Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pole sana!! Kwa taarifa tu ni kwamba mimi ni afisa mstaafu kwenye utumishi wa umma. Ninaongea kwa uzoefu halisi!! Sehemu kubwa ya watumishi huwa na makato ya mikopo na mikopo juu ya mikopa hadi wanastaafu. Kosa walilifanya tokea mwanzo wa ajira!! Mwajiriwa mpya japo ana mshahara mdogo lakini ana uwezo wa ku-save pesa kama akikubali kuishi kimkakati (kuishi kama mtumwa mwanzoni ili aje aishi kama mfalme baadaye). Baadaye mtumishi akioa na kuanza kupata watoto watakaohitaji gharama za elimu, hapo ndo watu huanza kujiingiza kwenye mikopo!! Lakini kama alijinyima mwanzoni atakuwa na uwezo wa kusomesha, kujenga nyumba mdogo mdogo bila kukopa. Ukishindwa ku-save pesa mwanzoni na kujenga tabia hiyo, hutaweza ku-save pesa maisha yako yote hata kama mshahara utaongezeka sana. Ukipiga hesabu ya riba anayolipa mtu katika kipindi chote cha ajira ni zaidi ya sh 100,000,000/=, na akistaafu chini ya kikokoto kipya hiyo pesa hawezi kuipata kwenye mafao ya kustaafu!!Unaongea kirahisi rahisi tu nyie ndio watu hamjawahi kushika hela mnaongea kiubwete ubwete tu hapa
Ni kweli kabisaMkuu, mimi nafikiri huyu mtu anapaswa kuhurumiwa aiseee, pamoja na kwamba makosa ni yake
Hapa hakuna cha ushauri. Unatakiwa ulipe kama mlivyokubaliana. Ulitakiwa usome makubaliano. Kukatwa 414,000 kwa makato 96 ni sawa 39,744,000 414000X96 = 39,744,000).Nimevumilia ila nimechoka acha niwaambie, ndugu walimu nimekopa AbC bank shilingi milioni 14 nikatwe kwa miaka nane sawa na miezi 96, nakatwa shilingi laki nne na elfu 14 kwa mwezi.
Nimeshangaa kukuta kwenye salary slip deni ni milioni 39😥😥😥, nimelia sana yaani nakopa 14M narudisha 39?
Mimi kwakua nilikua nina dharula ya haraka sana nilienda ABC maana niliabiwa kule hauzunguki sana na nilipofika niliongea nao tu mda ule ule nikajaza fomu nikaondokq mkopo ukaingia kesho yake, najuta sikupata mda wa wenda kusoma makubaliano na wala hawakunipa nakala yoyote!
Hii sio haki serikali iko wapi jamani?
Nifanyeje naombeni ushauri wenu
View attachment 2744997
Bank na tasisi nyingi za fedha hasa hizi ndogondogo mikataba yao huwa wanaweka kipengele cha kwamba ukitaka kufuta mkopo ni lazima uwe umerejesha walau nusu ya muda wa mkopo. Hivyo usishangae akaambiwa alipe nusu ya 39m (~19.5) kama ndio kwanza kachukua mkopoHi si sahihi, ukweli ni unarusiwa kufuta au kuhamisha deni muda wowote kwenye hizi bank. Wanangalia mpaka Siku unafuta au kuhamisha bado unadawai Kiasi gani kwenye Ile principal (14Mil Kwa hii kesi) na penalty kama ipo, kumbuka kila mwezi unaporusha pesa unalipa sehemu ya principal+riba. Hii unaweza kuwa katika mtindo wa flat au reducing rate.
Haraka haraka HAINA baraka.hata Kama ulikuwa na dharula kiasi gani ungetulia maana issue yoyote ya PESA INAHITAJI UTULIVU NA UMAKINI.Nimevumilia ila nimechoka acha niwaambie, ndugu walimu nimekopa AbC bank shilingi milioni 14 nikatwe kwa miaka nane sawa na miezi 96, nakatwa shilingi laki nne na elfu 14 kwa mwezi.
Nimeshangaa kukuta kwenye salary slip deni ni milioni 39😥😥😥, nimelia sana yaani nakopa 14M narudisha 39?
Mimi kwakua nilikua nina dharula ya haraka sana nilienda ABC maana niliabiwa kule hauzunguki sana na nilipofika niliongea nao tu mda ule ule nikajaza fomu nikaondokq mkopo ukaingia kesho yake, najuta sikupata mda wa wenda kusoma makubaliano na wala hawakunipa nakala yoyote!
Hii sio haki serikali iko wapi jamani?
Nifanyeje naombeni ushauri wenu
View attachment 2744997
Mkuu ukiacha wanaokopa kununua magari hata ukikopa kimkakati ufanye biashara si mbaya. Shida huwa ni mtu anokopa ajenge akimaliza anatop up anunue gari.Deni lolote benki kama si kwa matumizi ya kibiashara ni hasara tupu!! Ili mtu afanikiwe kutokukopa benki inabidi awe na mkakati huo tangu mwezi wa kwanza wa ajira yake. Iko hivi: Amua kuishi kwa kadri ya kipato unachopata. Amua kuweka 250,000/= benki kama akiba ambazo uhesabu kuwa hazipaswi kuingia kwenye matumizi yako. Panga chumba cha bei rahisi kimkakati, kula kimkakati na vaa kimkakati. Ukifanikiwa zoezi hili kwa miaka 5 utakuwa una akiba ya sh 15,000,000/=.
Hapo unaweza kuanza kukopa toka kwenye akiba yako mwenyewe, na zoezi la kutunza 250,000/= kwa mwezi liwe endelevu muda wote uwapo kazini. Mkakati huu unawezekana tu kama ukiuanza mwanzoni kabisa mwa ajira yako. Usikubali kuiga maisha ya watu, unajua wenzio watakopa benki na kuanza kuendesha magari, kununua vitu vya kifahari nk, hao watakutisha kwa miaka 5 tu basi!! baada ya miaka 5 utakuwa na akiba ya kukutosha kufanya vitu vya kimaendeleo. Lakini usipokuwa na mikakati hiyo utajikuta unalazimika kukopa ili kupeleka watoto shule, kununua kiwanja na kuanza ujenzi wa nyumba!! Ukikwepa mikopo utaokoa mamilioni ya riba ambazo wakopaji hulazimika kulipa. Utafanikiwa kupata vitu walivyopata wenzio bila gharama ya riba.
Lakini ukijiingiza kwenye mikopo, utajikuta unakuwa mkopaji muda wote uwapo kazini. Unakopa marejesho kwa miaka 8 kabla hujamaliza unapata shida nyingine unafanya top up, na mchezo huo huendelea hadi mtu anastaafu. Hutakwepa kukopa kama hutafanya mkakati wa ku-save pesa from day one!!
Yote uliyosema ni sahihi ila KUO siyo dharura mkuu, itoe hapo kabisa. Ni ujuha mtu kujiingiza kwenye mikopo kausha damu ili apate pesa ya kuoaDharula ya haraka sana kama mleta mada anavyodai ni ugonjwa, kuoa, kufiwa/mazishi (fullstop). Haya ndo matatizo ya kiswahili hayaishi! Ujiingize kwenye kongwa la miaka 8 kisa dharula! Ungesema nimechoka kupanga na kulipa kodi nataka niamie kwangu ningekuona wa maana!
Labda wewe ndiyo una tatizo. Arudishe zilezile alikopa kwa mjomba, kaka, dada, mama, baba, babu au bibi!Hata wewe akili huna unakopaje Hela harafu unalipa zaidi ya Hela uliyokopa ety? Ungekuwa karibu yangu ungekula vibao
Mimi nilipoajiriwa, wakati huo tulikuwa tunapokelea mshahara kazini bila kupitia benki. Unasaini kupata mshahara kwenye pay rol kwa cashier. Hapo unaona net pay ya watu wote walio kwenye ukurasa wako wa pay roll. Sikuamini macho yangu!! Mimi ndio nilikuta nina net salary kubwa kuliko karibuni wati wote japo ishahara ya wengine ilikuwa mikubwa sana kuliko wa kwangu!! Nilishangaa sana!! Baadaye nikagundua kuwa karibuni kila mmoja ana makato ya mikopo ya benki au saccos!! Kabla deni halijaisha mtu analazimika kukopa tena kwa top up ili watoto waende shule!! Hayo ndiyo maisha ya watumishi walio wengi!! Makazini utakuta vijana wamepark magari ya kutembelea waliyoyapata kwa mkopo, mikopo yenyewe utakuta ni ya miaka 7+, kwa nje wanaonekana kuwa na maisha mazuri lakini9 kumbe walishaingia kwenye mtego na watajikuta ni wahanga wa mikopo maisha yao yote!!Mkuu uko njema sana kiakili nakupa maua yako. Na nawapa wazazi wako maua yao wamekuza mtu timamu na makini sana
BayportKwanini usingeenda NMB au CRDB?
Bayport walinifata ofisini ili wanikopeshe nilipowauliza riba ni asilimia wakaanza chenga chenga braah braah kibao,nikambananisha mmoja wao akaniambia riba ni 47% nikawafukuza ofisini.
Succoss ndo mdudu upi?Mmi nilichukua mkopo Kwa succoss 4ml Kwa maika 2 full burudan
Nakatwa 197470 per month
At the end ntalipa 4.75m
Kwanza deni lake kama hakuna adhabu na malimbikizo linatakiwa kusoma 14m tu.Unafikiri akiuza hilo deni crdb wtaandikaje kwenye salary slip?
Kama hivyo hiyo ni Riba ya kawaida na mabenki yote hutoa hiyo ribaRiba asilimia 13.79 KWA mwaka compund interest.