Hiki ni kiwango kilichopitiliza cha Ukatili kwa watoto

Hiki ni kiwango kilichopitiliza cha Ukatili kwa watoto

Kuna shule ya ipo karibu yangu hapa madogo wanakula sana mboko, sasa imagine dogo kala mboko skuli, kafika home msosi hakuna, anawahi madrasa huko nako anakutana na bakora 5 za moto.

Huyu akija kua kibaka kukutia bisu hataona kazi dadeki.
Kulingana na umri wa mtoto, na saikolojia Tete ya mtoto, lazima achukie kuja duniani na akiwa kwa mfano na watoto wengine natoa mfano ukatili wa baadhi ya wasaidizi wa ndani dhidi ya watoto tunaowaachia, nyuma ya historia ya maisha yao, kunakuwa na maumivu mengi Sana ... Hawajui kingine kuhusu kulea zaidi ya akili inamwambia piga...... Halafu tunakuja tena kulalamika na kusifiana eti sisi tulipigwa. Tunasahau hiyo spirit inabebwa na kusambaza Hadi kwa msaidizi wako, mke wako na mume wako. Halafu tunashangaa tena. Tunachopanda, ndiyo tutavuna.

Tarehe 24 x space tuna mjadala kuhusu sayansi ya malezi na makuzi na madhara ya hizi hatua za kupiga piga. Karibuni
 
kama ulikiishi basi unajua msaada wa njiti katika kukushape uwe ulivyo leo.

Acha kutype vitu visivyo na mantiki wakati unaelewa maisha ni nini.

📌Sio jazba tunakemea uzwazwa.Uzwazwa wa kujifanya wewe ndo unajua sana kupenda kuliko wengine.Hayo maisha ya kujionesha hayana afya.
Kuna watu ni makatili kuliko huyo lakini nikwambie binti yangu nilimwachishaga huko.Hao wamezidi
 
kuolewa sio mafanikio je huko kwenye ndoa mambo yanaenda???

Wajukuu zako watakuzwa kimaadili au kibroilabroila kesho wakifanikiwa kumaliza elimu zao kisha wakapangiwa kazi huko Nanjilinji wakashindwa kucope na mazingira kwasababu ya malezi mabovu.
Usipime malezi mazuri kwa mzani wa fimbo.Wengine tumeishi bila hata kutishwa na kupigwa na tunaheshimu na kuheshimiwa na watu mbalimbali.
 
Tulichambue Jambo Hili Bila kudhihirisha chuki au Mapenzi Yetu katika Dini Zetu.

Ukatili Ni nini?? Unaweza Kutafsiri ukatili kuwa ni kila Adhabu ya Viboko anayopewa Mtoto??
Au ukatili unapimwa kwa reaction ya mfanyiwaji bila kuangalia aina ya adhabu na Ukubwa wake??

Basi sisi kama wazazi wote ni wakatili Sisi Tunawaadhibu watoto wetu Kwa bakora zaidi ya Hivyo.

Huyo mwalimu Ametoa Adhabu ya Bakora za Mikononi ##Tano hadi Sita kwa Kila mwanafunzi (Hatujui kosa ni Nini labda tungejua kosa gani wamefanya Hao watoto labda tungeiona hiyo adhabu kuwa ni Ya kawaida tuu.

Shule za Serikali na binafsi adhabu ya Viboko bado ipo tena wanafunzi wanapigwa kwelikweli.

Nakumbuka nikiwa Shule Mwalimu alikuwa anaweza kumuadhibu mwanafunzi hadi bakora 20 yes 20 na ni kawaida tuu kwa walimu wa shule za Serikali sisemi ni sawa lakini Ni namna ya njia ya Kuwanyoosha Vijana iliyochaguliwa na Wahusika.

Ikiwa ni Hivyo jee Suala ya Bakora 5 au sita tena za Mkononi sehemu Salama kabisa itafsiriwe ni Ukatili!!! Labda kama tunataka kuwalea Watoto wetu kizungu alafu baade waje watushitaki ukimkalipia au ukimfokea kama walivyo watoto wa kizungu nowdays.

Jee tunataka tufike huko???
Uko sahihi mimi nakumbuka shule ya msingi nilipata hesabu 90,ila mwalimu wa hesabu aliniadhibu tena sawa na waliopata F kwasababu mimi nilikosa maswali marahisi nikapata magumu😀😀😀.Kwa kipindi kirefu nilimchukia sana yule mwalimu mpaka nilipokuja kuelewa alimaanisha nini kwa wakati ule.

Imagine kila alipokuwa akisahihisa paper za hesabu mimi alikuwa hakosi kunichapa kwasababu ya kukosa hesabu ndogondogo na kufaulu zile complicated.Ila ndo maisha leo naelewa kuwa alikuwa ananikumbusha kuzidisha umakini na kutochukulia mambo kwa wepesi hata kama unayamudu.
 
Usipime malezi mazuri kwa mzani wa fimbo.Wengine tumeishi bila hata kutishwa na kupigwa na tunaheshimu na kuheshimiwa na watu mbalimbali.
kwa mazingira yetu ya kiafrika yaliyojaa vurugu.Fimbo na ukali kidogo ni lazima kwa hawa watoto zetu lazivyo siku za mbeleni tutaanza kushikana uchawi.

📌📌Watoto zetu wanakulia katika mazingira ambayo yapo soo vunarable kiasi kwamba ukilegeza kidogo unampoteza huyo mtoto.
 
Kusema ukweli utandawazi umeharibu maadili hivi hapo kina kipi cha ajabu? Kipindi tunasoma sisi mwalimu wetu alikuwa anakuvua kaptura unabaki na chupi ndo anakushushia mvua ya fimbo lakn hakuna kulalamika.
Lakin sasa hiv mnataka mtoto akikosea apetiwe petiwe acheni mambi yenu bwana nyie ndiyo mnasababisha maadili yanaporomoka
Alivyokuvua kaptula alikulawiti?acha kutetea upumbavu
 
Kusema ukweli utandawazi umeharibu maadili hivi hapo kina kipi cha ajabu? Kipindi tunasoma sisi mwalimu wetu alikuwa anakuvua kaptura unabaki na chupi ndo anakushushia mvua ya fimbo lakn hakuna kulalamika.
Lakin sasa hiv mnataka mtoto akikosea apetiwe petiwe acheni mambi yenu bwana nyie ndiyo mnasababisha maadili yanaporomoka
THAT WAS UKATILI ULIOPINDUKIA,
 
Mbona sijaona ukatili wowote hapo? Alie toa post hii lazima atakuwa mzungu tena wa kike au diaspora.

Ustaadh yupo sahihi kabisa anawafundisha watoto discipline.

Sema alicho kosea tu ni kwenye hesabu wengine alikuwa anawapiga fimbo nane wengine fimbo nne, au zingine alikuwa hazihesabu anazifuta nini?
 
kwa mazingira yetu ya kiafrika yaliyojaa vurugu.Fimbo na ukali kidogo ni lazima kwa hawa watoto zetu lazivyo siku za mbeleni tutaanza kushikana uchawi.

📌📌Watoto zetu wanakulia katika mazingira ambayo yapo soo vunarable kiasi kwamba ukilegeza kidogo unampoteza huyo mtoto.
NOT THAT WAY SI AJABU HUYO KACHEELEWA NDIYO UNAWAPIGA WATOTO HIVYO
 
Mbona sijaona ukatili wowote hapo? Alie toa post hii lazima atakuwa mzungu tena wa kike au diaspora.

Ustaadh yupo sahihi kabisa anawfundisha watoto discipline.

Sema alicho kosea tu ni kwenye hesabu wengine alikuwa anawapiga fimbo nane wengine fimbo nne, au zingine alikuwa hazihesabu anazifuta?
HAKUNA NJIA NYINGINE?
 
Hujambo? Ahsante Sana kuniTag. Tayari jambo liko Polisi kwa hatua zao za uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na maafisa ustawi wa jamii. Watu tuwe na subira kwani, nyuma ya jambo moja aina kama hii, huwa kunakuwa na mengi mengine hivyo, tupewe nafasi tutimize wajibu wetu mliotupatia kuhusu sheria ya mtoto na 21 ya Mwaka 2009 na marekebisho yake yote.

Ahsanteni Sana
ASANTE MAMA YETU. LIMENIUMA SANA. UMRI ULE KUNA NAMNA YA KUWAADHIBU SIYO KWA MIKWAJU YA NGUVU MA MISURI VILE!
 
NOT THAT WAY SI AJABU HUYO KACHEELEWA NDIYO UNAWAPIGA WATOTO HIVYO
Sijamtetea mwalimu ila naongea kwa experience.

Kama umesomea hapa hapa Tanzania basi unajua mila na desturi za kitanzania( UVIVU NA UZEMBE).

Enzi zetu tupo shule mtu anajua saa moja kamili ndio muda wa kengele ya mstarini ila yeye anaamka saa kumi na mbili na dakika 55😀😀😀 akili za kiuanafunzi bila mboko na mwalimu kuliamsha huko mabwenini watu hawaendi paredi.

Kila siku mwalimu mkuu anaongea ila watu hawafati baada ya mboko na adhabu za nje na kukosa vipindi watu wakaanza kukaa kwenye mstari.Leo hii baadhi ya wale madoja ndio hawa wanatetea mtoto asiadhibiwe😄😄😄
 
Tulichambue Jambo Hili Bila kudhihirisha chuki au Mapenzi Yetu katika Dini Zetu.

Ukatili Ni nini?? Unaweza Kutafsiri ukatili kuwa ni kila Adhabu ya Viboko anayopewa Mtoto??
Au ukatili unapimwa kwa reaction ya mfanyiwaji bila kuangalia aina ya adhabu na Ukubwa wake??

Basi sisi kama wazazi wote ni wakatili Sisi Tunawaadhibu watoto wetu Kwa bakora zaidi ya Hivyo.

Huyo mwalimu Ametoa Adhabu ya Bakora za Mikononi ##Tano hadi Sita kwa Kila mwanafunzi (Hatujui kosa ni Nini labda tungejua kosa gani wamefanya Hao watoto labda tungeiona hiyo adhabu kuwa ni Ya kawaida tuu.

Shule za Serikali na binafsi adhabu ya Viboko bado ipo tena wanafunzi wanapigwa kwelikweli.

Nakumbuka nikiwa Shule Mwalimu alikuwa anaweza kumuadhibu mwanafunzi hadi bakora 20 yes 20 na ni kawaida tuu kwa walimu wa shule za Serikali sisemi ni sawa lakini Ni namna ya njia ya Kuwanyoosha Vijana iliyochaguliwa na Wahusika.

Ikiwa ni Hivyo jee Suala ya Bakora 5 au sita tena za Mkononi sehemu Salama kabisa itafsiriwe ni Ukatili!!! Labda kama tunataka kuwalea Watoto wetu kizungu alafu baade waje watushitaki ukimkalipia au ukimfokea kama walivyo watoto wa kizungu nowdays.

Jee tunataka tufike huko???
Bila kujali kosa la hao watoto hiyo adhabu ni kubwa kwao.

Nawashangaa sana ninyi mnaofananisha dunia ya sasa na hiyo ya miaka ya tisini.

Mfano kosa la uchelewaji, hilo kosa kwa miaka yetu ya giza utakumbushwa kwa viboko, ila siku hizi kuna means nyingi unaweza kuelekezwa zikakufanya ukawahi kuamka/kuwahi jambo fulani.

Hao madogo wamechelewa, mtoto kama huyo kuchelewa madrasa mara nyingi huwa sio kosa lake, kuna mwingine hapo kabeba kapu kabisa ikiwa na maana aidha akitoka hapo au alikotoka huko kahemea ndio kaenda madrasa.

Hivi kweli unashindwa kuicontrol akili ya mtoto hadi umpige, mbona akili yake unaisoma chap tu na kupredict his/her next move.
 
HAKUNA NJIA NYINGINE?
Unavyosema hakuna njia nyengine unafurahisha sana😄😄😄😄

1.Je hao waalimu mmewaanda kuwa walimu???
2.Tunapenda miujiza bila kuandaa process ya kuifikia!!!

Ndomaana ninasema kwa mazingira yetu watoto wachapwe tu,,,,hakuna namna wachapwe!!!! Elimu ya kubembelezana wanaweza wazungu tu ila sisi weusi hatuwezi kwakua hatujajiandaa kufanya hayo.
 
Sijamtetea mwalimu ila naongea kwa experience.

Kama umesomea hapa hapa Tanzania basi unajua mila na desturi za kitanzania( UVIVU NA UZEMBE).

Enzi zetu tupo shule mtu anajua saa moja kamili ndio muda wa kengele ya mstarini ila yeye anaamka saa kumi na mbili na dakika 55😀😀😀 akili za kiuanafunzi bila mboko na mwalimu kuliamsha huko mabwenini watu hawaendi paredi.

Kila siku mwalimu mkuu anaongea ila watu hawafati baada ya mboko na adhabu za nje na kukosa vipindi watu wakaanza kukaa kwenye mstari.Leo hii baadhi ya wale madoja ndio hawa wanatetea mtoto asiadhibiwe😄😄😄
Mzee hiyo clip ni ya madogo ambao hata miaka 10 hawana, hao magoja ndio sie ambao tulikua umri wa balehe. Na sio kua huko nyuma tulikua hatulimwi mboko, tulilimwa na tukazoea na tulikalili tukidakwa ni mboko then inaisha iyo.
 
Hujambo? Ahsante Sana kuniTag. Tayari jambo liko Polisi kwa hatua zao za uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na maafisa ustawi wa jamii. Watu tuwe na subira kwani, nyuma ya jambo moja aina kama hii, huwa kunakuwa na mengi mengine hivyo, tupewe nafasi tutimize wajibu wetu mliotupatia kuhusu sheria ya mtoto na 21 ya Mwaka 2009 na marekebisho yake yote.

Ahsanteni Sana

Madam, ningeshauri suala hili waelekezwe Bakwata wadili nalo kwa sababu vinginevyo jamii inaweza kutafsiri kwamba serikali inaingilia masuala ya Imani. Kwa sababu kutoa adhabu kwa watoto walio fanya makosa mbalimbali ya kinidhamu ni sehemu ya mafundisho ya dini.

Ni hayo tu🙏🙏🙏🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom