wa darasa la kwanza ama la pili hutandikwa sana zaidi ya hapo. Sasa huko uswahili huchaguliwi sehemu ya kupigwa yaani unapigwa mwili mzima kama vile mwizi. Hivyo basi nitoe neno Kwa huyo waziri atembelee Tanzania nzima huko uswahili na mashule ya msingi ya serikali aone mambo zaidi ya hayo.
 
Mbona hapo hamna ukatili mnataka kila mtu alee mtoto kama mnavyolea mitoto yenu inaishia kuwa mishoga na mi malaya inayozalia nyumbani.

📌Samaki anakunjwa akiwa mbichi.!
 
Atembelee mashuleni hasa za bweni uone jinsi wanafunzi wananyooshwa fimbo za mapajani dazeni dazeni kama kweli tunataka kupunguza ukatili.
Aliyepost video na aliyechukua video yawezekana wamelelewa kimayai mayai sisi wengine tuna makovu ya njiti na kila kovu lina stori ya kusisimua.

Leo hii mnataka mtoto asipigwe fimbo sipati picha enzi zangu nisingepigwa mboko leo ningekuwa mtukutu kuliko.Acheni watoto wa kiafrika walelewe kiafrika.

Mazingira yetu hayatushawishi kulea watoto kimagaribi magaribi kwakua mifumo yetu bado haijatengemaa.Wanaofosi kulea kizunguzungu wanaishia kuharibikiwa watoto
 
Mwanangu humchapi hivyo na madrassa ndo basi tena,toka nizaliwe sijawahi piga kiumbe Cha kike Leo mwanangu unampigaje hivyo.
Huna akili na mwanao huyo atakuja kuwa MALAYA aliyeshindikana.

Sio kwamba wanaopiga watoto hawawapendi ila wanawajengea watoto adabu,heshima na utii wa yale wanayoelezwa na wakubwa wao.

Hata katika jamii kama hufati kanuni na taratibu utaadhibiwa na jamuhuri kwa kupelekwa mahakani na kufungwa.

📌📌📌Kwahiyo adhabu zipo tu usipomuadhibu wewe ULIMWENGU UTAMUADHIBU!!!
 
Ninyi ndio mmeifanya hii nchi kua masikini mpaka kesho.

Yaani unachapwa uchi na unakaa kimya, mlikua mazombi wa namna gani aisee.
Wewe acha kujifanya Gen Z wakati ni millenia au baby boomer😀😀😀

Enzi zetu unachapwa mbaya mbovu na hakuna mahali utashtaki.

Huu mmomonyoko wa maadili umeletwa na vilaza wanaofake maisha ya ulaya wakati mifumo yenu ni ya kimbwambwa.Acheni kutetea ujinga hauwafanyi kuonekana mnaakili ila mapunguani.
 
Huna akili na mwanao huyo atakuja kuwa MALAYA aliyeshindikana.

Sio kwamba wanaopiga watoto hawawapendi ila wanawajengea watoto adabu,heshima na utii wa yale wanayoelezwa na wakubwa wao.

Hata katika jamii kama hufati kanuni na taratibu utaadhibiwa na jamuhuri kwa kupelekwa mahakani na kufungwa.

📌📌📌Kwahiyo adhabu zipo tu usipomuadhibu wewe ULIMWENGU UTAMUADHIBU!!!
Kama wenye akili wote watatumia fimbo basi jamii hazina watu wenye akili.Kwa hiyo hapa ustaadhi anapambana na umalaya bahati njema binti yangu kaolewa mwenye heshima na taadhima
 
Wewe acha kujifanya Gen Z wakati ni millenia au baby boomer😀😀😀

Enzi zetu unachapwa mbaya mbovu na hakuna mahali utashtaki.

Huu mmomonyoko wa maadili umeletwa na vilaza wanaofake maisha ya ulaya wakati mifumo yenu ni ya kimbwambwa.Acheni kutetea ujinga hauwafanyi kuonekana mnaakili ila mapunguani.
Kwani ulichapwa peke YAKO mkuu,hata sisi kizazi hicho tulikiishi.Halafu punguza jazba.
 
Kama wenye akili wote watatumia fimbo basi jamii hazina watu wenye akili.Kwa hiyo hapa ustaadhi anapambana na umalaya bahati njema binti yangu kaolewa mwenye heshima na taadhima
kuolewa sio mafanikio je huko kwenye ndoa mambo yanaenda???

Wajukuu zako watakuzwa kimaadili au kibroilabroila kesho wakifanikiwa kumaliza elimu zao kisha wakapangiwa kazi huko Nanjilinji wakashindwa kucope na mazingira kwasababu ya malezi mabovu.
 
Kwani ulichapwa peke YAKO mkuu,hata sisi kizazi hicho tulikiishi.Halafu punguza jazba.
kama ulikiishi basi unajua msaada wa njiti katika kukushape uwe ulivyo leo.

Acha kutype vitu visivyo na mantiki wakati unaelewa maisha ni nini.

📌Sio jazba tunakemea uzwazwa.Uzwazwa wa kujifanya wewe ndo unajua sana kupenda kuliko wengine.Hayo maisha ya kujionesha hayana afya.
 
Hapana huyu mwalimu amepitiliza adhabu,Mie mwenyewe mtoto wangu niliyemzaa wa umri huo siwezi kumuadhibu kiasi hicho.

Tusilee huu ujinga mtoto mdogo tena wa kike anapigwa kama mwizi?
Hiyo mitoto yenu mnayoiabudu kuna siku ndio watakuwa viongozi na wananchi wa hii nchi 😀😀😀.Kwa trend inavyoonyesha hiyo mitoto iliyo na low IQ na EQ haitaweza kusurvive!!!
 
Sidhani kama dini inataka hivi.

Oneni wenyewe. Aione Dkt. Gwajima D

Hujambo? Ahsante Sana kuniTag. Tayari jambo liko Polisi kwa hatua zao za uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na maafisa ustawi wa jamii. Watu tuwe na subira kwani, nyuma ya jambo moja aina kama hii, huwa kunakuwa na mengi mengine hivyo, tupewe nafasi tutimize wajibu wetu mliotupatia kuhusu sheria ya mtoto na 21 ya Mwaka 2009 na marekebisho yake yote.

Ahsanteni Sana
 
Back
Top Bottom