Hili la Bandari, lawama hii iende kwa hayati Magufuli

Tafadhali 0acha kuleta ujinga wako hapa kila kitu unataka kumuunganisha JPm na mabo ya yasiyofaa.

Jenga hoja kuonesha udhaifu wa uongozi uliopo. Mbona mbunge wa Ngorongoro ameungana na wananchi wenzie kuwatetea lakini serikali hii wanamkamata. Mzungumzie kiongozi aliyeko madarakani ndio chanzo cha yote siyo JPM.

Angekuwepo JPM kwanza yeye mwenyewe mkataba huo ungeletwa kwake au kushauri nafikiri angefunguliwa mashitaka kwanza na hata huko bungeni mkataba huo usingepelekwa maana angeutupilia mbali. JPM alipenda sekta binafsi ya Tanzania ishirikiane na wawekezaji kwa nia ya kuwapa ujuzi, uzoefu na kujengewa uwezo kuendesha shughuli za kiuchumi ili kipato cha pesa za kigeni zinufaishe taifa badala ya sasa.
 
Mkuu Diwani, kwanza kabisa chukuwa maua yako. Miundombinu ya kisiasa anayoitumia SSH, muasisi wake ni JPM. Siyo kwamba Magufuli aliengua wapinzani tu, hata huko kwenye chama chake alipitisha watu aliowataka yeye bila kuzingatia maoni ya wanaccm wenzake waliyoyatoa kwenye sanduku la kura za maoni.Kwake yeye mtu mwenye uwezo wa kuhoji na kukosoa hakuwa sahii kwake bila kujali chama anachotoka. Nikupe mifano michache ambako kura za maoni zilisiginwa: Shinyanga mjini, Kawe, Mwibara, Mueza...na sehemu nyingine nyingi tu. Kosa hili ni kweli analistahili pamoja watu wake waliokuwa wakimzunguka. Tulipokuja kwenye uchaguzi yalikuwa ni maigizo tu na kuumiza wapinzani bila sababu ya msingi. Nakumbuka bila aibu Bashiru Ally akiwa Mwananchi Communication alitamka bayana kuwa vyombo vya dola vitatumika kuisaidia Serikali ya Magufuli ktk uchaguzi na kweli ndicho kilichotokea. Kwenye campaign jpm alienda mbali na kuhaidi watu vyeo serikalini hata kama hawakuchaguliwa kwenye huo uchaguzi. Ni bahati mbaya tu hapa nchini kwetu utawala wa Sheria ulishasiginwa lakini uchagu huo haukuwa uchaguzi bali ujambazi wa uchaguzi.

Kwa hali ilivyokuwa, si vibaya kabisa kwa wale wenye maoni kuwa, JPM alikuwa akiweka miundo mbinu ya kubadili katiba hili apewe mitano tena. Japo alikuwa akijikataza lakini mazingira tayari yalikuwa wazi. Kauli kama vile za spika wa wakati ule "atake hasitake", kauli za kina Nkamia nk vilikuwa ni viashiria tosha ya kile kilichokuwa kikipikwa. Zaidi ya hayo JPM hakutaka kukosolewa wala kuhojiwa kwa kile alichokuwa akikifanya, hasa vile vyenye maslahi yake binafsi. Kwa mantiki hiyo alichaguwa wabunge ambao yeye angeweza kuwamdu. Kwa miundo mbinu hiyo aliyoiasisi JPM serikali ya Samia inatumia weakness hiyohiyo kupitisha mambo yake. Kwa maana nyingine bunge aliisadii Serikali, badala yake limekuwa kama mzigo kwa serikali kwasababu wanalipwa bila kutimiza wajibu wao kama wabunge. Hii inadhibitishwa na kauli ya Kinana aliyoitoa hivi karibuni akiitaka nec ya CCM imutake Rais kuwaondoa mawaziri wavivu na kukemea bunge lisipitishe kila kitu kinacholetwa na serikali bila kuhoji.

Siyo swala la mkataba wa bandari tu ambao umepita ktk hili bunge na kuleta malalamiko mengi ktk jamii. Nakumbuka tozo za ajabuajabu zilipitishwa na hili bunge hadi mitandao ya kijamii na vyombo vya habari ndo viligeuka kuwa bunge. Ni bunge la Magufuli, Bashiru na Polepole.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…