Hili la kufungwa barabara limekaaje? Kwa namna hali ilivyokuwa leo kwenye usafiri maeneo ya Posta na Kivukoni mpaka ifike hiyo tarehe 30 tutakuwa hoi

Hivi kule kwenye mazishi yz Elizabeth UK walikojazwa kwenye bus hawakujifunza jambo?
 
labda Arusha.

Dodoma haina uwezo wa kuhost hao wakubwa
 
akili zao zimeishia kwenye kufunga barabara tu, hawana utashi mwingine hao
 
Kwani kabla ya bodaboda na bajaj tulisafiri vipi hapa mjini? Bodaboda na bajaj katikati ya jiji ni uchafu wafanye huduma zao nje ya city centre.
Na support asilimia. Hakunaga mji ulioendelea duniani ukiwa na bodaboda na bajaji kama usafiri wa umma.
Lawama zote ni kwa serikali kuingiza siasa kwwnye mambo ya msingi.

Mfumo wa BRT ndo ufanye kazi kwenye main roads...wakishindwa kuleta mabasi watafute watu binafsi wasafirishe abiria.

Huku wakija na mipango wa city light rails, trams,metros nk. We have to think big. Uwezo tunao.

Kama wanasema Riziki, riziki zipo tu...sidhani kuna mtu anapenda kuwa Bodaboda au dereva bajaji
 
Hivi kule kwenye mazishi yz Elizabeth UK walikojazwa kwenye bus hawakujifunza jambo?
Hata huko barabara zilifungwa, utofauti ni kwamba wako na barabara nyingi hivyo hakukua na tafrani kwa raia wa kawaida
 
Sasa muwape taarifa ma gabachori tusipoenda kazini wasipige
Shabaniiii mbona huji peleka watoto shulee
 
Hata wakifunga wana options nyingi ingawa huu upuuzi hamna. Si uliona mazishi ya Lizzy hawa wanaofunga njia leo walipakiwa kwenye daladala na walitulia tuliiii.
Hivi lile daladala walilopakiwa, if I'm not mistaken, hata dereva hawakupewaga; walijitafuta wenyewe from airport hadi mitaa ya ushuani. Wanashindwa nini kufanya hivo wakiwa kwao as well? I mean, hapa nyumbani tungeboresha zaidi; tafuta Youtong moja la maana, au Makpolo halafu kamamda 1 ana drive hilo with full of ulinzi na escort ya maana, tukio linakua la mara moja then wananchi wanendelea na shughuli zao, wakitaka kutoka, zoezi linafanyika hivo hivo, I think lisaa limoja tu lingekua linatosha
 
K
Kila kitu kiliandaliwa na mwenyeji wao.
 
Mkuu hufungwa kwa muda tu, pale msafara wa viongozi wanapotaka kupita, na ni kwa wale wenye vyombo vya moto na baiskeli tu, kwa watembea kwa miguu huruhusiwa kuendelea na shughuli zao kama kawaida, baada ya msafara kupita na askari wa usalama barabarani kujiridhisha kuwa hakuna ratiba nyingine ya msafara wa viongozi basi barabara hufunguliwa mara moja kuendelea na shughuli za kiuchumi, nimeona kwa macho yangu hapa Keko mataa, msafara unapita Nyerere road kutoka Nyerere Air port na kupita barabara ya kati ya mwendokasi kuelekea IKUL.U haupiti juu ya (fly over) daraja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…