Wewe baby boomer acha kujifanya Gen Z huyo mtoto wa miaka 9 mpaka 11 kumuelewesha kwa maneno ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.Bila kujali kosa la hao watoto hiyo adhabu ni kubwa kwao.
Nawashangaa sana ninyi mnaofananisha dunia ya sasa na hiyo ya miaka ya tisini.
Mfano kosa la uchelewaji, hilo kosa kwa miaka yetu ya giza utakumbushwa kwa viboko, ila siku hizi kuna means nyingi unaweza kuelekezwa zikakufanya ukawahi kuamka/kuwahi jambo fulani.
Hao madogo wamechelewa, mtoto kama huyo kuchelewa madrasa mara nyingi huwa sio kosa lake, kuna mwingine hapo kabeba kapu kabisa ikiwa na maana aidha akitoka hapo au alikotoka huko kahemea ndio kaenda madrasa.
Hivi kweli unashindwa kuicontrol akili ya mtoto hadi umpige, mbona akili yake unaisoma chap tu na kupredict his/her next move.
Mkiwa mnaiga maisha igeni vile vyenye manufaa.Sio kila jambo linalowezekana ULAYA na huku mavumbini lawezekana.
Wenzetu wameandaa mifumo waalimu wamesoma ualimu tena kuna nchi nyingine waalimu wa awali(chekechea) wanamasters sasa huwezi kumfananisha huyo mbobevu na mwalimu ambaye kwanza ameenda kusomea ualimu kama last option.
Pili hana intrest wala hajui makuzi ya watoto yanataka nini na approach zake.Kiuhalisia mnachokitetea kitawezekana kama mtawekeza kwa hao walimu.