Hili draft la Dalmax la Google Play limenishinda aisee, hii app ina mchezo mkubwa sana

Duh mzee, hili gemu hatari! Lakin inabid niendelee kulicheza! KWENYE asilimia mia nimeweza kutoa sare mbili ,na vichapo vya kutosha! Ila nikajua kupunguza nikaja 70% hapo nimemchakza na alikuwa ana haha kutafuta suluhu zakufa mtu!
 
Watu mnajisifu mmelipasua mliowengi kwa sababu mmeweka asilia 100%, ila wengi kuna kitu mmesahau kuzingatia. Ukiweka hiyo 100% pia na ulipe muda wa kutosha wa hilo kufikiria, maximum sekunde 5 angalau hapo utajisifu bingwa, la sivyo unajidanganya mwenyewe. Unakuta wewe unafikiria sekunde 15 halafu hilo umelipa maximum sekunde 3 halafu unajiita bingwa! Halafu isitoshe una-undo! Mi nitakusifia tu kwamba ni mkali lakini sio bingwa kama hujazingatia hayo, kwa sababu hilo game hata uki-undo bado linakutoa jasho.
 
Mimi wakati nacheza nalo nilikuwa sifikirii hata sec5
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…