Hiki ni nini? Naombeni ushauri nachanganyikiwa. Nimekopa Milioni 14 natakiwa kurudisha Milioni 39

Hiki ni nini? Naombeni ushauri nachanganyikiwa. Nimekopa Milioni 14 natakiwa kurudisha Milioni 39

23% per year ni nyingi sana fair ni 12% fixed rate Kwa mwaka hio iwe funzo next time usikurupuke watu hutumia matatizo yako kama fursa
 
Kitu muhimu cha kujua ni kwamba muda unavyozidi kuwa mrefu, makato kwa mwezi yanakuwa madogo, lakini malipo kwa ujumla yanakuwa makubwa
 
Unaongea kirahisi rahisi tu nyie ndio watu hamjawahi kushika hela mnaongea kiubwete ubwete tu hapa
Pole sana!! Kwa taarifa tu ni kwamba mimi ni afisa mstaafu kwenye utumishi wa umma. Ninaongea kwa uzoefu halisi!! Sehemu kubwa ya watumishi huwa na makato ya mikopo na mikopo juu ya mikopa hadi wanastaafu. Kosa walilifanya tokea mwanzo wa ajira!! Mwajiriwa mpya japo ana mshahara mdogo lakini ana uwezo wa ku-save pesa kama akikubali kuishi kimkakati (kuishi kama mtumwa mwanzoni ili aje aishi kama mfalme baadaye). Baadaye mtumishi akioa na kuanza kupata watoto watakaohitaji gharama za elimu, hapo ndo watu huanza kujiingiza kwenye mikopo!! Lakini kama alijinyima mwanzoni atakuwa na uwezo wa kusomesha, kujenga nyumba mdogo mdogo bila kukopa. Ukishindwa ku-save pesa mwanzoni na kujenga tabia hiyo, hutaweza ku-save pesa maisha yako yote hata kama mshahara utaongezeka sana. Ukipiga hesabu ya riba anayolipa mtu katika kipindi chote cha ajira ni zaidi ya sh 100,000,000/=, na akistaafu chini ya kikokoto kipya hiyo pesa hawezi kuipata kwenye mafao ya kustaafu!!

Mtu anayefaidika na mkopo ni yule ambaye anaufanyia biashara tu maana kwa huyo riba italipwa na wateja wake!! Lakini unakopa ili kununua gari, kusomesha, kujenga nyumba ya kuishi, hapo hesabu ni maumivu!!
 
Nimevumilia ila nimechoka acha niwaambie, ndugu walimu nimekopa AbC bank shilingi milioni 14 nikatwe kwa miaka nane sawa na miezi 96, nakatwa shilingi laki nne na elfu 14 kwa mwezi.

Nimeshangaa kukuta kwenye salary slip deni ni milioni 39😥😥😥, nimelia sana yaani nakopa 14M narudisha 39?
Mimi kwakua nilikua nina dharula ya haraka sana nilienda ABC maana niliabiwa kule hauzunguki sana na nilipofika niliongea nao tu mda ule ule nikajaza fomu nikaondokq mkopo ukaingia kesho yake, najuta sikupata mda wa wenda kusoma makubaliano na wala hawakunipa nakala yoyote!

Hii sio haki serikali iko wapi jamani?

Nifanyeje naombeni ushauri wenu
View attachment 2744997
Hapa hakuna cha ushauri. Unatakiwa ulipe kama mlivyokubaliana. Ulitakiwa usome makubaliano. Kukatwa 414,000 kwa makato 96 ni sawa 39,744,000 414000X96 = 39,744,000).
 
Hi si sahihi, ukweli ni unarusiwa kufuta au kuhamisha deni muda wowote kwenye hizi bank. Wanangalia mpaka Siku unafuta au kuhamisha bado unadawai Kiasi gani kwenye Ile principal (14Mil Kwa hii kesi) na penalty kama ipo, kumbuka kila mwezi unaporusha pesa unalipa sehemu ya principal+riba. Hii unaweza kuwa katika mtindo wa flat au reducing rate.
Bank na tasisi nyingi za fedha hasa hizi ndogondogo mikataba yao huwa wanaweka kipengele cha kwamba ukitaka kufuta mkopo ni lazima uwe umerejesha walau nusu ya muda wa mkopo. Hivyo usishangae akaambiwa alipe nusu ya 39m (~19.5) kama ndio kwanza kachukua mkopo
 
Nimevumilia ila nimechoka acha niwaambie, ndugu walimu nimekopa AbC bank shilingi milioni 14 nikatwe kwa miaka nane sawa na miezi 96, nakatwa shilingi laki nne na elfu 14 kwa mwezi.

Nimeshangaa kukuta kwenye salary slip deni ni milioni 39😥😥😥, nimelia sana yaani nakopa 14M narudisha 39?
Mimi kwakua nilikua nina dharula ya haraka sana nilienda ABC maana niliabiwa kule hauzunguki sana na nilipofika niliongea nao tu mda ule ule nikajaza fomu nikaondokq mkopo ukaingia kesho yake, najuta sikupata mda wa wenda kusoma makubaliano na wala hawakunipa nakala yoyote!

Hii sio haki serikali iko wapi jamani?

Nifanyeje naombeni ushauri wenu
View attachment 2744997
Haraka haraka HAINA baraka.hata Kama ulikuwa na dharula kiasi gani ungetulia maana issue yoyote ya PESA INAHITAJI UTULIVU NA UMAKINI.
 
Deni lolote benki kama si kwa matumizi ya kibiashara ni hasara tupu!! Ili mtu afanikiwe kutokukopa benki inabidi awe na mkakati huo tangu mwezi wa kwanza wa ajira yake. Iko hivi: Amua kuishi kwa kadri ya kipato unachopata. Amua kuweka 250,000/= benki kama akiba ambazo uhesabu kuwa hazipaswi kuingia kwenye matumizi yako. Panga chumba cha bei rahisi kimkakati, kula kimkakati na vaa kimkakati. Ukifanikiwa zoezi hili kwa miaka 5 utakuwa una akiba ya sh 15,000,000/=.

Hapo unaweza kuanza kukopa toka kwenye akiba yako mwenyewe, na zoezi la kutunza 250,000/= kwa mwezi liwe endelevu muda wote uwapo kazini. Mkakati huu unawezekana tu kama ukiuanza mwanzoni kabisa mwa ajira yako. Usikubali kuiga maisha ya watu, unajua wenzio watakopa benki na kuanza kuendesha magari, kununua vitu vya kifahari nk, hao watakutisha kwa miaka 5 tu basi!! baada ya miaka 5 utakuwa na akiba ya kukutosha kufanya vitu vya kimaendeleo. Lakini usipokuwa na mikakati hiyo utajikuta unalazimika kukopa ili kupeleka watoto shule, kununua kiwanja na kuanza ujenzi wa nyumba!! Ukikwepa mikopo utaokoa mamilioni ya riba ambazo wakopaji hulazimika kulipa. Utafanikiwa kupata vitu walivyopata wenzio bila gharama ya riba.

Lakini ukijiingiza kwenye mikopo, utajikuta unakuwa mkopaji muda wote uwapo kazini. Unakopa marejesho kwa miaka 8 kabla hujamaliza unapata shida nyingine unafanya top up, na mchezo huo huendelea hadi mtu anastaafu. Hutakwepa kukopa kama hutafanya mkakati wa ku-save pesa from day one!!
Mkuu ukiacha wanaokopa kununua magari hata ukikopa kimkakati ufanye biashara si mbaya. Shida huwa ni mtu anokopa ajenge akimaliza anatop up anunue gari.
Pia inategemea n amshagara sababu utakuta mtu anapokea kidogo hata cha kusave hana.
 
Dharula ya haraka sana kama mleta mada anavyodai ni ugonjwa, kuoa, kufiwa/mazishi (fullstop). Haya ndo matatizo ya kiswahili hayaishi! Ujiingize kwenye kongwa la miaka 8 kisa dharula! Ungesema nimechoka kupanga na kulipa kodi nataka niamie kwangu ningekuona wa maana!
Yote uliyosema ni sahihi ila KUO siyo dharura mkuu, itoe hapo kabisa. Ni ujuha mtu kujiingiza kwenye mikopo kausha damu ili apate pesa ya kuoa
 
Hata wewe akili huna unakopaje Hela harafu unalipa zaidi ya Hela uliyokopa ety? Ungekuwa karibu yangu ungekula vibao
Labda wewe ndiyo una tatizo. Arudishe zilezile alikopa kwa mjomba, kaka, dada, mama, baba, babu au bibi!
 
Kwa kifupi Sana,baada ya wewe kusaini ule mkataba,loan officer aliitwa na kupewa glass ya wine wakajipigia cheers kabisa a huyu loan officer akifanya deal hizi mbili zaidi atapanda cheo,naomba watalam wa Benki walioajiliwa wamsaidie huyu mtu kiushauri je! Atafanyaje au ndo alipe Ila kwa msaada wa haraka ni yeye kurudi na kuusoma mkataba mwanzo mwisho aangalie km Kuna loophole yoyote anayoweza kutumia kutoka kwenye hiki kifungo
 
Mkuu uko njema sana kiakili nakupa maua yako. Na nawapa wazazi wako maua yao wamekuza mtu timamu na makini sana
Mimi nilipoajiriwa, wakati huo tulikuwa tunapokelea mshahara kazini bila kupitia benki. Unasaini kupata mshahara kwenye pay rol kwa cashier. Hapo unaona net pay ya watu wote walio kwenye ukurasa wako wa pay roll. Sikuamini macho yangu!! Mimi ndio nilikuta nina net salary kubwa kuliko karibuni wati wote japo ishahara ya wengine ilikuwa mikubwa sana kuliko wa kwangu!! Nilishangaa sana!! Baadaye nikagundua kuwa karibuni kila mmoja ana makato ya mikopo ya benki au saccos!! Kabla deni halijaisha mtu analazimika kukopa tena kwa top up ili watoto waende shule!! Hayo ndiyo maisha ya watumishi walio wengi!! Makazini utakuta vijana wamepark magari ya kutembelea waliyoyapata kwa mkopo, mikopo yenyewe utakuta ni ya miaka 7+, kwa nje wanaonekana kuwa na maisha mazuri lakini9 kumbe walishaingia kwenye mtego na watajikuta ni wahanga wa mikopo maisha yao yote!!

Sina matatizo na anayekopa ili afanye biashara!! Huyo wateja ndo watagharimia kurejesha mkopo na riba yake! Ilapo iwe ni biashara iliyofanyiwa utafiti na una uhakika faida kwenye biashara itatosha kurudisha mkop[o na riba yake na wewe ukabaki na faida!
 
Kwanini usingeenda NMB au CRDB?
Bayport walinifata ofisini ili wanikopeshe nilipowauliza riba ni asilimia wakaanza chenga chenga braah braah kibao,nikambananisha mmoja wao akaniambia riba ni 47% nikawafukuza ofisini.
Bayport
Platinum
OYA
Maboto

Hao wanatakiwa wapigwe vyuma hadharani

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Unafikiri akiuza hilo deni crdb wtaandikaje kwenye salary slip?
Kwanza deni lake kama hakuna adhabu na malimbikizo linatakiwa kusoma 14m tu.

Sasa kwa nini aliuze CRDB? Kwa kuuza deni lake CRDB anapata faida ya kuchajiwa riba ndogo zaidi ya asilimia 13 kwa mwaka. Effect ya riba pekee inatosha kushusha mzigo wa marejesho kwa takribani nusu ya gharama ambazo ABC watataka alipe.

Kwa kiasi cha 414,166 anayokatwa kwa mwezi kwa riba ya CRDB angetumia miaka 3 na miezi 7 kuclear deni na jumla ya marejesho na riba angelipa 17.6m pekee.

Kukopa ni hesabu, usikope bila kupiga hesabu vizuri
 
Back
Top Bottom