Hiki ni nini? Naombeni ushauri nachanganyikiwa. Nimekopa Milioni 14 natakiwa kurudisha Milioni 39

Hiki ni nini? Naombeni ushauri nachanganyikiwa. Nimekopa Milioni 14 natakiwa kurudisha Milioni 39

screenshot_20230910-135725_1-jpg.2744908
Natamani nijue hii michezo naonaga tu watu wanapiga hela 🤭🤭
 
Nimevumilia ila nimechoka acha niwaambie, ndugu walimu nimekopa AbC bank shilingi milioni 14 nikatwe kwa miaka nane sawa na miezi 96, nakatwa shilingi laki nne na elfu 14 kwa mwezi.

Nimeshangaa kukuta kwenye salary slip deni ni milioni 39😥😥😥, nimelia sana yaani nakopa 14M narudisha 39?
Mimi kwakua nilikua nina dharula ya haraka sana nilienda ABC maana niliabiwa kule hauzunguki sana na nilipofika niliongea nao tu mda ule ule nikajaza fomu nikaondokq mkopo ukaingia kesho yake, najuta sikupata mda wa wenda kusoma makubaliano na wala hawakunipa nakala yoyote!

Hii sio haki serikali iko wapi jamani?

Nifanyeje naombeni ushauri wenu
View attachment 2744997

Una sain vip doc bila kusoma maelezo? Lipa tu.
 
Kwa kifupi hapo huna Cha kufanya,umesaini mkataba na hela umewekewa,ukirudi kwao ukasema unataka kulipa yote sahizi kwa mkupuo watakukwambia tupe 39m,unachotakiwa ni kujifunza tu kutokana na makosa
Tusimtishe hapo wamekosea, haiwezekani umdai 39 wakati ulimpa 14. Inatakiwa adaiwe 14 na riba ya wakati huo, ili akiamua kulipa kwa mkupuo analipa deni na kitu inaitwa early settlement fee.

Mleta mada dai mkataba wako angalia riba ni kiasi gani uza mkopo kwa mabenki kama CRDB then enjoy maisha. Usiwe mnyonge na mtumwa. Kukopa sio dhambi.
 
Hiyo ni riba ya uongo, maana ukipiga hesabu ya kiasi anachotakiwa kulipa baada ya miaka hiyo 8 unakuta riba ni zaidi ya asilimia 60
39000000-14000000=25000000
Interest ya bank=25000000Tsh/=
Interest=(principle*rate*time)/100

25000000=(14000000*rate*8)/100

25000000=140000*8*rate

Rate=25000000/1120000

Rate=22.321%
 
Hii tabia ya kuruka kote bila kusoma yaliyoandikwa hata serikali yenu inayo sana ndio maana mikataba inakuwa ya hovyo na mwisho mnalia na kusema tunasitisha mkataba halafu mnapigwa faini ya mabilioni

Tabia ya kusema nisaini wapi inawa cost wengi

Hata kwenye legal binding mnaangalia tu wapi wameandika I AGREE Mnabonyeza kitufe

Sasa wewe unakopa unakubali kurudisha kwa miaka 8 deni la 14m ulitegemea wakudai ngapi?

Ungesaini kurudisha miaka 2 ingepungua sana

Siku nyingine kopa unachoweza kumudu kwa mshahara wako usiwasikilize wanaokukopesha ni wajanja sana

Mataifa ya Ulaya mengi kwa sasa hulazimishwi wala kushawishiwa kisa tu eti una account nao hata kama huna kazi, hii ilikula kwao maana walikula hasara ya mabilioni na serikali imewaambia mtakopaji mtu hela nyingi ambazo hana uwezo wa kuzilipa wala hazilingani na mshahara wake?

Yote kwa yote kataa RIBA ni Haram
 
Acha dharau umbumbumbu wa fedha ni swala la mtu binafsi na watanzania walio wengi hawana elimu ya fedha usionee walimu eti kisa walimu wanaonekana kirahisi sababu ya wingi wao
Kama unaona Kuna la kukusaidia kwenye hili andiko langu chukua, litakusaidia for future, lakini kama huoni chochote Cha kukusaidia potezea. Wabongo tunapenda kujitutumua mafichoni pale wanapohisi hawaonekani au anavyoishi hapaonekani kwa wakati ule, ila ukimuweka kwenye vilengeo ni hopeless
 
Lakini ni hiyo si miaka 4, 96÷12=8 hii ni minane, labda wamekuchomekea unapokopa benknowa muda mrefu unalipa mpunga mrefu pia.

Ushauri wangu kama unaweza PATA pesa sehemu nyingene nenda kafute deni utalipa riba ya muda ulio kaa na pesa tu, kama kuna penalty itakuwa ndogo tu. Kuliko hili.
 
39000000-14000000=25000000
Interest ya bank=25000000Tsh/=
Interest=(principle*rate*time)/100

25000000=(14000000*rate*8)/100

25000000=140000*8*rate

Rate=25000000/1120000

Rate=22.321%
Ila ni too much Mkuu, yaani pamoja na Serikali kutoa riba nafuu kwa Mabenki ya asilimia 7 ila wao wanatupiga riba za 23% 🙆‍♂️🙌
 
Tusimtishe hapo wamekosea, haiwezekani umdai 39 wakati ulimpa 14. Inatakiwa adaiwe 14 na riba ya wakati huo, ili akiamua kulipa kwa mkupuo analipa deni na kitu inaitwa early settlement fee.

Mleta mada dai mkataba wako angalia riba ni kiasi gani uza mkopo kwa mabenki kama CRDB then enjoy maisha. Usiwe mnyonge na mtumwa. Kukopa sio dhambi.
Mkuu Early settlement fee kawaida inatakiwa isizidi kiasi gani?
Maana kuna loan officers janjajanja sana
 
Nimevumilia ila nimechoka acha niwaambie, ndugu walimu nimekopa AbC bank shilingi milioni 14 nikatwe kwa miaka nane sawa na miezi 96, nakatwa shilingi laki nne na elfu 14 kwa mwezi.

Nimeshangaa kukuta kwenye salary slip deni ni milioni 39[emoji26][emoji26][emoji26], nimelia sana yaani nakopa 14M narudisha 39?
Mimi kwakua nilikua nina dharula ya haraka sana nilienda ABC maana niliabiwa kule hauzunguki sana na nilipofika niliongea nao tu mda ule ule nikajaza fomu nikaondokq mkopo ukaingia kesho yake, najuta sikupata mda wa wenda kusoma makubaliano na wala hawakunipa nakala yoyote!

Hii sio haki serikali iko wapi jamani?

Nifanyeje naombeni ushauri wenu
View attachment 2744997
Ulipo jana form na kila mwezi unalipa 400k kwa mda wa miezi 96 hukupiga hesabu kuwa inakuja 38.4m ....hkuona hilo? ..... nahisi wew ndo una makosa
 
Kwanini usingeenda NMB au CRDB?
Bayport walinifata ofisini ili wanikopeshe nilipowauliza riba ni asilimia wakaanza chenga chenga braah braah kibao,nikambananisha mmoja wao akaniambia riba ni 47% nikawafukuza ofisini.
Sasa mbona hii ni karibu riba ya asilimia 200?
 
Back
Top Bottom