Vishu Mtata
JF-Expert Member
- Dec 15, 2019
- 15,954
- 35,415
Zamani mzee wetu alikua anatupiga sana, ila mwisho wa siku aliacha alipoona tunaelewa zaidi kwa maneno kuliko viboko na adhabu za kijeshi.Mwanangu humchapi hivyo na madrassa ndo basi tena,toka nizaliwe sijawahi piga kiumbe Cha kike Leo mwanangu unampigaje hivyo.
Mwalimu wenu wa madrasa ndo alikuwa anavua nguo anabaki na kaptura?Kusema ukweli utandawazi umeharibu maadili hivi hapo kina kipi cha ajabu? Kipindi tunasoma sisi mwalimu wetu alikuwa anakuvua kaptura unabaki na chupi ndo anakushushia mvua ya fimbo lakn hakuna kulalamika.
Lakin sasa hiv mnataka mtoto akikosea apetiwe petiwe acheni mambi yenu bwana nyie ndiyo mnasababisha maadili yanaporomoka
Aliyepost video na aliyechukua video yawezekana wamelelewa kimayai mayai sisi wengine tuna makovu ya njiti na kila kovu lina stori ya kusisimua.Atembelee mashuleni hasa za bweni uone jinsi wanafunzi wananyooshwa fimbo za mapajani dazeni dazeni kama kweli tunataka kupunguza ukatili.
Huna akili na mwanao huyo atakuja kuwa MALAYA aliyeshindikana.Mwanangu humchapi hivyo na madrassa ndo basi tena,toka nizaliwe sijawahi piga kiumbe Cha kike Leo mwanangu unampigaje hivyo.
Wewe acha kujifanya Gen Z wakati ni millenia au baby boomer๐๐๐Ninyi ndio mmeifanya hii nchi kua masikini mpaka kesho.
Yaani unachapwa uchi na unakaa kimya, mlikua mazombi wa namna gani aisee.
Kama wenye akili wote watatumia fimbo basi jamii hazina watu wenye akili.Kwa hiyo hapa ustaadhi anapambana na umalaya bahati njema binti yangu kaolewa mwenye heshima na taadhimaHuna akili na mwanao huyo atakuja kuwa MALAYA aliyeshindikana.
Sio kwamba wanaopiga watoto hawawapendi ila wanawajengea watoto adabu,heshima na utii wa yale wanayoelezwa na wakubwa wao.
Hata katika jamii kama hufati kanuni na taratibu utaadhibiwa na jamuhuri kwa kupelekwa mahakani na kufungwa.
๐๐๐Kwahiyo adhabu zipo tu usipomuadhibu wewe ULIMWENGU UTAMUADHIBU!!!
Kwani ulichapwa peke YAKO mkuu,hata sisi kizazi hicho tulikiishi.Halafu punguza jazba.Wewe acha kujifanya Gen Z wakati ni millenia au baby boomer๐๐๐
Enzi zetu unachapwa mbaya mbovu na hakuna mahali utashtaki.
Huu mmomonyoko wa maadili umeletwa na vilaza wanaofake maisha ya ulaya wakati mifumo yenu ni ya kimbwambwa.Acheni kutetea ujinga hauwafanyi kuonekana mnaakili ila mapunguani.
kuolewa sio mafanikio je huko kwenye ndoa mambo yanaenda???Kama wenye akili wote watatumia fimbo basi jamii hazina watu wenye akili.Kwa hiyo hapa ustaadhi anapambana na umalaya bahati njema binti yangu kaolewa mwenye heshima na taadhima
kama ulikiishi basi unajua msaada wa njiti katika kukushape uwe ulivyo leo.Kwani ulichapwa peke YAKO mkuu,hata sisi kizazi hicho tulikiishi.Halafu punguza jazba.
Hapana huyu mwalimu amepitiliza adhabu,Mie mwenyewe mtoto wangu niliyemzaa wa umri huo siwezi kumuadhibu kiasi hicho.Waaachie wenye Dini Yao wahukumu!
Hiyo mitoto yenu mnayoiabudu kuna siku ndio watakuwa viongozi na wananchi wa hii nchi ๐๐๐.Kwa trend inavyoonyesha hiyo mitoto iliyo na low IQ na EQ haitaweza kusurvive!!!Hapana huyu mwalimu amepitiliza adhabu,Mie mwenyewe mtoto wangu niliyemzaa wa umri huo siwezi kumuadhibu kiasi hicho.
Tusilee huu ujinga mtoto mdogo tena wa kike anapigwa kama mwizi?
Hujambo? Ahsante Sana kuniTag. Tayari jambo liko Polisi kwa hatua zao za uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na maafisa ustawi wa jamii. Watu tuwe na subira kwani, nyuma ya jambo moja aina kama hii, huwa kunakuwa na mengi mengine hivyo, tupewe nafasi tutimize wajibu wetu mliotupatia kuhusu sheria ya mtoto na 21 ya Mwaka 2009 na marekebisho yake yote.