Hili la Bandari, lawama hii iende kwa hayati Magufuli

Hili la Bandari, lawama hii iende kwa hayati Magufuli

Mkuu, ulifikiri msra mbili kabla ya kuleta hili andiko lako?
 
Nimesoma Comments za wengi humu. Hakika, safari yetu bado. Matumaini yangu ni kuwa, safari inaendelea, na katika kuifikia hatma, tunapaswa kuwa na juhdi.

Mungu yupo nasi.
 
Wakati hao wapinzani wako wengi bungeni waliwahi kuzuia hoja gani isipitishwe na ccm!
Hata mimi nimeshangaa sana. Mleta uzi amenishanga kuja kuhusianisha na hili tukio la sasa na wahusika wakuu akiwaweka kando.
 
Bado sehemu mbalimbali za nchi yetu zinaendelea kujadili kuhusu Uwekezaji wa DP-World. Mbaya zaidi, mitazamo inayotolewa sasa inajadiliwa kwa milengo ya kidini, jambo ambalo si la kawaida katika nchi yetu.

Ni nini mzizi wa haya yote?

Kisa kilianza Mwaka 2020, wakati wa Uchaguzi Mkuu. Ulikuwa ni moja kati ya chaguzi ambazo zilijawa na malalamiko mengi kutoka upinzani, uvunjifu wa sheria za uchaguzi na kupeleka Uchaguzi ule kugubikwa na ripoti chafu za Waangalizi wa ndani na nje.

Lakini kwa nini haya yote yalitokea?

Haya yote yalitokea ili kutimiza adhma ya aliyekuwa Rais wa wakati huo Hayati, Dkt. John Magufuli ya kutaka kutengeneza Bunge la Jamuhuri ya Muungano lenye wanachama wa chama chake tu (CCM). Hili linathibitishwa na kauli yake aliyoitoa Tarehe 22 Januari 2020, alisema;

“Haiwezekani Mkurugenzi nikuteue mimi, nikulipe mini mshahara na kukujazia mafuta kwenye gari halafu kwenye Uchaguzi utangaze kuwa Mpinzani ameshinda”

Kauli hii ndio leo hii imesababisha leo bunge letu kuwa ni Bunge la chama kimoja. Hivyo, maamuzi yote kufanywa kwa kuridhisha chama na viongozi wake wakuu, wakiwamo Rais wa Jamhuri ya Tanzania kama Mwenyekiti wa Chama hiko.

Je, hasara ya jambo hili ni nini?

Hapa kwenye hasara ndipo kwenye lawama, Magufuli alituachia Bunge lisilo na meno, Bunge ambalo lingekubali kila kitu kwa kuwa kimekubalika na Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa chama. Bunge linalopitisha hoja bila kuchunguza kwa kina.

SUALA LA BANDARI SI LA KUJADILIWA VIJIWENI NA KWENYE NYUMBA ZA IBADA.

Haya maoni ambayo watu wanayajadili, vipengele ambacho vinatia shaka kwenye Mkataba, vilipaswa kujadiliwa bungeni kwa sababu, Bunge ndicho chombo pekee chenye Mamlaka ya kuongoza mijadala hii ambayo imezua gumzo, si kuacha mambo haya kwenda mpaka kwenye nyumba za ibada.

Naamini ya kuwa; kuna kundi kubwa la Wabunge ambao wanaamka sasa hivi kutambua kumbe kuna baadhi ya vipengele katika Mkataba vinazua utata, ila walivyokuwa bungeni, kwa sababu ya “Mob Psychology” wakakubali tu bila kuvitathimini ili vinapofika mtaani wananchi waelewe kuwa Bunge lao limejadili kitu gani kupunguza uwezekano wa kuzuka kwa utata huku mitaani.

Matokeo yake, suala hili linajadiliwa kidini leo hii. Tupo kwenye hatari ya KUGAWANYIKA.

JE, CCM HUJALI MASLAHI YA CHAMA KULIKO NCHI WANAYOONGOZA?

Ni rahisi sana kwa mtu yeyote kujibu swali hili kwa jibu la NDIO. Kwa sababu kuu mbili;

  1. Hoja nilizojadili hapo juu, naamini Hayati Magufuli wakti wa uhai wake hakufikiria madhara ambayo nchi ingeweza kuyapata endapo Bunge litaundwa kwa chama chake tu kupitia kupora Uchaguzi mkuu. Lakini hapa ndipo tulipofikia.
  2. Leo, tarehe 27 Agosti, Rais amekasirishwa sana na amepoteza imani na Mkurugenzi na Mkuu wa wilaya ya Mtwara, kwa sababu ya kushindwa kusambaza kadi za CCM kwa wananchi ambao kwa madai yake wanasema ni Upinzani. Amesema“Siwezi kustahimili kadi za chama zinarudishwa, Mkuu wa wilaya yupo, DED yupo, namtimua leo, kadi za chama zinarudishwa na watu wanashida anaulizwa nini, ooh! Unajua kule wengi wapinzani, so what? Watanzania wale, sina imani na mkuu wa Wilaya aliyesababisha kadi zirudishwe
Inaonyesha dhahiri kuwa, Rais ameumizwa kuona chama kinakataliwa na baadhi ya watu, ila sikuona hatua kama hii ikichukuliwa kwenye ubadhilifu ulioandikwa kwenye ripoti ya CAG.

Makosa yale aliyofanya Hayati, ya kutanguliza chama kisha Taifa. Anayafanya aliyepo sasa. Muda utaongoea.



Mwl. Diwani.



Acha unafiki wapinzani wameshaawwhi kuzui nini bungeni ili iwe ni mfano
 
Lakini amezungumzia hadi suala la kutumia mabavu kuhakikisha chama chake ndo kinakuwa na uwakilishi bungeni kitu ambacho kimepelekea kukosekana kwa wapinzani ambao wangepaza sauti bungeni kupinga mambo kama haya.

Ukiwa unatoa maoni yako ondoa hulka ya mahaba niue ndo utaiweka akili iwe huru ku argue mambo.
Kwani hayo mabavu ya Magufuli ndio yalipanda ndege kwenda Dubai kuwaleta waarabu wakapewa bandari milele?

Next time usikurupuke kujibu usichokielewa.
 
Leo, tarehe 27 Agosti, Rais amekasirishwa sana na amepoteza imani na Mkurugenzi na Mkuu wa wilaya ya Mtwara, kwa sababu ya kushindwa kusambaza kadi za CCM kwa wananchi ambao kwa madai yake wanasema ni Upinzani. Amesema“Siwezi kustahimili kadi za chama zinarudishwa, Mkuu wa wilaya yupo, DED yupo, namtimua leo, kadi za chama zinarudishwa na watu wanashida anaulizwa nini, ooh! Unajua kule wengi wapinzani, so what? Watanzania wale, sina imani na mkuu wa Wilaya aliyesababisha kadi zirudishwe
Inaonyesha dhahiri kuwa, Rais ameumizwa kuona chama kinakataliwa na baadhi ya watu, ila sikuona hatua kama hii ikichukuliwa kwenye ubadhilifu ulioandikwa kwenye ripoti ya CAG.
Wewe mpumbavu acha kupotosha. Rais alitoa hiyo kauli baada ya kukerwa na DC & DED waliokuwa wakichepusha miradi kutoka maeneo yaliyokusudiwa na kuipeleka kwingine ili kuwakomoa wakazi wa hayo maeneo ambao wengi wao ni wanachama wa upinzani. Waliokuwa wanarudisha kadi ni wanaCCM wanaoishi kwenye kata ambazo miradi waliyotegemea ije kuchepushwa. Sasa kama mwenyekiti wa chama unadhani atafurahishwa kuona wanachama wanarudisha kadi? Msipojibiwa mnapotosha sana. Kwa wapumbavu wengine wasiojielewa wataona umeandika point kumbe ushuzi mtupu
 
Upumbavu mtupu JPM kumweka kwenye huo upuuzi wenu!


Magufuli kasaini lini mkataba wa DPWORD?

Pumbavu kabisa!
Yeye si ndio alituletea huyu aliyesinya? Ina maana hakuona mwingine anayefaa zaidi yake?
 
Watu wana chuki. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom